drive slow by JCB ft Prof J

Kwenye corner homie x4

(chorus)
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye corner homie
Drive slow homie
you never know homie...
Mambo mengi yanatokea kwenye lami homie x2

(Verse1-JCB)
Punguza kasi kuna upepo mkali
120 haifai 80 afadhali
Ila tazama kuna kona kali
Toka kwa mbali
Trafiki wanajari ili kuepuka ajali za barabarani
Nazilaani kwenye lami napenda niione wami kama road za kilani
Me ni msomi kama sami ndio maana sipishani kwenye road
Kama madereva wa bedfod au pikipiki za toyo
Naogopa kuwa bodi na sipend offer au gar ya kukodi
Napenda kurekodi kama snoop dog
Hulali kama nyange na manongi
sema speed kali kwangu hainogi
Mfano mpo nyomi kwenye lami mnatoka manyoni
Dereva yuko kasi kwenye kona hona haioni
Jesus Christ bus ikaclimb

(chorus)
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye corner homie
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye lami homie x2

(Verse2.prof J)
Ajali wewe ndio umemchukua mama yetu mpenzi
alipokua akivuka barabara maeneo ya mbezi
Tunamiss upendo wako na tunakuombea kwa mwenyezi
Na mama pumzika pema daima tutakuenz
Dereva ebu simama pale unapoona zebra
Ona umemgonga mama na maisha ameyapoteza
Kinachotuuma zaidi eti sheria imemuachia
Daima tutakulilia muuaji hana hatia
Binadamu roho mbaya sasa imegeuka mtaji
Unampiga tofali wakati anakuomba maji
Drive slow drive slow uwe na lori au bajaj
Wanamuua majeruhi hili wagawane ulaji
Na nyie kwenye bodaboda mbona hamjavaa helmet
Mmepanda mishikaki na hii tunaiita hell on earth
Drive slow mbona mnachezea maisha
Trafiki wakamate au rushwa imehararshwa
Dereva anaongea na simu mwendo kasi kwenye kona
Anaovertake blindly bila mbele kuona
Kwel safari zetu sasa ni kufa na kupona
Na tiktak boom ndio kitu nachokiona

(chorus)
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye corner homie
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye lami homie x2

(Verse3-JCB)
Nimeshamkosa shangazi
Wengine wajomba ndugu na wazaziSio kwa maradhi kwa ajali
wengine vilema kwa bajaj
Kwa speed kali au kilaji
Pombe mbaya sana inachangia uone kona mchala
Dereva unageuka vipi nyuma kisa umeona msichana
Umepakiza beer vipi unaagiza beer
Msambiat ukikarbia utakumbuka gear
Ulevi unachangia ajali asilimia mia
Kila mahali Hata ulaya pia
Tungekuwa na mabawa tungetumia
Tumechoka kuona ndugu zetu wanavyoumia
Bila kutumia akili
Askari unampa leseni learner tena class C
Kwa kilo mbili
Tutaepuka vipi ajali
Kama tunauza utu na roho kwa hali na mali

(chorus)
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye corner homie
Drive slow homie
you never know homie
Mambo mengi yanatokea kwenye lami homie x2

(outro:Prof J
Majeruhi wengi sana wanafariki dunia
Wakisubiri pf3 wakatibiwe
Serikali ingeweka vitengo hivi muhimu
Karibu na hospital hili majeruhi wasaidiwe
Labda tungeweza kuokoa maisha yao
Mungu ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika amen ..

Jcb and prof J

No comments:

Post a Comment