Showing posts with label stories. Show all posts
Showing posts with label stories. Show all posts

Jose Chameleone msanii pekee atayeiwakilisha Afrika Mashariki katika UZINDUZI wa michuano ya LONDON OLYMPICS 2012



Jose Chameleone amepata dili la kuperform kwenye uzinduzi wa michuano ya olympic jijini London
Jose alipata dili hilo kupitia kampuni yenye makazi yake nchini Afrika kusini inayojulikana kama AS Entertainment.Kampuni hiyo ndio iliyompatia deal msanii huyu mwaka 2010 katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Afrika kusini
Kampuni hiyo bado inafanya mazungumzo na Jose kiasi gani anatakiwa kulipwa kwenye show hiyo
na Jose ndio msanii pekee ambaye mpaka sasa inaonekana atashiriki kwenye uzinduzi huo akitokea Afrika mashariki
michuano ya London Olympics inatarajia kuanza 25July kwenye saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku with two football matches of women's preliminaries at Millenium Stadium, Cardiff

Suma Lee afiwa na mama yake



Msanii wa kibao kilichoshinda wimbo bora wa Afro Pop na Wimbo wa Mwaka kwenye Kili Tanzania Music Awards 2012, Suma Lee, amefiwa na mama yake mzazi Muhimbili jana.
Mama yake Suma, ambaye alifikwa na mauti katika hospitali ya Muhimbili, alikua akiugua maradhi ya kiharusi.
Tunaiombea familia ya Suma, Faraja katika kipindi hiki kigumu,na kuiombea roho ya marehemu ilale mahali pema peponi, Amin.

WASHINDI WA TUZO ZA KILI

     1. WIMBO BORA WA RAGGAE
ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL
MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA
DUSHELELE BY ALI KIBA

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI
VIFUU UTUNDU BY A.T

5. WIMBO BORA WA TAARABU
NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI)

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI
DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA

7. WIMBO BORA WA AFRO POP
HAKUNAGA BY SUMA LEE

8. WIMBO BORA WA R&B
-NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL

9. WIMBO BORA WA HIP HOP
MATHEMATICS BY ROMA

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER)

11. RAPA BORA WA BAND
KALIJO KITOKOLOLO

12. MSANII BORA WA HIP HOP
ROMA MKATOLIKI

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA
 NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
KIGEUGEU BY JAGUAR

15. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE
KHADIJA KOPA

17. MTUNZI BORA WA MWAKA
    DIAMOND

16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
DIAMOND

18. PRODUCER BORA
MANECK

19. VIDEO BORA YA MWAKA
MAWAZO BY DIAMOND

20. WIMBO BORA WA MWAKA
HAKUNAGA BY SUMA LEE

21. HALL OF FAME
     TAASISI JKT

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI
      KING KIKII

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI
     DR. REMMY ONGALA

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE
     LADY JAY DEE

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME
      BARNABA

chek maandalizi ya KILIMANJARO MUSIC AWARDS

yatakayofanyika ndani ya ukumbi wa mikutano wa mlimani city mall







na hapa chini tujikumbushe na categories




nawatakia washiriki wote mafanikio mema...
tukutane kesho mapeeeema humu bloguni kujua ipi imekwenda wapi...

R.I.P STEVEN KANUMBA

ALICHOKIJIBU AFANDE BAADA YA CHIDI BENZ KUMJIBU




Baada ya juzi CHIDI BENZ kukubali kwamba
 pamoja na AFANDE SELLE kumdis, yeye bado 
yuko tayari kufanya nae kolabo ambayo alipanga
 kufanya na Afande wiki moja au mbili kabla hajamdis,
 Afande nae ametoa sentensi ya jibu kutokana na alichosema 
ChidiBeenz.
Afande amesema “yeah mi niko tayari, niko pamoja nae Chidi
 anajua hilo, na hiyo kitu alishaniambia kitambo tukapanga na
 mimi bila shaka matatizo yaliyotokea ni mambo ya kupita lakini
 mimi wimbo wake hata kesho nasububiri beat niandike tufanye 
kitu kilichobora zaidi nafikiri itakua na maana kuliko malumbano 
malumbano yanayoendelea haya sio mazuri, sina beef nae”
Chanzo cha beef yao ni baada ya Afande kuhojiwa East Africa 
Radio na kufananisha kuondoka kwa Ditto  watu pori kwenda
 La Familia, sawa na kuondoka Manchester United na kwenda 
timu ndogo kama Bolton, maneno ambayo yalimkasirisha sana Chidi Benz.
story na milardayo.com

Je! Beef hii ni Dar dhidi ya Arusha?




