kemosabe by Fid Q

Niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/
Sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
Kwahivyo nikaenda Dar na treni… of thoughts../
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
Sikutaka kuivaa mikosi..nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport..password.. pin..lakini ni crack codes/
Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/
Je mimi ni kaka mubaya…? kaka aso haya../
KAKA..? huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka.. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/
Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui?
Mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball…. hata kwa mpira wa makaratasi/
Unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
Ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE.. life ni zaidi ya ku-have fun/
Kwani.. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/
Nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/
Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
Ndiyo.. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
Mie ni mbishi.. muulize Nikki – hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba

I'm sorry JK by Nikki Mbishi

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(Verse1)
I’m sorry JK nimeona tu niseme/
Mzuka huu niliupata nikiwa Juu Kijenge/
Mikopo hakuna tena huendi chuo kikuu kizembe/
Bungeni wanalewa wanabonga tu king’eng’e/
Wakitwanga wanatamba wakisanda wanatubu/
Simuoni tena Jay tangu akutane Sugu/
Scorpion amegeuka ghostface mwema/
Aliyeota Rais atakufa anaitwa Godbless Lema/
RC na Wasafi uswazi madefender/
Hapa Kazi tu mtaani njaa kali sio sinema/
Kama kuisoma tushaisoma namba/Ungegombea awamu ya tatu ingekuwa bora labda/

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(verse2)
Enzi za bibi cheka wengi walikuita babu cheka/
Hawakujua kuwa nyakati zinakuja nakusepa/
Ulivunga wakibeza kuwa unapenda sana bata/
Na kiki ka” Makonda za Wasafi kuwafuata/
Wabongo watakumbuka kwenye sekta ya michezo/
Mpaka Taifa Stars nayo ikaonesha mauwezo/
Ukaongeza vigezo nyenzo matengenezo/
Leo Samatta ndo kinara na hachezi soka la dezo/
Tuzungumze magazeti Bunge wanaedit/
Hakuna mikakati bwana kumbe wanaekti/
Demokrasia demoghasia za Field Force/
Wengi wanafear ukweli kuwaambia Unju siogopi/
Mabenki yanafilisika madeni yanamimika/
Hali imekuwa ngumu hadi wageni wanasikitika/
Hatusheshi na shisha yaani sio fresh inatisha/
Bar mwisho saa sita siku hizi hatukeshi kabisa/

(Chorus)
It will one day make sense/
Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I’M SORRY JK/ (x2)

(Verse3)
Kila taarifa ya habari leo JPM/
Pesa imepotea kimazingara David Blaine/
Waathirika hawaelewi juu ya mipango ya Bukoba/
Tetemeko wasije kula michango ya Msoga/
Tumekosa usitupe laana tucorrect/
Weka kando chama tuwe wana tuconnect/
Hela imefichwa nyuma ya Pazia la viwanda/
Njoo Sogodo uone Tanzania ya vibanda/
Uone chafu moja na askari mia wakisanda/
Chocho za Panya Road mixer pwiya la miganja/
Kuna nyakati nilikudiss JK/
Now I’m calling for the peace,DAMN! We miss JK/
By Nikki Mbishi 2016

dume suruali by Mwana Fa

we ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami

(verse1):MwanaFa
who dat who dat hii ni salam na ufahamu
Kama unauza mapenzi sio kwa binam
Hakuna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama askari wa zamu
Dume suruali Dume kaptula
Shauri zako mradi sipati hasara
Usione utani me sihongi hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta mkosi
Sentano yangu hugusi Hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane ujambazi
Hata upige sarakasi Utachonga Viazi

(bahili kama nini!!!!!!)

Ndio mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

(Chorus):Vanessa Mdee
we ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
i want that gucci fendi
spend all on a girl like me
my name is vee money money
spend all on a girl like me

(Verse2):MwanaFa
Nihonge nanunua nini kwanini yani
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani
Usiulize ntakupa nini dada piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi me ni balaa
Unapenda hela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye baby tutaongea

(mwanaume wa hivyo wa nini sasa!!!!!!!!)

Ndio mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

(Chorus):Vanessa Mdee
we ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
i want that gucci fendi
spend all on a girl like me
my name is vee money money
spend all on a girl like me
(Bridge)Vanessa Mdee
Aje aje ajeeee Me mtoto fulani ghali
Nihonge gari Ma swt swt baby
i wanna C u to day unipeleke party
Aje aje ajeee Njoo nikupe TBT

(Verse3):MwanaFA
Sio kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyoyafanya nishayasikia
Ningekuwa mhongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote wangekuwa maadui zangu

(mwanaume ovyo wewe!!!!!)

