tushukuru kwa yote lyrics by Lameck Ditto

Verse 1
Kwa pamoja Tutazame Hapa Tulipo
Panatuonyesha Picha Ya Mbali Uko Tuendako Mpenzi
Mengi Utasikia Yakisemwa Usiweke Moyoni
Kuteleza Inatokea Mambo Ya Ndani Usiyaweke Hadharani
kama ndege njoo turuke angani wote
unishike nikushike ili tuwe wote
mvua ikinyesha iwe baraka ya penzi letu
lolote likitokea basi tuanguke na tufe wote

Chorus
wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana
tena pengine pesa siyo tatizo vipigo kati yao upendo hakuna

Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heeeeee Tushukuru kwa yotee

Verse 2
Asiye nipenda hakupendi hata siku moja
Siku tunaachana ndiyo wanachongoja mpenzi
Juzi nilikosea nikakukuta unalia machozi
Nilipo kuomba radhi ukaelewa samahani ikaokoa penzi

Chorus
wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana
tena pengine pesa siyo tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
tena pengine pesa siyo tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heeeeee Tushukuru kwa yotee
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heeeeee Tushukuru kwa yotee

Bridge
Ni siku nyingi tumejenga mapenzi imara
Wapo hwapendi wameamua kujenga na hila
Wasilete maneno na vikao wakatukalia
Ikawa sababu yakutufanya na sisi kuyumbaaaa

Chorus
wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana
tena pengine pesa siyo tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
tena pengine pesa siyo tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heeeeee Tushukuru kwa yotee
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heeeeee Tushukuru kwa yotee

source:http://www.lameckditto.com/

No comments:

Post a Comment