Tafakari by Suma Mnazaleti ft Mabeste & Ben Pol

[SUMA]
wajana wamebaki jana, leo ujana chanzo cha utozi
uzalendo hawana, viongozi wenye mvi wezi
kubana wanabana, ila suma na'score easy
ujana una maana, ila ukizidi mwisho upuuzi
siasa ya bongo kama soccer, ushabiki bungeni
muuza sura aliyetukuka, mchezo kwako kideoni
ka ufisadi ungekuwa nyimbo, basi chenge kapuni
makopo yanawakosesha shule, watoto mitaani
nyie ndo mlianza kunichukia, mama alifurahi kunizaa
tuna amani bila vita, ila shida inantupia njaa
kauli zao ukiwa na ndoo, tubebe kidumu
ina maana ukienda kazini, mwenzako ana zamu
madada mtaani, washapoteza dira
wanabeba mimba kwa beseni ili walipwe fadhila
wengi wanapenda kuwa mababa wanasahau ada milioni
kiburi chao shule za kata wakati walimu hawaonekani

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[MABESTE]
politics imeshakuwa polifix
rafiki wa jambazi leo kawa polisi
hadithi uongo lazima kisu ni butu
huwezi funga sonko jela tu kama wewe ni kapupu
ngojea tu ni mbichi Haijakamuliwa
na uongo una nguvu sana ukweli unabaguliwa
ndo maana maskini haki anachukuliwa
kwenye fight hivi hivi hawana nguvu wanakamuliwa
ah, watu wa chasey now wind it
ni vile vile sunday ndio kama monday
ndo maana maisha ya sasa imekuwa ngumu
ile kimiminiko si ni afadhali imekuwa sumu
life, better kwa masonko
adui wa haki TZ ni huyu Conc.
yaani corruption umpate kwa game ime go down
si ninapekwa, hii government imekaa pua
cause, msingeanza kisha later
sio gover.. tu ka' mafundi carpenter
na mimi ndio kiburi kipaza ka muhubiri
hakuna ngoja, step lazima tusibaki sifuri

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA]
Mistari yangu inamuamsha aliyelala usingizi wa pono
sauti ya ibada hawezi sikia, aliyelala usingizi wa pono
aliyeona akikuambia tofauti na aliyesikia
aliyesikia akikuambia kuna utamu kashaongezea
aliyefiwa na mzazi mmoja, siku zote hatumuiti mkiwa
wageni wana'make mshiko kwa wenyeji walipozaliwa
wanawake wana mambo mengi mi siweki dhamana
kuna mtu analea mtoto kumbe sio wake mwana
mbea anasema ukweli, ila tatizo hajaruhusiwa
na muongo ndio mzushi wa mtaa, ambaye kesho atakuzushia
maisha yalivyokuwa magumu, vijana wanakuwa mababu
mapenzi yashageuka sumu, hebu kayalambe ufe kwa tabu
miaka hamsini nikimulika, ni uwanja na barabara
town kariakoo na posta mvua ikinyesha bado msala
imani ikizidi utashi basi ukweli unajificha
tasnia imekuwa nyepesi, leo kila mtu anaigiza

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA; Akiongea]
ha, mensen
hii track in high pitch in panic disorder!
flow right beat red nyeusi wataogopa
tyta, lunduno is in the house man
Mnazaleti, again and again yeaah

[BEN; High pitched]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA; Fading...]
...siasa ya bongo kama soccer, ushabiki bungeni
...kuna mtu analea mtoto kumbe sio wake mwana
...ndo maana maisha ya sasa yameshakuwa...

its gonna be alright!

No comments:

Post a Comment