MASHAUZI CLASSIC YATAMBULISHA ALBAMU ZAO MBILI


MSANII wa muziki wa taarabu Tanzania Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, ambaye pia ni mmiliki wa bendi ya ‘Mashauzi Classic’, aliweza kuzitambulisha vyema nyimbo zao zinazopatikana katika albamu zao mbili ya ‘Si Bure Una Mapungufu’ na ‘Sijamuona Kati Yenu’, katika onesho lililofanyika kwenye klabu ya Sun Cirro Sinza.

Albamu hizo zote zina nyimbo nne nne na ambapo ya ‘Si Bure Una Mapungufu’, ina kazi kama ‘Niacheni nimpende’, ‘Mdomo Utakuponza’, ‘Fungu la Kukosa’ na hiyo iliyobeba jina la albamu ambapo hiyo itazinduliwa rasmi Aprili mwaka huu.
Mashauzi classic

Isha Mashauzi stejini 

Mashauzi Classic wakifanya mambo


Pia albamu ya ‘Sijamuona kati yenu’, ina nyimbo kama ‘Sitosahau Kwa Yaliyonikuta’, ‘Anayejishuku Hajiamini’, ‘Hivi Ndivyo Nilivyo’ na hiyo ilibeba jina la albamu.

Msanii huyo alionesha uwezo wake wa kuimba sambamba na wasanii wenzake katika klabu hiyo ambayo ilikuwa imefurika watu wengi hasa wapenzi wa taarabu ambapo walionekana kucheza kwa madaha ka kufuatisha wasanii hao wanavyoimba.

Hata hivyo msanii huyo baada ya kushuka jukwaani alisema kuwa kikubwa anachokiwaza kwa sasa ni kufanya kazi za kimataifa ambapo malengo yake ni kuanza kufanya shoo katika nchi kubwa kama Uingereza, Marekani, Falme za Kiarabu na Ugiriki.

“Malengo yangu ni kuipeleka bendi yangu kimataifa hivyo nahitaji kwenda kufanya matamasha makubwa nje na hii itanisaidia sana kupata mashabiki wengi,” alisema.

source:www.dartalk.com

No comments:

Post a Comment