(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukuaMbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda
(verse)
anapenda ku'bang anakazi huyu jamaa, na ma'star kadhaa wenye jina ndani ya Dar
si nikajaa mi mzawa wa Dar na nikaachwa kwenye mataa
Nashangaa namba zake nimezidiwa mang'aa mashaka alikuwa kando
Nilihisi mchizi Bonge la mwana, ah Kumbe mgambo
Vitani hawezi kushika zana, ah kweli kufa kufaana\
Nimeamini ya leo sio ya Jana {kweli ya leo sio ya jana}
Vizuri kufa na Ujana, ila Life ya dunia ni tamu sana
hizo sekunde na dakika bora zingerudi nyuma
niwe bonge la bitozi hata salamu ningeuchuna
Mbio zimegonga ukuta, kusanuka kishanuka na matuta nimeruka nimeanguka siwezi tena nyanyuka
hata, hata shabaa alinitonya wewe ni rafiki bar
nikapuuza kwakujua na mzawa wa kitaa
ghetto la darstamina pia nikalitaa nilihisi kama nabanwa
si ni wewe nilikulea ukiumia na'feel pain
utetezi juu yako kama jeshi la UN
Ulidaiwa sikusita kukulipia madeni
leo iweje uniingize mkengeni
(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda
(verse)
Nilikuwa ndani ya ghetto na'settle mipango ya kesho mara ring ring
kucheki alikuwa mwana, story ilikuwa hivi nanukuu Michapo
"mwanangu sio siri una zali la mentali
kuna binti mtaa wa pili anadai anakukubali
anasema nyimbo zako unajua panga mistari
Tajiri, hatari wekaa tuchume mali
isitoshe ana figure matata hana dosari
hata leo tukienda atakuhonga hata gari
kifupi sijajivunga na pozi zilikimbia
ghorofa nilionao mnyamwezi nikajitupia
pe..pendo ulikuwa faster kama goli la feste
tuliishi kwenye bungalow sio nyumba za gesti
shida nilizishinda hata kwa manji navimba
kumbe nimepewa goma limepiku si..
yule dada mwathirika nimetumika bila kinga
na mchizi alishajua nnapotimba nachinjwa
(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda
ichek video hapa
No comments:
Post a Comment