“These rap cats softer than a new born baby bottom... Eti big fish in this ocean... My pussy cat eats that shit..” Ni maneno yanayosemeka katika ukuta (wall) wa Harry Kaale maarufu kwa jina la One The Incredible aka Moko wa Miujiza. Ni fataki alilolielekeza kwa Joh Makini kuashiria kuwa vita katika ya Weusi kundi huru linalojumuisha rappers kutoka Arusha ambao ni yeye mwenyewe Joh, nduguye Nikki wa Pili, Gnako, Bonta aka Maarifa, Lord Eyez na wengine dhidi ya Nikki Mbishi aka Baba Malcom na One the Incredible na washirika wengine wa Lunduno na Illmatic imeiva.     
     
Chanzo cha ugomvi huu wa kimuziki kati ya pande hizi mbili unaaminika kuanza katika kipindi cha mwaka mmoja na kitu uliopita.  Katika mazingira mengi ya kuzuka kwa beef za hiphop mashabiki huwa na asilimia nyingi za kwao zinazopelekea wasanii fulani kupaniana kiushindani hali inayosababisha beef ya kawaida ama kali. Jina la “Nikki”ni sehemu moja wapo ya kuwepo kwa tension kati ya Nikki wa Pili na Nikki Mbishi. Watu walianza kumsikia kwa ukamilifu Nikki wa pili katika wimbo alioimba na ndugu yake Joe Makini “Niaje ni Vipi” . Hapo ndipo mashabiki wa hiphop Bongo wakatambua kuongezeka rasmi kwa orodha ya wasanii wenye uwezo mzuri kiuandishi nchini wanaotokea Arusha. Baadaye Nikki wa Pili alisimama mwenyewe kwenye ngoma aliyomshirikisha Rama D “Good Boy”.
Kwa upande wa Nikki Mbishi, safari yake ya kuwa nyota katika hiphop ilikuwa tofauti kidogo. Yeye alianza kujulikana nchini kabla hata hajaachia wimbo uliorekodiwa na kusambazwa katika mkondo mkuu wa muziki wa Tanzania. Nikki Mbishi alijizolea umaarufu katika kipindi cha Bongo Flava cha Clouds Fm kwa uwezo wake wa kuchana ,mitindo huru (Freestyles). Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu kwa ukaribu, wanasema Nikki Mbishi ana uwezo wa kurap kwa freestyle kwa masaa kadhaa bila kurudia mada na ndiye msaani ambaye One anamhofia kuliko wote nchini.

Baada ya kuvikwa taji la mchanaji bora wa mitindo huru enzi hizo, Nikki Mbishi aliongezea msumari mzito kwa mashabiki wake katika wimbo wake wa “Punch za kwenye Line”  Kama jina la wimbo unavyojieleza, wimbo mzima ulijaa uandishi mzito unaohitaji muda mrefu kuchambua na kupata maana halisi ya kila alichokuwa anatema (spit), sifa ambayo imekuwa ikipelekwa pia kwa maswahiba wake One na Stereo. Mashabiki wa wasanii hawa wanaofanana majina ya mwanzo wakawa na shauku ya kujua uwezo wa kila mmoja ili kupata jibu na ni mkali zaidi ya mwenzie. Jibu wanalo mashabiki wenyewe. Lakini hapo ndipo story hii iliyotawala vinywa vya mashabiki wa hiphop nchini, vituo vya radio na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa sasa kuhusu beef kati ya Weusi na Nikki Mbishi na One ilipopandikiza mbegu zake.

