uliponitosa mie, nilibembeleza ukataa tena..
sikuwa na kosa mie, mie nahisi sina chapaa
sasa sijapata, hata kama nikipata
nitazidi kutafuta, naomba ondoka
mwenye mapenzi ya kweli, asije akakuta
ningekusamehe ila, ila wewe huna ila
ningekuwa na we, ila, ila unapenda sana hela
eeh
nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
mimi, ya kale achana nayo, niko chini ya miguu yako
kwani nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
mimi, ya kale achana nayo, niko chini ya miguu yako
mmh
mhhh
basi sikia mpenzi, mbona wanipa kazi
bila wewe siwezi, nitajawa na simanzi
mwenyewe wajua, jinsi gani nimekufia
basi nakuimbia, usiweze kunikimbia
unajua sina ujanja wa kuachana nawe
kuniacha njia panda, nitapata kiwewe
huyo mtimue, mi unirudie eh
usiniache nilie, wewe ni wangu mie
mhhh, eeeh
ningekusamehe ila tayari mi nishampata mwingine
ulitaka uniuwe nitaichwa chizi mi nikikupa nafasi nyingine
nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
mimi, ya kale achana nayo, niko chini ya miguu yako
kwani nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
mimi, ya kale achana nayo, niko chini ya miguu yako
ni machungu kiasi gani, uliponiacha gizani mi
ulitaka nifanye nini, kama si kusaka kampani
nilidata, nikasaka, na hatimaye nikapata
nashangaa, wanifuata, eti tusahau yalopita
ningekusamehe ila ila, ila sio kimapenzi
ningekuwa na wewe ila ila ila nimeshapata mupenzi
sina habari, sitaki kuwa nawe tena
huna nafasi ndo hivyo nishakutema
nakupa fact unielewe kiundani
sina mapenzi kwako yalikuwepo tu zamani
nenda tu uniache wala usijali
nimempata mwingine ananipa mapenzi ya kweli
ulivyonitenda mi nasema iliniuma
we nenda tu mi sikutaki tena
sina habari mami sikuhitaji tena
mtoto mzuri nipo naye mwenye heshima
na shida zote atavumilia na
atanipa mapenzi ndivyo alivyoniambia
andika story ya kwamba ulikuwa nami
andika story ya kwamba ulikuwa nami
kifo cha panzi ni furaha kwa kunguru
sikutaki tena mami we niache huru
nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
kwani nani? alotaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho
No comments:
Post a Comment