mwaka jana lyrics by Izzo business ft shapsin

2011 nakuchukia, ulifanya niporwe demu kisa pesa sikuwanayo
zilizagaa kila sehemu, konde nilipiga moyo
ulimtesa baba yangu kutwa kushinda mahakamani
uliuvuruga ubongo wangu, chuo sikutamani
mwakyembe akawa hoi, na sichoki kumuombea
2011 na hapa nakuchukua, Mr ebo kama ndoto, leo hatupo nae
five star matumbo joto, pengo lao nani akae
bora upite bora uende, tuliobaki tusonge
umetesa wamachinga, japo mbeya nyumbani kwangu
jangwani na mafuriko, labda mipango ya mungu
umeleta marafiki, japo wengi siwaelewi
wanafiki, kuzua hawachelewi
pesa nyingi ulizuia, hata katu sikupata
jina tu lilinisaidia kwenye viwanja vya bata

nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!

wengi wao hawaamini, japo kocha waliletewa
taifa stars wapewe nini ,kwenye challenge wakazomewa
ghadaffi king wa libya, leo hawapo naye
afghanstan nako msiba, Osama hawapo naye
2011, mwaka wa vioja
sio kwako labda kwangu, na haya mawazo yangu
nilipata simu ya vitisho nkatishiwa maisha yangu
ah, usinikoshe naapa kwa jina langu
masoko ya biashara vya vilio vilitawala
kila siku tu moto, masoko yanaungua
wakubwa mpaka watoto mabomu yanawalipua
nazungumzia gongo la mboto, nani asiyejua
marlaw kaweka besta ndani, basi iringa oya oya!
leo niko na manecky, na ngoma iko on fire
diamond mtoto wa tandale sio kwa uchawi wala ndumba
labda yalimcheza machale akatoa pete ya uchumba


nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!


niko hapa swagga zangu ziko full bro
yes business and i run the show
they like what, what more
baada ya keshokutwa, ni mtondogo
niko hapa swagga zangu ziko full bro
 yes business and i run the show
they like what, what more
baada ya keshokutwa, yo mtondogo


nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!

[Shapsin]
wabongo walikosa heshima takwimu zinaonyesha tu
labda kwasasa ndo lazima maana wanawarudisha full ah

hisia za mtaa by SUMA MNAZALETI FT STEVE RnB

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, yeah, yeah
kando wa visimu mtaani natamathali za semi
namba moja chatini, walionidiss hawahemi
stanza yangu moja, ni staili tatu za stopper
mimi Mtanzania asilia, na nina maneno ya kukopa
ugumu wa maisha so kigezo, cha kunifanya nikabe
au niishe kimitego kama shangarai na mugabe
yatima analia mtaani, nani amfute machozi
nyumba yake inavuja ndani, na mfukoni hana hata cash
mtoto wa mtaaa, mwenye revolution zaidi ya che' guevara
nishakaa midomi, kama mabomu ya mbagala
wanapenda we ufanye kazi, ila usinunue viatu
moyoni washaota kutu, kama pemba na CUF
wanatuchekea kwa tabasamu nzuri lenye mvuto usoni wakati ndani ya moyo nuli
washatutia motoni man, washatutia motoni!
yeah

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, ah
tunatumia miaka sita kuwakamata mafisadi, na uongozi miaka tisa wakumi tunaachia ngazi
siwalipii visasi walionifanyia mabaya, siwasaidii hata kwa cash mwishoni wataona haya
sina ndoto ya utukufu, kwenye ufalme wa Faraoh,
na ntahit bila beef ya kudiss nyimbo zao
chuki zimewajaa moyoni, mpaka wakipumua
wanasababisha global warming kwa kutoboa ozone layer
watu wa mtaaaa!, ziacheni roho za giza
karibisheni za taa, cheki maisha yanaenda kasi
yatawaacha mmezubaa
Mademu wanaamua kuwa feki, kama simu za kichina
daily wanayasaliti mapenzi, sababu ya noti kuziona
mtaani mtu ni mzima, na kila siku anatembea
lakini akienda kupima, malaria imemtembelea
iko vipi, iko vipi man!