Kwa mujibu wa story za chini kwa chini ni kwamba Nikki Mbishi alimshirikisha Rama D kwenye chorus ya Punch za Kwenye Line lakini baadaye Rama D akaomba kuondolewa sauti zake kwenye wimbo huo kwakuwa hakutaka kugombana na Joh Makini ambaye inasemekana hakuwa anampenda Nikki Mbishi. Kutokana na uamuzi huo wa Rama D, Duke ambaye ndo producer wa wimbo huo pamoja na uongozi wa MLAB wakaamua kumchukua Grace Matata kufanya chorus. Kwao MLAB huo ulikuwa ni uamuzi uliofanyika kwa kutopenda kwakuwa Grace kipindi hicho alikuwa bado msaani mchanga na asiyejulikana kwa wengi kama ilivyo sasa.

 Baada ya hatua hiyo kukaanza kuzuka maneno kutoka kwenye kambi ya River Camp Soldiers na kuonekana kuwepo uwezekano wa kambi hiyo kuwadiss Lunduno (kundi huru lililopo maskani wanapotokea Stereo na nikki ambao kwa sasa wamejitoa). Kambi ya Lunduno kupitia One ikatupa jiwe lake kuelekeza kwa River Camp soldiers ambao kwa sasa wapo ndani ya kundi kubwa linalowajumuisha pia member wa Nako 2 Nako liitwalo “Weusi”.

Kwa mujibu wa mahojiano na Clouds FM, One alidai kuwa alirekodi wimbo katika studio za Tongwe Records ambayo kuna mstari unasema siwezi kuuza kura yangu kama Bonta akimaanisha wimbo wa Bonta uitwao “Nauza Kura”. Pamoja na dongo hilo lililoekezwa kwa Bonta, hakuna jibu la wazi kutoka kwa Bonta zaidi ya kujibu “Sina tofauti nao” alipoulizwa kuhusu msimamo wake.

Katika mahojiano hayo One alisema anashangaa kujikuta yupo kwenye beef na Weusi wakati anawasiliana mara kwa mara na Joh Makini pamoja na Lord Eyez ambao kwake ni kama kaka zake kimuziki. Japokuwa kauli hii ya One inakinzana na status yake hapo mwanzoni kabisa mwa makala haya ambapo anamdiss wazi wazi Joh Makini.

Mahojiano hayo yalifanyika kutaka kuwepo ufafanuzi kuhusiana na status ya facebook aliyoiweka jumatano (28/03/2012) iliyosema: “Niki wa pili: sijakutaja, usijihusishe, this is none of your biz..Do you homo…”



One alifafanua kuwa sababu ya kuandika status hiyo ni kutokana na hatua ya Nikki wa pili kumtumia ujumbe Nikki Mbishi ambao Mbishi alimfowadia ukisema kuwa wao akina One bado ni wadogo kwenye muziki na hawawezi rap, pia album ya Mbishi inasound kama single moja.

Kuhusu namna anavyowachukulia members wa Weusi, One anasema “Ni wazi kuwa siwakubali Weusi, si kama nawakosea heshima bali ni jibu nitakalokupa kama ukiniuliza kama shabiki, mimi si shabiki wao, Ujue nina waheshimu wao kama kundi lenye mafanikio kulingana na kile wanachofanya, hivyo hiyo ni heshima kubwa niliyonayo kwao lakini mimi si shabiki wao” (phatbeattz.blogspot.com).

Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kutomkubali Bonta kama msanii hali inayoashiria kuwa ni ngumu kwa Bonta ama Weusi kwa ujumla kukaa kimya; “Ninaposema Bonta hayupo conscious namaanisha kuwa naheshimu anachofanya, ana ujumbe wa maana lakini uwasilishaji wa ujumbe wake kwa umma ndio tatizo. Kwa neno moja naweza kusema Bonta ni MC mbovu,na ninaposema hivyo namaanisha kuwa hajui kurap, anachofanya nikuongea na wakati mwingine anapata beat nzuri za kuongelea. Nadhani huu ni muda wa kuwaambia ukweli” (phatbeattz.blogspot.com)

Hata hivyo kama mwenzie One, Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kung’ata na kupuliza kuhusiana na suala hili “if my mind is a belly then am bellyful I don't think if there is a space to put this cow meat a.k.a BEEF......”

