ielewe mitaa lyrics by Fid Q


uh, yeah
sipo kama nilivyokuwa, haimaanishi niko tofauti
iwe kiroho kimwili kiakili mashairi na hii sauti
mi niacheni emcee shupavu mwenye verse adimu
asiwe hygenic ni ile chick ya life left nim
sistaduu ukiibiwa moyo, usilie mfanye awe official
kidume atulie umuibie jina la mwisho
we skeevy taking this world
kuna friends na foes
kuna snake fake niggaz na ma gigaloo
ukiwa wa ukweli hau'bounce na hautofeli
ubingwa unashika fasta ka mimba na mahausgeli
wananiita mamlaka ya reli kwa hii treni on thoughts
ni kawe rebirth ya makaveli brain drain niondoke
haikiwi fixed bila juhudi nisichokiamini haki happen
naeza lala na bundi na ukaamka mwenye bahati
usilale fofofo, ruzuku itakwisha
utatembea hovyo ka kuku aliyekatwa kichwa
maisha yako fast na yana speed ya light
unaeza freeze kama ice ndani ya fridge ice ice
ukienda mbio, na muda mtapishana
mafanikio, huja kwa kupenda ninachokifanya

ielewe mitaa kisha, ielewe sanaa
napita mmekaa, natisha jamaa
ukibisha ntakushangaa
kukufundisha mi nafaa
nalisha wenye njaa
naweza rudisha masaa

ielewe mitaa (ielewe ikuelewe), ielewe sanaa
napita mmekaa, natisha jamaa
ukibisha ntakushangaa
kukufundisha mi nafaa
nalisha wenye njaa
naweza rudisha masaa
ielewe mitaa

usiache ulichotaka maishani, ghafla tu na kufuata kile ulichotamani
ielewe ikuelewe, kama oxygen na carbon
hauwezi game bila pain muulize saigon
naishi kiboss na usanii haupotei
natumia noti, tangu ina sahihi ya mtei
niletee mabumunda, mjeshi nikiwa vitani
nikikuta mnaabudu punda, ntawapelekea majani
wangapi huji'stress, hujitia mapozi na hawajielewi
msiache nutcase, inaeza ka divorce ya hail mary
funny huh?, sijui serious yuko wapi
i make cred gos in the front row forward left
ni ngumu kuitafuna? usiimeze haraka
sumu ushakunywa, jiandae tu kucheza salsa
urembo na uzuri upo ndani kwa nje mnajiongopea
muuza sura usikose amani makunyanzi yakikutokea
badili mwendo mkwepe skendo, mwache aende zake
au muonyeshe upendo, tembo hachoshwi na pembe zake
ujinga ni mjukuu wa uoga yule aliyemzaa chuki
vina vinanipa nyota unaonifaa kama mkuki
simmwagii chumvi konokono asiye na gamba
na simkumbatii nyuki kwa maono ya asali kuilamba
ilewe ili usionewe usinyonywe usipuuzwe tena
unyonge uondolewe, usonge mbele wewe uishi vyema


ielewe mitaa kisha, ielewe sanaa
napita mmekaa, natisha jamaa
ukibisha ntakushangaa
kukufundisha mi nafaa
nalisha wenye njaa
naweza rudisha masaa

ielewe mitaa (ielewe ikuelewe), ielewe sanaa
napita mmekaa, natisha jamaa
ukibisha ntakushangaa
kukufundisha mi nafaa
nalisha wenye njaa
naweza rudisha masaa
ielewe mitaa

ielewe ikuelewe!

12 comments:

  1. Fid! is the swag don! i aint get tired of him.... damn! Much respect brother!

    ReplyDelete
  2. This shit z dope a aint gettin tierd of listening it

    ReplyDelete
  3. anakipaji chs mashairi, i luv u my bro

    ReplyDelete
  4. Bila Fid hamna sanaa

    ReplyDelete
  5. The artist of next generations,watch and learn

    ReplyDelete
  6. Poa Sana..Yaani Hatarieh

    ReplyDelete
  7. Hiphop talented Noma mzee Mbuzii

    ReplyDelete
  8. Enter your comment...fantastic verses

    ReplyDelete
  9. Icon ya tz hip-hop fid
    Q

    ReplyDelete