Baada ya kuukubali mwaliko wa
kwenda kuimba kwenye stage moja na Usher Raymond Marekani, alafu
akaukubali tena mwaliko wa mama Laura bush kwenda na kurudi marekani kwa
mara ya pili, Exclusive leo on millardayo.com mwimbaji Linah Sanga
ameukubali mwaliko wa tatu wa kurudi tena marekani kwa ajili ya showz.
Time hii anapelekwa na mbunge
wa viti maalum (Chadema) Leticia Nyerere ambae anafanya showz kwa ajili
ya kutangaza utamaduni wa Afrika, mavazi yanayovaliwa na wasanii wa
Afrika, jinsi wanavyopafom na mengine.
Akiwa msanii wa kwanza na pekee
kwenye hiyo tour atakayozunguka majimbo karibu 15, Linah ambae atakaa
Marekani kwa miezi minne amesema show zake mbili za kwanza atapiga
Washington DC, ambapo atakua mwenyewe kwenye stage na kuimba kwa kutumia
instrumental tu na atakua anaimba na nyimbo za wasanii wengine pia.
Baadhi ya majimbo atakayotembelea ni pamoja na LoS ANGELES, CARLIFONIA, MIAMI – FLORIDA na TEXAS.
source .millardayo.com
No comments:
Post a Comment