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

yeah, ah
kimashairi mi ni shule, ili ufaulu uje kusoma
sio midevu imekuchomoka, mtu mzima unaona noma
nishatunga!
uite killer ka shigongo, ukawagawia
mwishoni wamejenga chuki, hawakumbuki walinitumia
unaweza ukadai chako, halafu ukapigwa wewe
na hicho ndicho kilichofanya mababu zetu wasijielewe
(wa mashariki!) wenzetu wanakwenda mbele si mbona tunarudi nyuma
mkataba feki sio real eti wamesaini bila kusoma
usiulize kwetu wapi mabibo ndo nnatokea
I'm the Mafia from the Hood, usinijaribu utapotea
maisha ya leo ni kutafuta, ndo maana yana mfumo
sio lazima utajwe jina, ukinidiss nawe umo
mshapoteza sana muda kuwasha moto mchemshe mawe
rhymes zangu sio za siasa nawaambia ili muelewe man!

haha

Hizi ni hisia za mtaa zinachoma mpaka kwenye moyo
sisi tulio kitaa tuna hustle mpaka tuone mwisho
Usione tuna raha, toka mwanzo sisi tunakomaa, daily
kila siku ni karaha, ila juhudi inatupa faraja tuende mbele

Tafakari by Suma Mnazaleti ft Mabeste & Ben Pol

[SUMA]
wajana wamebaki jana, leo ujana chanzo cha utozi
uzalendo hawana, viongozi wenye mvi wezi
kubana wanabana, ila suma na'score easy
ujana una maana, ila ukizidi mwisho upuuzi
siasa ya bongo kama soccer, ushabiki bungeni
muuza sura aliyetukuka, mchezo kwako kideoni
ka ufisadi ungekuwa nyimbo, basi chenge kapuni
makopo yanawakosesha shule, watoto mitaani
nyie ndo mlianza kunichukia, mama alifurahi kunizaa
tuna amani bila vita, ila shida inantupia njaa
kauli zao ukiwa na ndoo, tubebe kidumu
ina maana ukienda kazini, mwenzako ana zamu
madada mtaani, washapoteza dira
wanabeba mimba kwa beseni ili walipwe fadhila
wengi wanapenda kuwa mababa wanasahau ada milioni
kiburi chao shule za kata wakati walimu hawaonekani

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[MABESTE]
politics imeshakuwa polifix
rafiki wa jambazi leo kawa polisi
hadithi uongo lazima kisu ni butu
huwezi funga sonko jela tu kama wewe ni kapupu
ngojea tu ni mbichi Haijakamuliwa
na uongo una nguvu sana ukweli unabaguliwa
ndo maana maskini haki anachukuliwa
kwenye fight hivi hivi hawana nguvu wanakamuliwa
ah, watu wa chasey now wind it
ni vile vile sunday ndio kama monday
ndo maana maisha ya sasa imekuwa ngumu
ile kimiminiko si ni afadhali imekuwa sumu
life, better kwa masonko
adui wa haki TZ ni huyu Conc.
yaani corruption umpate kwa game ime go down
si ninapekwa, hii government imekaa pua
cause, msingeanza kisha later
sio gover.. tu ka' mafundi carpenter
na mimi ndio kiburi kipaza ka muhubiri
hakuna ngoja, step lazima tusibaki sifuri

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA]
Mistari yangu inamuamsha aliyelala usingizi wa pono
sauti ya ibada hawezi sikia, aliyelala usingizi wa pono
aliyeona akikuambia tofauti na aliyesikia
aliyesikia akikuambia kuna utamu kashaongezea
aliyefiwa na mzazi mmoja, siku zote hatumuiti mkiwa
wageni wana'make mshiko kwa wenyeji walipozaliwa
wanawake wana mambo mengi mi siweki dhamana
kuna mtu analea mtoto kumbe sio wake mwana
mbea anasema ukweli, ila tatizo hajaruhusiwa
na muongo ndio mzushi wa mtaa, ambaye kesho atakuzushia
maisha yalivyokuwa magumu, vijana wanakuwa mababu
mapenzi yashageuka sumu, hebu kayalambe ufe kwa tabu
miaka hamsini nikimulika, ni uwanja na barabara
town kariakoo na posta mvua ikinyesha bado msala
imani ikizidi utashi basi ukweli unajificha
tasnia imekuwa nyepesi, leo kila mtu anaigiza

[BEN]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright


sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA; Akiongea]
ha, mensen
hii track in high pitch in panic disorder!
flow right beat red nyeusi wataogopa
tyta, lunduno is in the house man
Mnazaleti, again and again yeaah

[BEN; High pitched]
sikiliza tafakari, changanua tatu mbili.. moja
subiri ubongo wako una'load..
nangonja, nasubiri, patiently...na believe
its gonna be alright

[SUMA; Fading...]
...siasa ya bongo kama soccer, ushabiki bungeni
...kuna mtu analea mtoto kumbe sio wake mwana
...ndo maana maisha ya sasa yameshakuwa...

its gonna be alright!