Tayari mashabiki wa pande zote mbili wameanza kujihusisha moja kwa moja kwa kutoa mawazo yao katika kurasa za wasanii hao. “Tunachoshindwa kuelewa wabongo siku zote ni hiki.., Ukweli haui-justified kwa pesa, umaarufu na ujanja ujanja wa maneno. Muziki utabaki kuwa Muziki. Hip Hop itabaki kuwa Hip Hop. Kama "samaki Kwenye Hii Bahari" atazingua.., "tunamvua" tu kwani niaje...!? SUPPORT KWA Nikki Mbishi BabaMalcom NA WOTE WANAOSIMAMA FOR HIP HOP!!!”  


Wengine wameshindwa kuzuia chuki zao na kuandika maneno makali dhidi ya Weusi kuonesha namna wanavyoiunga mkono kambi ya akina Nikki Mbishi. “Watajichubua tu hao weusi. Watoto wazuri wanajiita weusi, hatutaki matozi. One, stereo na Nikki Mbishi wana big screen inayoönyesha u2po wa mabitch weusi. One wagonge ta**o, Nikki mbishi, wachinje huku wanakuchea, stereo watie vitasa watoto wanazingua”.

Vyombo vya habari husasan radio ambavyo siku zote vinaongoza kwa kukuza beef za aina hii vimechukua nafasi zao kwa kufanya mahojiano kupata ufafanuzi juu ya suala lenyewe hali inayolikuza zaidi.

 MLAB ambayo ni nyumbani kwa One, Nikki Mbishi na Stereo imeonesha kutofurahishwa na beef hiyo inayoendelea kukua kwa kasi. Meneja wa wasanii na Studio wa MLAB Patrick Gondwe amemuomba Nikki Mbishi kuachana na beef hiyo.  “ Kama kaka, nakuomba kuachana na suala hili Nikki! Kambi zote mbili ziache kuwagawa mashabiki…..Wapo kwa ajili yetu na hilo ni suala muhimu… Hatutakiwi kutawaliwa na vyombo vya habari.. Siku zote habari mbaya ni habari njema kwao….kutatokea mengi ya kuchanganya  lakini mwisho wa siku sisi tutapoteza mara mbili. Tukubali kukosa (lose) kwa kutokuandika vitu hasi kwenye mitandao ya kijamii na kuziba midomo yetu dhidi vyombo vya habari kuhusu suala hili. Nakuomba sana”

Uamuzi wa kukaa kimya kwa pande zinazohitirafiana unaweza kuwa na faida na hasara. Faida ni kuwa mashabiki wa pande zote mbili watapata fursa ya kuujua ukweli wa jambo lenyewe na kutafakari. Kwao Weusi na akina Nikki Mbishi wanaweza kutumia mahojiano na vyombo vya habari kuzuia kuwagawa mashabiki wao. Hasara ni pale ambapo pande hizi zitajikuta zikitumiwa na radio ama watu wenye lengo la kufanya biashara kupitia mgongo wao. Mfano halisi ni jinsi Darlive ilivyotumia beef ya Roma na Izzo kibiashara.

Kama beef hii ikiendelea kukua madhara yake yataenda mbali zaidi ya hapa ilipo. Beef hii inahusisha wasanii wanaowakilisha mikoa mikubwa yenye ushindani katika muziki wa hiphop, Arusha na Dar es Salaam. Kwa muda mrefu Arusha imekuwa ikitajwa kuwa ngome imara kwa hiphop nchini hivyo beef hii inatoa picha ya wazi ya ushindani kati ya Arusha na Dar es Salaam.

 Hatari ni pale mashabiki wa pande hizi mbili wakigawanyika katika misingi ya kimkoa. Ikiwa hivyo itakuwa ngumu kwa wasanii kama One, Nikki Mbishi na Stereo kwenda Arusha kufanya show wakihofia usalama wao. Historia ya mkoa wa Arusha inatueleza ni kwa kiasi gani watu wa huko walivyo na ushirikiano katika kupinga kitu wasichokipenda. Japo katika hiphop beef zina umuhimu wake, tuombee Mungu beef hii isije kufikia hatua ya watu kupigana wanted katika maskani zao bali kuwapa hasira za kiuandishi wote wanaohusika na mwisho wa siku kuwapa mashabiki muziki mzuri.


