(Verse1)
Mawazo kichwani sawa
na tamthilia ya kusadikika
kuwa na magari
majumba yasiohesabika
Niweze ishi maisha ya iringa kama nipo amerika
sababu na mkwanja nngemuoa mtoto malaika
nngekuwa mrefu kwenye mkapu ni patashika
nngewapa madunk yale yakukata na shoka
nngechora tattoo kichwani nywele nngesuka
kuonyesha msisitizo Kiswahili kisingesikika
nngependa kuongea lugha ya asili nilikotokea
gangi njombe ugonile si unainyaka
mistari yangu verse kinyakyusa nngeandika
na kufanya lugha yangu kisanii kutambulika
maisha yangu yangekuwa hadithi kihesa mpaka isoka
mpenzi wangu angepata kile anachokitaka
fedha ingeongea sauti yangu ingesikika
shikamoo mzee nngepata kwa kila rika
wapambe nngekuwa nao wasiohesabika
hata niongee upumbavu makofi yangesikika
nngefanya uhalifu polisi nao wasingenishika
kunako mahakama mshiko wangu ungetumika
vyombo vya dola sheria za nchi nngeshika
nembo ya taifa bongo recods ingetumika
watoto wadogo mic lazima wajue kushika
lakini yote hii ni kama
(Chorus)
kama mike tee nngekuwa star
kama ningekuwa na mkwanja kachaa
kama ningekuwa ni mrefu na mkwanja kachaa
iringa town ningekuwa balaa
*2
(verse2)
Kama ninge kama ningekuwa mimi star
Hakika jina langu kila mtaa lingezagaa
Anzia ngazi ya shina ,tawi mpaka mkoa
Vibanda vya mc katuni vyote nngebomoa
Na watu wangenipa sifa nyingi za marehemu
Na kuonekana kama nusu mtu nusu mazimu
Mademu wangesema ‘’mike tee we handsome’’
Hata kama uso wangu una makovu kila sehemu
Nngenunua benzi sita zote za rangi ya blue
Mkata majani wangu asingetembea kwa mguu
Msela akitaka jiti me namkatia blue
Nakuonyesha mambo yangu ni safi usawa huu
Kwakuwa na mkwanja hata mungu angesaulika
Huku kuingia peponi
nngekuwa na uhakika
Kwa kujipa moyo mbona natoa nyingi sadaka
Jina langu siku ya
mwisho halitasaulika
Kwa mbumba kachaa aah ntakuwa nasifika
Kinyalu mdomoni
hakika hakitanitoka
Kama kutosa me ntasema kudaga
Na ntajenga kilabu kikubwa cha pombe dabaga
Na ntapeleka muswada bungeni ulanzi uitwe lager
Uuzwe supermarket za bongo na hata za Canada
Watu wapate mshiko wanyalu waache kudaga
Music awards za mtoni zifanyike dabaga
Ntajenga trade center za nguvu tanangozi
Mabinti wote wa kinyalu wasome waende kozi
Hili wapate ujuzi waache ubabaishaji
Ila yote ni kama
(Chorus)
kama mike tee nngekuwa star
kama nngekuwa na mkwanja kachaa
kama nngekuwa ni mrefu na mkwanja kachaa
iringa town nngekuwa balaa
*2
(Chorus)
kama mike tee nngekuwa star
kama nngekuwa na mkwanja kachaa
kama nngekuwa ni mrefu na mkwanja kachaa
iringa town nngekuwa balaa
*2
No comments:
Post a Comment