hisia za mtaa by SUMA MNAZALETI FT STEVE RnB

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, yeah, yeah
kando wa visimu mtaani natamathali za semi
namba moja chatini, walionidiss hawahemi
stanza yangu moja, ni staili tatu za stopper
mimi Mtanzania asilia, na nina maneno ya kukopa
ugumu wa maisha so kigezo, cha kunifanya nikabe
au niishe kimitego kama shangarai na mugabe
yatima analia mtaani, nani amfute machozi
nyumba yake inavuja ndani, na mfukoni hana hata cash
mtoto wa mtaaa, mwenye revolution zaidi ya che' guevara
nishakaa midomi, kama mabomu ya mbagala
wanapenda we ufanye kazi, ila usinunue viatu
moyoni washaota kutu, kama pemba na CUF
wanatuchekea kwa tabasamu nzuri lenye mvuto usoni wakati ndani ya moyo nuli
washatutia motoni man, washatutia motoni!
yeah

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, ah
tunatumia miaka sita kuwakamata mafisadi, na uongozi miaka tisa wakumi tunaachia ngazi
siwalipii visasi walionifanyia mabaya, siwasaidii hata kwa cash mwishoni wataona haya
sina ndoto ya utukufu, kwenye ufalme wa Faraoh,
na ntahit bila beef ya kudiss nyimbo zao
chuki zimewajaa moyoni, mpaka wakipumua
wanasababisha global warming kwa kutoboa ozone layer
watu wa mtaaaa!, ziacheni roho za giza
karibisheni za taa, cheki maisha yanaenda kasi
yatawaacha mmezubaa
Mademu wanaamua kuwa feki, kama simu za kichina
daily wanayasaliti mapenzi, sababu ya noti kuziona
mtaani mtu ni mzima, na kila siku anatembea
lakini akienda kupima, malaria imemtembelea
iko vipi, iko vipi man!

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, ah
kimashairi mi ni shule, ili ufaulu uje kusoma
sio midevu imekuchomoka, mtu mzima unaona noma
nishatunga!
uite killer ka shigongo, ukawagawia
mwishoni wamejenga chuki, hawakumbuki walinitumia
unaweza ukadai chako, halafu ukapigwa wewe
na hicho ndicho kilichofanya mababu zetu wasijielewe
(wa mashariki!) wenzetu wanakwenda mbele si mbona tunarudi nyuma
mkataba feki sio real eti wamesaini bila kusoma
usiulize kwetu wapi mabibo ndo nnatokea
I'm the Mafia from the Hood, usinijaribu utapotea
maisha ya leo ni kutafuta, ndo maana yana mfumo
sio lazima utajwe jina, ukinidiss nawe umo
mshapoteza sana muda kuwasha moto mchemshe mawe
rhymes zangu sio za siasa nawaambia ili muelewe man!

haha

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

No comments:

Post a Comment