Fredrick Bundala aka Skywalker

Tone Radio

www.toneradiotz.com

MPIGIE KURA MTANZANIA MWENZETU ILI ASHINDE SHINDANI LA MODAL24 LINALOFANYIKA NEW YORK, MAREKANI






Mpigie kura Mtanzania mwenzetu ili aweze kushinda shindano la modeling la kutafuta modal24 kwa ajili ya kufanya photo shoot ya bilboard New York, Marekani.

Katika shindano hilo linajumuisha washiriki wapatao elfu moja (1,000) na katika watu hao yeye yupo katika nafasi ya tisa kati ya watu elfu moja.

Jinsi ya kumpigia kura ingia web; www.project.badoo.com, utakuta picha ya Joseph Adriani unachotakiwa kufanya ni kulike hizo picha au link (theproject.badoo.com/gallery).

Huyu ni mwanamitindo wa kwanza wa kiume ambaye anafanya kazi zake nje ya Tanzania naomba tumsaidie ili aweze kufika malengo yake. Joseph Adriani alishawahi kufanya muziki na alishashiriki katika shindano la Bongo Star Search 2008 na alifanikiwa kuingia katika 10 bora.

R.I.P E-Sir



Issah Mmari


Born Issah Mmari, on May 20, 1981 in California Estate, and raised in South c estate Nairobi, Kenya, E-Sir was a Kenyan hip hop artist signed to the Ogopa DJs label who was famous for his deft lyrical ability and command of the Swahili language. He is still widely regarded as one the best rappers to emerge on the Kenyan hip hop scene. He first came to be known in 2001 by his song "Jo", a song done in the same style as Black Rob's "Whoa." The song proudly declared E-Sir's arrival on the Kenyan music scene and was featured on the Ogopa DJs debut album . He went on to release his debut album "Nimefika" in 2003 which was a big hit with virtually all the songs on the album becoming radio singles. He won 4 categories in the 2003 Kisima Music Awards.
E-Sir died in a road accident on March 16, 2003, while in the company of fellow label mate Nameless. He was on his way back from a concert in Nakuru town that was to help promote the album. His fans were shocked and grieved for days on end after hearing the news of his death. His death was considered coming at a time when his career was starting to take off. His other hits include "Mos Mos," "Boomba Train," "Hamunitishi" and "Leo ni Leo." His only posthumous song was the collaboration between him and Nameless called "Maisha".
E-sir's younger brother Habib is also an upcoming rapper in the Kenyan music industry. He has couple of singles to his name, some of them with his partner Manga
     

    

Quick Racka ku''hit the floor'' hivi karibuni



MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Quick Racka, amesema kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘On the floor’, ambayo itakuwa maalumu kwa kwa ajili ya mashabiki wake wa klabu.


Msanii huyo alisema kuwa wimbo huo utaenda sambamba na video ambapo baada ya kukamalisha video ya ngoma yake ya ‘Fire Atherm’ kazi ndiyo itakuwa inafuata.


Alisema ameamua kutoa ngoma hiyo kwa ajili ya mashabiki wake kwani ni wimbo ambao utakuwa unachezeka hata sehemu zote hasa kwenye kumbi za starehe kama vile klabu.


Hata hivyo aliongeza kuwa kikubwa anachotaka kufanya ni kutoa ngoma mbili ambazo ni hizo ‘On the Floor’ na ‘Fire Atherm’, ikiwa sambamba na video zake.


“Maandalizi yapo na ngoma hiyo mpya tayari inakamilika lakini kikubwa nachotaka kufanya ni kutoa zote kwa mpingo pamoja na video ili tu mashabiki wangu waweze kuona nini kinachoendelea katika muziki wangu,’ alisema.

