karibu dar by kala jeremiah ft Ben pol

(Verse1)
picha linaanza ka muvi ya solomoni
ghafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani
hii ndiyo dar, karibu ila usijisikie nyumbani
hapo ubungo usinunue simu utauziwa sabuni
panda daladala tukutane buguruni
kuna watu wanapiga utadhania majini
mtaani usiku utaona rangi zote za bikini
wanauza miili ili wanunue wali maini
usicheke bro kwa sababu mimi si mr. bean
chunga wallet yako hapa kuna wizi wa mfukoni
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi
daladala zina bajaji inakesha macho
ka huamini ngoja usiku ndo uamini we thomaso
wasio na kazi wanashindia stori za freemason
wajanja wamepanga sinza, kino na tabata
mchana anazibua vyoo usiku anakula bata
usikojoe ovyo bro mgambo watakukamata
hii ndo dar, mbona unadata kabla hata hujapata
starter?

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

(Verse2)
karibu sana kwenye hili jiji la joto
uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto
si ulisikiaga mabomu ya gongolamboto
yalifanya rafiki yangu Adamu akafia ghetto
yaliacha kovu kubwa kama la mbagala
dar es salaama watu wengi tu hawanaga pa kulala
kama unataka mirungi twenzetu mitaa ya ilala
magomeni, na ujanja wangu wote niliitwa ----
watu wanaingiza pesa wakiwa ghetto wamelala.....
watu wengi toka waje hawajawahi kurudi kwao
sababu hawana nauli japo wamemiss ndugu zao
kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao
wauza sura wanaishi kwa kuuza madem zao
mama anauza bangi, baba amekata ringi anashinda
anacheza bao
wake zao wanazini kurisha watoto wao
vijana wao wanatembeza karanga, wanatembeza
maji, wanatembeza vocha siyo kwa mitaji yao
jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao
hii ndo dar, ukipenda unaweza kuita bongo
machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo
siri haiwi siri uswahilini ukipata mchongo
wapangaji watakuandama bro mpaka utahama
(bongo)
ni majungu mixer wanga
utaenda tu kwa mganga utakapolala ghetto kwako
halafu ukamwagiwa mchanga

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

(Verse3)
dar es salaam ingekuwa nchi rais angekuwa lowasa
huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa
usione watu wamependeza wengine hawana hata
mia
hapa mboga ni maharage, nyanyachungu na bamia
brazamen anatembea toka keko kwa mguu
anakwenda mlimani city kununua mkate tuu
(are you on facebook?) ndiyo maswali ya maduu
ukitaka demu wa peke yako kata mgomba lala juu
ukimuita dem wako baa, wanakuja 'crew'
utachunwa mpaka raba utabaki miguu juu
hapa bomba halijatoa maji mwezi mzima
hii ni uswahilini tu, wala si kwa jiji zima
twende mbezi au masaki yanatoka mwaka mzima
katiza kwa mtogole uporwe simu mchana
siku hizi mwanaume anavaa suruali ya kubana
siku hizi dada'ako ana kalio za kichina
ukimtafuta humpati ashabadili rangi na jina

CHORUS (ben pol)
bata ni daily (daily)
karibu bushmen kaa chini tukupashe habari
shangaa mataa dar ugongwe na gari
dar es salaam ya sasaX2

joto hasira by Lady Jay dee ft Prof Jay


CHORUS
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba

VERSE1
Kila siku nimenuna kwanini tunagombana
Tena tunakosoana kama tumechanganyikiwa
Na sioni hata maana ya si kuzinguana
Yaani kila mtu anajua sana au yote sababu ya sababu ya

CHORUS
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba

VERSE2
Mazao twalima wote sahani wavuta kwako
Kama  chakula tule wote kwanini  chote kije kwako
Kisu mpini umeshika wewe ni tishio kunikata mimi
Mmmmh Au yote sababu ya sababu ya

CHORUS
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba

VERSE3
(LADY JAY DEE)
Sahau sahau shida ooh kamilisha jana
Say goodbye joto rest in peace shida
Nok nok money
(PROF JAY)
Wenyewe wanasema usawa unakaba na rafiki wa kweli ni mama na baba
Hawa wengine wala usiwaamini binadamu wa sasa wana roho saba
Watakuwa na wewe kwenye raha na hawatakuwa na wewe kwenye njaa
Bora nipige misele yangu peke yangu niruke peke yangu uwoga niliukataa
Nabadilika kama saa na siku hazigandi   na sitakata tama
Wamejaa usaliti na chuki
Watu wa karibu wamenageuka mamluki
booom  General nasonga
Iwe joto au baridi naamini tutashinda
Kama mbwai iwe mbwai barida
We make more money rest in peace shida
Ukinuna unataka tunune wote
Ukilia unataka tulie wote
Vita vyako tunapigana wote
Tukishinda tushinde au bora tufe wote
Kama kulima kote tumelima wote
Hata kupanda kote tumepanda wote
Kupalilia tumepalilia wote
Aah nashangaa sasa mbona hatuvuni wote


