Msanii wa
muziki wa kizazi kipya Banana Zorro, amesema kuwa katika suala la mavazi, mara
nyingi huwa ananunua nguo zenye gharama kubwa ambapo suti zote anazomiliki kila
moja amenunua kwa shilingi laki 500 , 000 . Akizungumza na DarTalk, msanii huyo
alisema hana tatizo la fedha hivyo kutoa kiasi hicho cha pesa haoni tatizo
kwani anahitaji kupendeza muda wote. Alisema huwa anafanya manunuzi ya nguo kwa
mwezi mara tatu, na kila anapoenda dukani hutumia shilingi milioni 10, hadi
kumaliza mahitaji yake yote ikiwa pamoja na yale ya familia. “Najipenda sana na
ndiyo maana navaa nguo za bei mbaya, siyo kwamba ninajisifia lakni huo ndo
ukweli uliyopo, unajua maisha haya ukiwa hutumii pesa huwezi kuendelea au
kufanya chochote cha maana,” alisema.
Source:http://www.pekuatz.com/news/navaa-suti-
zenye-thamani-ya-sh-laki-5-kila-moja-%E2%80% 93-banana-zorro%E2%80%A6
No comments:
Post a Comment