Showing posts with label nikki mbishi. Show all posts
Showing posts with label nikki mbishi. Show all posts

I'm sorry JK by Nikki Mbishi

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(Verse1)
I’m sorry JK nimeona tu niseme/
Mzuka huu niliupata nikiwa Juu Kijenge/
Mikopo hakuna tena huendi chuo kikuu kizembe/
Bungeni wanalewa wanabonga tu king’eng’e/
Wakitwanga wanatamba wakisanda wanatubu/
Simuoni tena Jay tangu akutane Sugu/
Scorpion amegeuka ghostface mwema/
Aliyeota Rais atakufa anaitwa Godbless Lema/
RC na Wasafi uswazi madefender/
Hapa Kazi tu mtaani njaa kali sio sinema/
Kama kuisoma tushaisoma namba/Ungegombea awamu ya tatu ingekuwa bora labda/

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(verse2)
Enzi za bibi cheka wengi walikuita babu cheka/
Hawakujua kuwa nyakati zinakuja nakusepa/
Ulivunga wakibeza kuwa unapenda sana bata/
Na kiki ka” Makonda za Wasafi kuwafuata/
Wabongo watakumbuka kwenye sekta ya michezo/
Mpaka Taifa Stars nayo ikaonesha mauwezo/
Ukaongeza vigezo nyenzo matengenezo/
Leo Samatta ndo kinara na hachezi soka la dezo/
Tuzungumze magazeti Bunge wanaedit/
Hakuna mikakati bwana kumbe wanaekti/
Demokrasia demoghasia za Field Force/
Wengi wanafear ukweli kuwaambia Unju siogopi/
Mabenki yanafilisika madeni yanamimika/
Hali imekuwa ngumu hadi wageni wanasikitika/
Hatusheshi na shisha yaani sio fresh inatisha/
Bar mwisho saa sita siku hizi hatukeshi kabisa/

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(Verse3)
Kila taarifa ya habari leo JPM/
Pesa imepotea kimazingara David Blaine/
Waathirika hawaelewi juu ya mipango ya Bukoba/
Tetemeko wasije kula michango ya Msoga/
Tumekosa usitupe laana tucorrect/
Weka kando chama tuwe wana tuconnect/
Hela imefichwa nyuma ya Pazia la viwanda/
Njoo Sogodo uone Tanzania ya vibanda/
Uone chafu moja na askari mia wakisanda/
Chocho za Panya Road mixer pwiya la miganja/
Kuna nyakati nilikudiss JK/
Now I’m calling for the peace,DAMN! We miss JK/
By Nikki Mbishi 2016

KUPANDA NA KUSHUKA by NIKKI MBISHI FEAT ONE,SONGA&LADY JAYDEE

Tamadunimuzik.....Yeah
Combination sounds....
Combinenga.....

Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2

Verse 1:Nikki Mbishi
Vaa wema vua shari safari hatua,
Round hii mbishi niko gengeni na jua kali,
Siuzi nyanya vitunguu wala pilipili hoho,
Too little too late ushachelewa Jojo,
Wakiniona mi nashine wanachonga,
Ndo maana kila line wanaponda,
Vipi nikisign na Anaconda,
Busy kwenye show mi nashow biz na kwa flow hizi si ndo time ya kusonga,
Hahahahaaa!!! hii ni hit ya kubaki,
Mwenyei kaniumba fit ndo maana lift sitaki,
Nabang kila session mpaka morning groove,
Eti niko chini hunioni juu?,Mi ni leader wa performing crew,
Nizungue ubaki mweupe design ya hair style ya Monikuu,
Haah Nikki Mbishi Songa One The Incredible,
Komando Yosso ni mzozo ngoma ni terrible,
Karibuni..

Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2

Verse 2:One the inredible
Wanasema wanapenda vile mi hubonga kila kitu,
Rap sonara madini huwa nachonga kila siku,
Sina fleva za kibongo naonja kila kitu,
Bila woga wanaloga niwe kioja kila siku,
Kama unaipenda push play ama itose,
Everyday iwe kush nei ama okayyy,
Wazushi msichoke naghushi ninyooshe,
Nipe changamoto sio kila nikigusa tu okayyy
Kuna watu wangependa nigote kwenye misele,
Iwe kwere kote Moko nisote nisiende mbele,
Nichoke niwe kero kokote au niende selo nisitoke,
Ila msiogope nipo milele,
Kwani muumba ndo mpaji kutunga kipaji,
Niko macho wanataka kuniua niwe mtaji,
Niko Anaconda na hii ndo ile siku niko mcaho,
Ila wengi watakesha kila siku..

Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2

Verse 3:Songa
Chungu kichungu natema sumu kisumu,
Hali ni mgumu je utabeba dumu kidumu,
Na kidumu mpaka wasaa utapotambaa,
Na kushangaa kwamba kufika humu ni ngumu,
Ukicheck chance hola,unawaza utaishi vipi endapo majambazi wakipora,
Basi bora,kuwa na wasi kama polisi ni sawa na wazazi wenye bastola,
Heeey.. na bado utakosa njozi,kazi hakuna utanuna utashona gozi,
Niite Songa endapo utakosa pozi,
Au nyong'onyea zaidi ya mgonjwa aliyekosa dozi,
We si kiongozi...ndio,
Mbona maji hakuna wananchi mtaani wanaoga chozi....
(kicheko]

Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2