verse1 in 2030 by R.O.M.A


Huwezi kuijenga ROMA haikujengwa kwa siku moja
Iwe kwa raha leo au simba mtoto Tanga utakuja
Hata pancho pia ni mwamba ila bado ana kitaka kiuno
Kaskazini bila Tanga ni msondo bila gurumo
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa na halitatikisika
Waumini tuianze misa
Wenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padri au Allah
Adhana ikilia amka ukamuombe Allah
... We shehe mrudie mungu masanja kawa mchungaji
Sujudu maka na dina tajiri hataki kuhiji
Maulidi ubungo kibangu
Ndio mishahara ya madrasa
Ona rafiki wa padri kawa mhasibu wa kanisa
Wengi wanapeana kindugu mwanangu kuwa uyaone
Familia ilikata ringi na mama akabaki mjane
Sikuwa na damu ya kiarabu
Kwamba nitarithi mabasi
Dingi akutupa msingi ona gari tunaifanya tax
Tazama gongo la mboto mtoto
Kazaa mtoto na atalelewa na nani baba yake mmefunga keko
Wape buku waue winga wale watoto wa moroco
Mungu atazidi kulinda kesho utaiona sabato
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
Ana wake watatu je watoto watarithi nini
Ndio chanzo cha kurogana na kutupiana majini
Huyu akipandisha makata huyu maimuna subiyana
Maana pesa ndio ilifanya tusiwe na tanga ndugu
Pesa ilileta ubaguzi kati ya loyola na pugu
Pesa ndio ilichochea beef ya nice na dudu
Na pesa ndio ilimaliza beef ya ruge Na sugu


....TO BE CONTINUED

No comments:

Post a Comment