hakuna matata by Sugu



(chorus)
Nataka swagger za hakuna matata
Kama nataka flows pia matata
Nataka peace hakuna matata
Kama unataka beef pia hakuna matata

(verse1)
Bado nachana kama nina miaka ishirini
Kuna time mpaka mwenyewe siamini
Kwenye hili game tulishakula yamini so kuliacha haiwezekani
Aibu kwao waliosema hatutaweza
maana tumeweza
na tumeweza hadi tumepitiliza
Kwa wana wote sitaacha kusisitiza mambo yanapokuwa magumu
Kinachotakiwa kukaza komaa kaza msuli
Kumbuka daima mungu yu na mwenye kusubiri
Sionekani sana dar
Sababu naishi jimboni kama sipo jimboni labdai nipo mjengoni
Daily barabarani njiani
Ndani ya land cruiser amazoni
Kinachopunguza uchovu ndani nina television

(chorus)
Nataka swagger za hakuna matata
Kama nataka flows pia matata
Nataka peace hakuna matata
Kama unataka beef pia hakuna matata

(verse2)
Hakuna matata lakini ukinigusa tu nakuletea utata
Ndio maana mitaa ya kati wananiita mtata
Kwa wanaonijua wengi wananikubali
Na ndio maana sijali kama we unikubali
kwani wanaonikubali wananitosha
sugu anatisha a.k.a baba sasha
miaka yote maisha yangu ni kubisha
na inshallah ndoto zangu zote nitazikamilisha
mjengo mkali
wife mzuri
na mungu kanijalia nina kabinti kazuri
na ingawa nipo bungeni
bado ni mwanajeshi na general vitani
ukileta namna gani jua nakupa namna gani
na sio sababu natembea gun
 ila sababu wananiita president wa kitaani

(chorus)
Nataka swagger za hakuna matata
Kama nataka flows pia matata
Nataka peace hakuna matata
Kama unataka beef pia hakuna matata

Sugu nah ii kwa mashabiki waliokuwa wanaulizia track one for the road Deiwaka


No comments:

Post a Comment