Ndio mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisifii tena
Kwani unauza nini dada
Hunitakii mema

(Baki na hamu zako

(Chorus):Vanessa Mdee
we ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
i want that gucci fendi
spend all on a girl like me
my name is vee money money
spend all on a girl like me
(baba bure huyu)

Hata pantoni lina staff

unamwambia nani sasa
unamwambia nani sasa

roho by fid q ft christian bella

(VERSE 1:FID Q)
Nilipommiss Hakutokea, ili kunigea kiss au kuni-hug/
Hakuni-care huyu binti, aliendelea kunimwaga/
Sijawahi penda kama hivi lakini mapenzi yakaniditch/
Nilisurvive vipi sikumuita 1st LOVE B@#$?/
Ninahisi.. nilipata vibe ya kuipa truth a facelift/
‘Haupati love bila michuzi hauna cash Fid ‘/
Nikakesha ndani ya booth.. HUYU NA YULE ikawa 1st hit/
Show kila mkoa haikosi groupie kwa guest list/
Life ikawa poa.. lakini u-Playa siuwezi Fid/
Sikufichi inaboa ile mbaya kuvaa jezi nyingi/
plus.. hawara anapasha kitanda moto/
Na haifanyi upweke ukaniacha kiasi cha kumganda huyu mtoto/
Na kuimba mahaba niue.. with a smile on my face/
Haijalishi kama ana uzuri wa kumturn hadi Gay straight/
Mapenzi ni kama ‘ ligi ya mbuzi ‘ Striker anaweza potea/
Wengi wanawa-cheat na kuwaudhi wachache wanao-Play fair/


CHORUS ( CHRISTIAN BELLA )
Mapenzi ni matamu lakini ninahofia kuumizwa moyo/
Nashindwa kujaribu.. roho inaniuma/
roho inaniuma x 5

BRIDGE ( CHRISTIAN BELLA )
Ninahofia.. kuumizwa moyo, bila hata kupewa pole/
dudu liumalo, kwanini nilipe kidole?/
ooh moyo.. roho inaniuma mie/

VERSE2 ( FID Q)
Dear hustle.. ni wazi penzi lako ni safi na huniacha happy kila wakati kubaki nawe ni kisamati baby/
Kipi sipati? ninahiti kwa chati.. waliotashtiti mziki haunilipi.. wako wapi? waniache.. mkate nipate baby/
Money makes a man.. lakini love ni hustle/
You know who you love but you dont know who love’s you/
Wakuniletea Baraka kama Michelle/
Na Tabasamu zaidi ya wafungua mlango wa 5 star hotel/
Dawa sio chungu ndugu.. chungu maradhi/
Hakyamungu tena.. chuki humchoma anayeihifadhi/
Kumsahau siwezi.. ni sawa na kumkumbuka nisiyemjua/
Mapenzi yalifanya nikaumbuka.. ninachoshukuru hayakuniua


CHORUS ( CHRISTIAN BELLA )
Mapenzi ni matamu lakini ninahofia kuumizwa moyo/
Nashindwa kujaribu.. roho inaniuma/
roho inaniuma x 5

salome by Diamond Platinumz ft Ray Vanny

[Verse 1: RayVanny]
Kioo hakidanganyi mama
Umejipodoa umepodoka
Mwendo na shape vyote mwanana
Mi suruali yanidondoka
Tukimbizane nini Salome wangu?
Hiyo michezo ya jogoo
Mbona watizama chini Salome wangu?
Ukimuona jongoo
Inama kidogo
Shika magoti
Mi nimesimama kama ngongoti
Mtoto jojo sio roboti
Chumbani bingiribingiri ‘samasoti’

[Chorus: Diamond Platnumz]
Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aaah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Verse 2: Diamond Platnumz]
Utamu kolea a porokoto
Ting’ali ting’ali ndani kwa moto
Ntamnyongea msokoto
Nteme sumu kali kama koboko
Eeh mapenzi yananipa shida
(Shida mama)
Ni donda lisilokuwa na tiba
(Tiba bwana)
Usije baby ukanicharanga
Ukanichambua moyo kama karanga
Mie baby kwenye msambwanda
Huwa siendagi nge nge ni nga nga nga

[Chorus: Diamond Platnumz]
Unantenkenyaga ukinyonga Salome
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Unantenkenyaga ukinyonga kweli
(Unantekenyaga ukinyongaa)
Aah orera bakuru vani
Orera ngambee
Orera na Zari ma
Orera ngambe

[Verse 3: RayVanny]
Miee mwenzako nyang’anyang’a
Miee binzari we ndio nyanya
Baby kwang’waru
Nisimamie kama kangaroo
Ibane kangwaru
Babu Juma mpige kwakwaru
(Kwakwarukwa)

[Bridge]
Asa chambua kama karanga sasa
(Chambua kama karanga)
Ichambue kama karanga Salome
(Chambua kama karanga)
Asa washa, washa, moto washa, washa
Songa, songa, ugali songa, songa
Mpaka chini ka chi
Mpaka chini ka chi
Wenye wivu wajinyonge leo
(Wenye wivu wajinyonge)
Aaah wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)
Wenye wivu wajinyonge kweli
(Wenye wivu wajinyonge)
Oooh wenye wivu wajinyonge sana
(Wenye wivu wajinyonge)

[Outro]
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Macho kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Wale kodo!)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(Ukinyonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa
(We ukisonga)
Wanakodoa kodo!
Wanakodoa