CHORUS
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Hili joto hasira amba
Upepo hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba
Foleni mzee mzima  amba
Na pesa hakuna amba
Naruka mwenyewe yerela yerela amba

nje ya box by Nikki wa pili,Joh makini and G.wara wara


House of music A city in tha house
Mpeleke joh makini nikki wa pili wara wara
Mpeleke Nje nje nje ya kumi na nane
Nje ya kumi na nane
Mpeleke Nje nje nje ya kumi na nane

(VERSE1: Niki wa pili)
Mungu nijalie demu mpenda pesa
kila siku nipigane kuwa bakhresa
Asinipende mimi apende verosa
Wana wamegewa wengi  ndio kitu wamekosa
Malighafi ya suruali si boxer
Siri nyingi mahali dingi alikosa
Demu wa  shida na raha na misoto sana
Huyo demu hanifai changamoto hana
Ikiwa demu wako anapenda vidogo
Uwezi kuwa na vingi na kuwa kigogo
Demu amsifie sana bosi wangu
Nikasirike kesho nijenge kiwanda changu
Sitaki demu wa kitanga jioni moja kanga
Tayari amejipanga kwa mabusu  mangapi
Demu nayemtaka manka wa kichaga jioni anaulizaga umeingiza sh ngapi

(CHORUS: G –Nako)
Mpeleke nje nje nje nje ya kumi nane
Nje nje nje nje ya kumi na nane
Mpeleke nje nje nje nje nje nje   ya box  nje ya box
Nje ya kumi na nane

(VERSE2: Joh Makini)
Namtoa nje ya box ndio nampecha ndani ya box
Aulizie ferrari jo ni kitu gani verosa
Demu boda boda kwenye bajaj anasinzia
itaua kipaji na uwezo wa kufikiria
Asinipende kama joh anipende kama stars
Super kabisa  ile gumzo ya kitaa
Hili nikaze asinilemaze nikadumaa
Sio demu anayehitaji kuwa na ndoa
Bali mwanamke anayehitaji mahitaji ya ndoa
Na sheria mikononi simpgi demu
Nachukua sheria kiunoni joh let me kill them
Asiyefanya kazi ndio neno lenye uhai
Asishike neno ashike maneno lenye maslahi
My lips don’t shine when yo hips don’t lie
Sio wa lift vocha  chips mayai
Demu cheap me hanifai
Habari gani afanye niwze milioni
Kumuonga laki mbili tabu nisione
Ukiona mdundo ni mapene ya mweusi
Sio miaka thelethini na tano driving school

(CHORUS: G –Nako)
Mpeleke nje nje nje nje ya kumi nane
Nje nje nje nje ya kumi na nane
Mpeleke nje nje nje nje nje nje   ya box  nje ya box
Nje ya kumi na nane

sorry by Barnaba


This is Barnaba boy classic
Ima the boy classic
And good music classic

(verse1)
Aaah haya eeh aah
nyuma nilitaka kuzungumza na we ila nafasi hiyo kwako nikakosa
sikujuta wala sikulalamika sababu naamini kukupenda wewe sijafanya makosa
japo nilisuffer machozi nikaangusha ila hujawahi nifuta hata kwa kuniongopea
ndio kwanza unacheka huku ukinibeza na mashoga zako vibarazani kuniongelea
mpenzi dunia imebadilika bado naweza nikakupa pesa na bado nikawa nakuongopea
basi vumilia kesho nitapata
nitakupa kila unachotaka sababu wewe ni malkia

(chorus)
baby wangu  am sorry hiii hii
sorry hiii hiii
sorry hii hii hii
sorry hii hii
baby wangu  am sorry hiii hii
sorry hiii hiii
sorry hii hii hii
baby am sorry hii


(verse2)
oneni navyolia kama mtoto
 kwenye sekta ya mapenzi nahisi nimechapwa viboko
na kinachoniumiza ni yangu huruma
maana mama barnaba alisema mwanamke akikuudhi usije kumpiga
oneni ndio nasuffer huruma yangu  inaniponza
kazi yangu kufungua milango usiku wa manane wenzangu wakigonga
nakupenda bado unampenda
namvumilia kila akinitenda
nahisi hiyo ndio nafasi anayoitumia kuniumiza
inshallah navumilia najua yataisha
ipo siku atagundua me ni wake wa maisha
na sitamlipizia nitamvulia na ntambembeleza nitamsahihisha
kila atakapokuwa anakosea

(chorus)
baby wangu  am sorry hiii hii
sorry hiii hiii
sorry hii hii hii
sorry hii hii
baby wangu  am sorry hiii hii
sorry hiii hiii
sorry hii hii hii
baby am sorry hii