beef kati ya Ludacris na Drake lachukua sura mpya

Big Sean,Drake and Ludacris
Drake


Drake na Ludacris




rapa DRAKE wa young money, amejibu matusi yaliyoimbwa na Luda criss kwenye track yake mpya ya badaboom ambapo Kwenye track hiyo, Luda japo hajawataja majina aliwadiss drake na big sean kutokana na kelele zao walizokua wanapiga kwamba kawaibia style yao ya kurap na kuitumia kwenye track yake ya my chic bad.
Baada ya hiyo track ya diss ya Luda kutoka juzi kupitia mixtape yake, big Sean alijibu kupitia interview na kusema Luda ni mmoja kati ya marapa wakubwa sana na anaowaheshimu ambapo Muda mfupi baadae pia drake alimuandikia big sean kwenye twitter kwamba, natamani hawa marapa wakongwe wangeacha kutufatafata, sasa nani nitakae muamini mwaka 2012, hakuna hata mmoja, hata mimi mwenyewe sijiamini… alisema drake ambae kuhusu kuibiwa stile na luda, amesema sio kwamba hamheshimu Luda, “ila stile yangu ya kurap ni marapa wachache sana wanaoweza kuflow nayo, na ninachukia sana marapa ambao hawaiwezi alafu wanaing’anga’nia” hiyo ni kauli aliyoitoa DRAKE akihojiwa MTV.
Beef yao inazidi kukua sasa hivi baada ya Ludacriss kuwachana mwishoni kwenye video yake mpya, ambapo amesema hamna vyeo vyovyote kwenye huu muziki, wakati mwingine mkiwa na chakusema kuhusu mimi, nifate iwe uso kwa uso na sio kwenda kuandika kwenye twitter..




source:http://millardayo.com

No comments:

Post a Comment