Mwambie Mwenzio by Stamina ft Darasa and Warda

[Intro - Stamina]
You know what Tidi..
This is One Love Effects man
Shodobwenzo on this one
Its Moro Town baby!!

[Verse 1 - Stamina]
Uh!
Wakuja rudi bush, mji unahitaji waliosoma
Kicheche usikae uchi huku umevaa sketi ya ngoma
Safisha kope braza Mungu sio Deus
We ushangai mzungu mweupe ila anakivuli cheusi..uhh!
Kuitwa lijali anamaana nyumbani tule
Ukimwi kuutibu aghali sa iweje upate kwa bure!?
Binti usitoe mimba ukihisi utakosa soko
Zaa umtunze kinda mbinguni usichomwe moto...what!
Acha kuiba we fisadi uliyetukuka
Mshtue na Ngaliba nae aache watu wanakufa
Dogo unaekunywa gongo ukifa utazikwa la mboto
Na denti skuli ndo mchongo ya mjomba mwachie Mpoto
Teja pandisha mlege rudisha kete kwa pusha
Mwambie atanyea debe akikamatwa na vya Arusha
Acha makuzi mpendaji ili ufike mbali
Mapenzi king'amuzi na pesa ndo dijitali

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Verse 2 - Stamina]
Ewe mtegemea ndugu mwenye mikono na miguu
Maskini tatizo sugu kuliko hata Mr. II...eeh!
Baba la baba weka ubaba kila levo
Kitaani usawa unakaba hadi padri anaishi devo
Mabadiliko daima huanza na wewe
Kama unakokwenda siko uliza ili usichelewe
Mche Mungu kama hajapanga hajapanga
Kama riziki mafungu kwanini ushinde kwa mganga!?
Kusoma mpaka uchizi ni kukosa kujiamini
Mvivu unaependa usingizi utakufa ukiwa maskini
Endapo utailaza akili usitegemee shida kukuamsha
Hakuna mpenzi kama dili funga nae pingu za maisha
Hakuna tofauti kati ya tajiri na maskini
Uvae bukta uvae suti ila wote tutazikwa chini
Usimtenge mkiwa kisa wazazi wake walimtupa
Hata ng'ombe ana mziwa ila akila sumu anakufa

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Verse 3 - Stamina]
Uuh!
Huna hata cheti cha form 4, na una ndoto za kuwa raisi
Nyumbani unajaza choo, hupaswi kungoja na urithi
Kufeli hasara akili hailetwi na milo
Sio kisa dunia duara ndo denti upate ziro
Kila kitu kizuri duniani huletwa na pesa
Braza elimu haina umri usiogope kusoma memkwa
Ujanja hauna miaka kiujinga we baki mdogo
Acha uchu wa madaraka kwa kuongoza hadi vigogo
Hivi vifo vya wasanii vinatokea ka ajali
Ehh Mungu mshushe Nabii atukumbushe kusali
Tumia akili maishani uongoze jahazi
Na usitafute utajiri kwa kumtoa kafara mzazi
Hujachelewa bado cha msingi we piga kago
Shukuru bado unahema wala usishe vilago
Kijana taifa la leo usilale we ijenge kesho
Ukoloni mambo leo usikufanye ujione special...What!!

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Outro - Warda & Darasa]
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!

Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!

No comments:

Post a Comment