Msanii Baby Mahada, amesema kuwa malengo yake aliyojiwekea ni kuja kugombea ubunge
anauwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hivi,
msanii huyo alisema kuwa hashindwi kuwatumikia wananchi hivyo baada ya miaka
kadhaa atakuwa katika mchakato huo. Alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya
kutaka kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na vitendo vya baadhi wanasiasa kutowajali
wananchi ambao ndiyo waliowapa dhamana. “Malengo yangu ni kuja kuwa mbunge na
kikubwa ambacho nataka kukifanya ni kuwatumikia Watanzania, ambao kila siku
wanalia juu ya wasansiasa ambao wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya maisha yao
binafsi,” alisema. Hata hivyo mwandisi alimuuliza swali, msanii huyo kwamba
atatumia chama gani katika mchakato wake huo, ambapo alijibu kuwa hataki kuweka
wazi chama chake lakini muda ukifika kila mtu anaweza kujua.
Source:http://www.pekuatz.com/news/baby-madaha- ataka-kugombea-ubunge%E2%80%A6
No comments:
Post a Comment