Na Laurent Samatta wa Dartalk.com

chek na lyrics ya wimbo wake wa

DIAMOND KUIMBA TAARABU






MSANII anayewika kwa sasa wa muziki wa kizazi kipya bongo, Diamond, amesema kuwa anafikiria kuimba nyimbo za taarabu baada ya kukosa mpinzani kwenye bongo fleva.

Aidha alisema kuwa katika muziki wake hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango alichokuwa nacho kwani katika kuthibitisha hilo ndani ya nyimbo zake hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha.

Aliongeza kuwa kikubwa kinachomsukuma kufanya kila aina ya muziki ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho kwani hakuna kitu anachoweza kushindwa kutokana na uwezo aliyokuwa nao.

Msanii huyo aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.

“Naweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watastuka sana,” alisema.

Hata hivyo alipoulizwa kama anatshirikiana na wasanii wakongwe wa nyimbo hizo za mipasho, alisema kuwa kwanza atasimama mwenyewe lakini baada muda ataweza kuwashikisha vichwa kama Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na wengi kibao.

Na Laurent Samatta wa Dartalk.com




baada ya Asha Baraka kulalamika bosi wa mashujaa afunguka

baada ya boss wa band ya AFRICAN STARS (Twanga Pepeta) Asha Baraka kulalamika kwamba amekua akipokea vitisho vya msg, kupigwa chupa za uhai huku akidai pia kwamba watu kutoka vingunguti asiowafahamu walimfata dukani kwake na kumzomea, Vitisho ambavyo alisema vinatokana na Boss wa Band ya Mashujaa Opajo Hosea kuhusika kutuma hao watu.

Sasa leo Max ambae ni kiongozi mkuu wa band ya Mashujaa amesema maneno haya “nazikanusha hizi taarifa, Asha Baraka nadhani yeye ni mcha Mungu, aseme Ukweli tu manake sababu kubwa iliyozaa haya yote ni wanamuziki tuliowachukua kutoka TWANGA PEPETA ambapo mtu ambae alitakiwa kusema anatishiwa ni sisi kwa sababu ndio tumemchukulia wanamuziki, yani hii inaonyesha mama huyu ana tapatapa”

Max amesema kwamba “anaipandisha tu Mashujaa kwa kuiongelea, nafikiri angekaa kimya manake alikua yuko juu na sasa hivi anaanza kushuka, ajipange yeye na timu yake waangalie ni wapi wamekosea na sio kuleta challenge za kitoto namna hii, na kwa kuongezea tu wanamuziki wote ambao tumewachukua Twanga wao ndio walihitaji kazi Mashujaa”

yaibuka mapya katika beef la Prezzo na Jaguar



habari ambayo inavuma sana nchini Kenya kwa sasa, ni kuhusu staa wa single ya kigeugeu msanii Jaguar kuibuka tena na kumzungumzia hasimu wake CMB PREZZO, lakini sasa hivi amefunguka zaidi kuhusu kundi la MMG alilolianzisha Prezzo na kuungana na rappa mwenzake aitwae Cannibal.

Jaguar amesema “ni vizuri lakini mi sipendi jinsi wanavyomkopi Rick Ross na Cannibal kumkopi Lil Wyne, mimi ninaheshima sana kwa Cannibal ila alinistua sana kujiunga na kusainiwa na Prezzo, Cannibal ndio anatakiwa kumsain Prezzo na sio Prezzo kumsain Cannibal, Prezzo anapenda sana kukopi kwenye MMG yeye ni Birdman feki na Cannibali ni Lil Wyne, mimi ni rafiki sana na Cannibal na tunaongea kila siku ila amenishtua sana''

Kuhusu Beef yake na Prezzo, Jaguar amesema “siku hizi naona kama Prezzo ametulia, ameacha yale majigambo yake ya ajabu sasa sijui ni pesa imekwisha, ila namuombea vizuri afanikiwe na siwezi kumuombea aharibikiwe, kama ni muziki anafanya namtakia kila la kheri ila ajue tu always nitakua juu yake kimuziki, simchukii”



