MsaniiI wa muziki wa kizazi
kipya, Amini, amesema kuwa ametimuliwa rasmi Tanzania House of Talents ‘THT’,
lakini anahisi kama ameonewa kutokana na mabavu yaliyotumika. Vyanzo vya habari
vililipoti kuwa msanii huyo anajadiliwa na uongozi, lakini sasa taarifa
iliyopatikana kutoka kwa muhusika zinadai tayari ameshawekwa pembeni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, huku akitokwa na machozi alisema kuwa
uongozi haujatenda haki kwani kosa la kinidhamu alilofanya walipaswa kukaa naye
na kuzungumza lakini wameamua kumfukuza kitu ambacho anahisi ameonewa. “Mimi
sioni kama kuwa wema ndani ya THT, ila nachoweza kusema kwamba naenda kufanya
muziki wangu na mungu atanijalia tu kwa sababu kila kitu ni mipango,” Amini
alipigilia msumali wa mwisho.
Source:
bongoflavortz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment