Baada ya juzi CHIDI BENZ kukubali kwamba
pamoja na AFANDE SELLE kumdis, yeye bado
yuko tayari kufanya nae kolabo ambayo alipanga
kufanya na Afande wiki moja au mbili kabla hajamdis,
Afande nae ametoa sentensi ya jibu kutokana na alichosema
ChidiBeenz.
Afande amesema “yeah mi niko tayari, niko pamoja nae Chidi
anajua hilo, na hiyo kitu alishaniambia kitambo tukapanga na
mimi bila shaka matatizo yaliyotokea ni mambo ya kupita lakini
mimi wimbo wake hata kesho nasububiri beat niandike tufanye
kitu kilichobora zaidi nafikiri itakua na maana kuliko malumbano
malumbano yanayoendelea haya sio mazuri, sina beef nae”
Chanzo cha beef yao ni baada ya Afande kuhojiwa East Africa
Radio na kufananisha kuondoka kwa Ditto watu pori kwenda
La Familia, sawa na kuondoka Manchester United na kwenda
timu ndogo kama Bolton, maneno ambayo yalimkasirisha sana Chidi Benz.
story na milardayo.com
No comments:
Post a Comment