Suma Lee afiwa na mama yake



Msanii wa kibao kilichoshinda wimbo bora wa Afro Pop na Wimbo wa Mwaka kwenye Kili Tanzania Music Awards 2012, Suma Lee, amefiwa na mama yake mzazi Muhimbili jana.
Mama yake Suma, ambaye alifikwa na mauti katika hospitali ya Muhimbili, alikua akiugua maradhi ya kiharusi.
Tunaiombea familia ya Suma, Faraja katika kipindi hiki kigumu,na kuiombea roho ya marehemu ilale mahali pema peponi, Amin.

No comments:

Post a Comment