B'Hits Studios New Release - March 2012



Hello Friends,

After the big launch ever to be hosted by a Record label in Tanzania, B'Hits Music is throwing its first card this year. Of course the surgeon General Mabeste is leading the postmortem once again. This time Mabeste is dropping some vulnerable lyrics reflecting the endevevours of his personal life. The little success he has attained has changed his way of life and he is promising never to go back. The song is titled "SIRUDI TENA" and it's the first time Mabeste has rhymed fast but with clarity and deep emotion on every word he is pronouncing; one could hear this from his tone. Pancho Latino as usual on his Piano is backing up the "gut spilling" session of Mabeste, and one may prefer to listen to the beat alone; No objection.

Artist: Mabeste
Written By: Mabeste
Created and Composed by: Pancho latino
Produced, Recorded, Engineered By: Pancho Latino
Mixed and Mastered By: Hermy B At B’Hits Studio 4, Dar es Salaam.

All rights Reserved Under Copyright And Neighboring Right Act, only for personal entertainment, not for sale.
Hermy B and Pancho Latino, appears courtesy of B’Hits Music Group Located In Dar es Salaam Tanzania.



Mabeste FT. Jux- SIRUDI TENA (Produced by Pancho Latino, Mixed and Engineered n Mastered By Hermy B)

Hope Ya’ll going to have fun.
Life’s Too Short…Make The most of it.
Hermes B. Joachim Lyimo (Hermy B)
CEO Bhitz Music Group Ltd.

+255 713 513512+255 785 513512

MASHAUZI CLASSIC YATAMBULISHA ALBAMU ZAO MBILI


MSANII wa muziki wa taarabu Tanzania Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, ambaye pia ni mmiliki wa bendi ya ‘Mashauzi Classic’, aliweza kuzitambulisha vyema nyimbo zao zinazopatikana katika albamu zao mbili ya ‘Si Bure Una Mapungufu’ na ‘Sijamuona Kati Yenu’, katika onesho lililofanyika kwenye klabu ya Sun Cirro Sinza.

Albamu hizo zote zina nyimbo nne nne na ambapo ya ‘Si Bure Una Mapungufu’, ina kazi kama ‘Niacheni nimpende’, ‘Mdomo Utakuponza’, ‘Fungu la Kukosa’ na hiyo iliyobeba jina la albamu ambapo hiyo itazinduliwa rasmi Aprili mwaka huu.
Mashauzi classic

Isha Mashauzi stejini 

Mashauzi Classic wakifanya mambo


Pia albamu ya ‘Sijamuona kati yenu’, ina nyimbo kama ‘Sitosahau Kwa Yaliyonikuta’, ‘Anayejishuku Hajiamini’, ‘Hivi Ndivyo Nilivyo’ na hiyo ilibeba jina la albamu.

Msanii huyo alionesha uwezo wake wa kuimba sambamba na wasanii wenzake katika klabu hiyo ambayo ilikuwa imefurika watu wengi hasa wapenzi wa taarabu ambapo walionekana kucheza kwa madaha ka kufuatisha wasanii hao wanavyoimba.

Hata hivyo msanii huyo baada ya kushuka jukwaani alisema kuwa kikubwa anachokiwaza kwa sasa ni kufanya kazi za kimataifa ambapo malengo yake ni kuanza kufanya shoo katika nchi kubwa kama Uingereza, Marekani, Falme za Kiarabu na Ugiriki.

“Malengo yangu ni kuipeleka bendi yangu kimataifa hivyo nahitaji kwenda kufanya matamasha makubwa nje na hii itanisaidia sana kupata mashabiki wengi,” alisema.

