Quick Racka ku''hit the floor'' hivi karibuni



MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Quick Racka, amesema kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘On the floor’, ambayo itakuwa maalumu kwa kwa ajili ya mashabiki wake wa klabu.


Msanii huyo alisema kuwa wimbo huo utaenda sambamba na video ambapo baada ya kukamalisha video ya ngoma yake ya ‘Fire Atherm’ kazi ndiyo itakuwa inafuata.


Alisema ameamua kutoa ngoma hiyo kwa ajili ya mashabiki wake kwani ni wimbo ambao utakuwa unachezeka hata sehemu zote hasa kwenye kumbi za starehe kama vile klabu.


Hata hivyo aliongeza kuwa kikubwa anachotaka kufanya ni kutoa ngoma mbili ambazo ni hizo ‘On the Floor’ na ‘Fire Atherm’, ikiwa sambamba na video zake.


“Maandalizi yapo na ngoma hiyo mpya tayari inakamilika lakini kikubwa nachotaka kufanya ni kutoa zote kwa mpingo pamoja na video ili tu mashabiki wangu waweze kuona nini kinachoendelea katika muziki wangu,’ alisema.

Na Laurent Samatta wa Dartalk.com

chek na lyrics ya wimbo wake wa

No comments:

Post a Comment