source:www.dartalk.com

Linah afanya interview VOA

juzi jumatano mwanadada Linah Sanga alifanya interview na Voice of America....mwanadada huyo yupo nchini Marekani kwa ziara ya miezi minne kupiga show pamoja na kutangaza utamaduni wa Afrika

baadhi ya picha Linah akiwa ndani ya studio VOA

baadhi ya picha Linah akiwa ndani ya studio za VOA

hivi ndivyo status ya mwanadada Linah ilivyokuwa inasomeka jumatano



MKE WA BEBE COOL ZUENA ANYOA NYWELE ILI KUCHANGIA WAGONJWA WA SARATANI


Zuena Kirema, Bebe Cool's wife


mke wa mwimbaji mashuhuri wa Uganda Bebe cool anayejilkana kama Zuena Kirema amenyoa nywele 
“Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa na hamu ya vitu mbalimbali, hamu yangu ilikuwa kunyoa nywele na nimfurahia kuchangia kwa wagonjwa wa saratani wa Boston Children’s Cancer Unit. Sasa najisikia fresh,” alisema Zuena baada ya kunyoa nywele zake.
Bebe Cool & Zuena

Zuena ambaye ana watoto wawili na anatarajia mapacha, yupo Marekani tangu mwezi December mwaka jana na tayari Bebe Cool amemtungia wimbo uitwao ‘Missing You.’ 

wawili hawa January 25 mwaka huu walitimiza miaka kumi ya kuwa kwenye mahusiano ...
blog ya kibabra inamtakia bdada Zuena kujifungua kwema

madaktari Nchini Kenya watunga wimbo kuhamasisha wagonjwa kutokwenda Hospital


moja ya mabango yanavyosomeka katika mgomo unaondelea nchini Kenya


mgomo unaoendelea nchini Kenya umechukua hatua nyingine kiasi kwamba madaktari nchini humo wamepuuza onyo lililotolewa na waziri wa huduma za matibabu Profesa Anyang la kuwafukuza kazi madaktari wote ambao hawatarejea kazini mpaka leo mchana.
Madaktari wameweka ngumu kurudi kazini japo wahudumu wachache wameonekana wakirudi kazini na pia kukitokea mgawanyiko kati yao, wengine wakirudi wengine wakiendelea na mgomo.
Madaktari hao wamebuni wimbo wao wa kuhamasisha wagonjwa kutokwenda hospitali, na baadhi ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huo ni  “wagonjwa msikujeeeee bado tunagoma, tunagoma, tunagomaaaa”

''kweli duniani kuna lugha mbili ambazo zinawezwa zungumzwa sehemu yoyote duniani na mswahili na mchina wakaelewana nazo ni MUZIKI NA MPIRA''

LILIAN INTERNET ATAJA MKWANJA ULIOMSHAWISHI AHAMIE MASHUJAA BAND!

Lilian Internet kwenye moja ya show alipokuwa na twanga pepeta


Stori iliyoshika nafasi ya kwanza ijumaa iliyopita kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, ilihusu band ya Mashujaa kuzidi kuchukua wakali wa muziki wa dance kutoka band ya African stars Twanga pepeta, ambapo meneja max wa mashujaa ndio alitangaza hizo habari Exclusive kwamba Wakali wawili waliowachukua walikwenda kuomba kazi wenyewe.

jana millardayo.com ndio ilkuwa ya kwanza kuzungumza na Lilian, hajazungumza na chombo chochote cha habari baada ya kuchukuliwa na Mashujaa.

Internet amesema sio kweli kwamba yeye ndio alikwenda kuomba kazi bali wao wenyewe Mashujaa ndio walimfata mara mbili na baada ya kuridhika na walichoafikiana ndio akaamua kujiunga nao kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo mshahara aliokua analipwa Twanga unatofautiana na wa Mashujaa kwa shilingi laki moja tu.

Lilian ameamplfy “walinipigia simu ila wakawa wanawasiwasi kwa kusema nyinyi bwana hamchukuliki kwenye ile band, mi nikawaambia kama kuna hela nzuri mi nahama wala sina shida, kitu kingine kilichonivutia kujiunga na Mashujaa ni kwamba nilivyokua Twanga pepeta nilikua sifanyi kazi kwa bidii sana, nilikua naona kuna uzembe flani hivi ila kwa Mashujaa mambo yatakua poa”

kwa kumalizia, Lilian amesema mbali na mkataba band hiyo ya Mashujaa imempa shilingi milioni tano kama donge nono la kumshawishi pamoja na kumlipia kodi ya nyumba kwa mwaka ambayo ni shilingi milioni tatu.


habari na millardayo.com