I am a professional lyrics by Fid Q

I am a professional
I am a professional
I am a professional

smiley faces za face
zikaitwa lyricists na racists
terrorists huniita bomb cause, i am a professional
na sio satanic verses cautious zaidi ya Titanic imezama
sio kama na flow wananiita mfalme cause, i am a professional
one of the realest illest killest cat you may see
mwanajeshi ka jeronimo plot cause, I am a professional
man who rules my government, uhuru is my lane
nam'Obama McCain cause, i am a professional
long time me i tell me coulda change dem plans
nikawa na dream ka da luther king cause, i have a dream!
na'speak in style kuwa unique, laying direct like an arrow
wananiita Malcom cause, i am a professional
Professional chuo kikuu cha ghetto nawafunza kitaaolojia
industialpolitrix hustlematrix cause, i am a professional
napima umbali kwa mwendo kisha ninahesabu siku
muda ninausoma kwa jua ni ukweli , i am a professional
na pause kama coma kwenye sentence, im the first and the second
nang'ara kama almasi girls best friend
killing the drop thats what im best at
vyema na hizi self expressions, less na mere more visions

I am a professional
I am a professional
I am a professional
I am a professional
I am a professional

ah
usiniite brief kama nike just do it, just do it
sikupaki matope kwenye hii dunia ya nguruwe
wala si stop nikiona red, natafuta daily bread
sasa im fully paid cause, I am a professional
mi ni zaidi ya bling bling magari pesa
kile ambacho hakiuzwi kwa bei ya chini and, I am a professional
Mr international Blackspot ipo pimped
usilete nyodo ka za michael Jackson bongo kuna stink!, I am a professional
panya avae miwani ukimgeza utakula carrot
you're the best of the worst and, I am a professional
sihitaji groupie love ila sababu wengi ni materialistic
naeza rudi home kwa mama na ukola unalamba lipstick
secrets wont stay secret for very long najiheshimu niheshimike cause, I am a professional
natokea mwanza home of  the greatest rappers,
mtoto wa dandu comes first then, I am a professional

I am a professional
I am a professional
I am a professional
I am a professional

Samaa X huniita Fid Q the future
machache niliyoyapitia kuna mengi nimejifunza, I am a professional
ruksa kunitoa ushamba kwa kile nisicho kijua
ntakuwa mjinga kwa sekunde kisha, I am a professional
nguvu ya elimu ina umuhimu pale elimu ikitumika
nalipwa kwa vyote ambavyo huvijui, I am a professional
muda mwingi niko sober kazi na sala kama mkoba
naamini Mungu ni mmoja ndo maana, I am a professional
tena im so grateful thankful, ili nipate mema natumia ufahamu, I am a professional
wanaongea walichosikia mi nasema nnachojua na sio ugly flow iko handsome, I am a professional
so usinitreat kama second class person utakuwa umefanya first class mistake hey, I am a professional
and im the best looking kama linen nikiwa mwendo kama Duke ukiwa kwenye mashine ah, I am a professional
HipHop ni vile unavyoishi rap ni kile unachofanya sikio la kufa zibuka usikie hizi dawa, I am a professional
katikati ya jana na kesho hapo ndipo kuna muda
kazi madeni kuzidi malipo mwiko mimi ni professional!

Kila siku by Nick Mbishi ft One, Belle 9

eyo
welcome to the booth
and love's rocking the party
im doing this for me
and im doing me for everybody
hizi ndo anasa za maisha
napuuza na black seven
mitungi ganja nyingi
madem utadhani heaven
roc boys in the building
nicki mbishi in the house
from the floor to the ceiling
girl groove and bounce
i guess you know wat im talkin' bout
mi na move gettin core
kuprove naona soo
now flow ina love
now down to the beats
hey lunduno whats up
im still rapping for machizi
mi na roll in a starlet
and in loving memory
Bongoflava RIP
call me the genius
cause no any rapper better than me
from the harper to the hyper
bado na hold the title
nakimbiza mchezoni mithili ya papa na michael
im intentionally known and Im crossing the broadest circle
nabrief na microphone wananiita street disciple
nawascratch kwenye tray kwa skillz ka steve b
biggy boss namake it rain uta game believe in me
kwa staili za kiswa kingi mentali nasaka dough
fainali ukishaitwa dingi misingi ushindwe control
Imma hustla homie, you're customer for me
nafurahi kuona you're happy but your smile is so funny
the ground is jampacked the place is going crazy
baby show me what you got
nobody just cant fade me
you made me?
ah so kweli homie i made ya
multiplatinum star sura yangu ndo front pager
na wa keep head side kwa rhymes ka mr vegas
straight to the sky na fly na den texas


tunapunguza stress kwa warembo na magambe
kila mtu yupo high club!
tunasahau shida zote tunaparty everyday
kila mtu hana time!
so lazima friday, friday
so lazima mpaka friday
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday (Its yo boy godzilla)
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday


Niko poa asee, nipo fresh asee
ukimuona duke mpe bapa mazee
cheki MVP kwenye private flights!
blaza patrick ameshawasha green lights!
kila dress code inakaa asee
ukisimama kama P mi nasimama kama J
hakuna tena ku delay
kula tungi all day
hii ngoma kali unaeza weka replay
life ni ngumu ila na fight so harder
ni kama kuwa na kesi ya first...
deeply murder!
hezilla in the house sala sala we go harder
nipo na texas yes he's my brada (brother)
ni party sio vita
leta tungi tena raundi ya tisa
huwezi kupita njia nnazopita
wizla, ha!

tunapunguza stress kwa warembo na magambe
kila mtu yupo high club!
tunasahau shida zote tunaparty everyday
kila mtu hana time!
so lazima friday, friday
so lazima mpaka friday
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday


ebwana mzuka mweke mwana nmeshtuka wajinga wanabana
everyday ni holiday sikumbuki lini ni jana
tungi stick mama duke beat na vinanda
ukae chini au juu ya kiti kama mbishi njoo na kitanda okay..
njoo unisome mi ndo kichwa cha habari
tahati hahati hapa hii ni picha ya hatari
nafunza kuandika kama teacher wa habari
tikisa kichwa tujue ka uko chicha uko shwari
sa, pisha ka mbali snitch shika tahadhari
mix teacher na kamfari upate misa na habari
nawang'arisha kama jiki au magadi
class mnafichwa ka picha ndani ya daftari
mi ndo M.I.S.T.E.R natema old skul vision kama VCR
Mi ndo ONE only definition ni HOT
They say money makes the world go round
i make it stop!


usiogope we jiachie una rock na king killer
its gettin hot in herre take off your chinchilla
today is a good day na stunt ka' gorilla
nigga get out ma way ni mbishi so godzilla
nadhibit kama X na kisha na multiply
50 kama doesnt fix kwa kiki pub iko high
sifanyi unsafe sex hata ukiwa na mtoto wa geti
isiwe grammar kisha story na habari kwenye gazeti

tunapunguza stress kwa warembo na magambe
kila mtu yupo high club!
tunasahau shida zote tunaparty everyday
kila mtu hana time!
so lazima friday, friday
so lazima mpaka friday
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday
kila siku party, party, warembo na magambe
so lazima friday [X2]

Kichaa cha Mbwa by Nikki Mbishi

yeah haha, yeah yeah
you know who i be, toka lunduno
Yeah, Bongo Jnr, Shasho
Nikki Mbishi in the Building yeah yeah
Im Busy, Im Busy, Im Busy yeah
yeah, yeah

Nakuja moja kwa moja na sishtui kama Joti
Sipumui na troti, nakata wimbi zaidi ya Boti
Nipo kifedha zaidi chagua siimbi kata noti
kukopi huogopi, msamaha hautoki kwa magoti
ubongo kamwe hausimami, sawa na meli juu ya lami
treni nje ya reli mteni we umeshafeli mtihani
sehemu kama msibani huzuni usheeni mtimani
watani msikae karibu nami mtaitonesha amani
mvua imenyeshea godoro leo unalala juu ya chaga
hutaki sakafu ipo kazi kwako kujimwaga
msanifu, sanifu lugha wanaweka nawekaga
wakuja wanazuga, wanashangaaje wanataga
nimecheza legeza lakini sio big deal
mautundu nikayaongeza kwa kuweza ku'make it real
wake up nigga buni vya kwako usipende vya kuiga
nastaajabu kuona swala anatamani matawi ya twiga
ridiculous, street wanasema nikki ni dangerous
scandalous, flow nnazotema sio weak ni tremendous
mapaparazzi wa uswazi hawapakazi
maviwako nakazi kushusha ngazi siwakatazi whaat?

kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, HEYA HEYA!
kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, MZEIYA MZEIYA!

Hizi habari za kuamina si hadithi za kakakuona
ukifa unazikwa na kusahaulika ka Issa Matona
siku ikifika macho yataongea na mdomo utaona
ugonjwa utajivika sanda kwa kukata tamaa kupona
hii mistari itagusa kila mahali,
antenna nazo bila booster zitashika stesheni za mbali
wanaostaajabu ya Musa wata..
patwa na mshangao wa samsoni miamba nikiangusha
majabali ya mfalme faraoh, na...
sibumbi stori kuteka fikra za watu kama mtungi shauri ukishtuka
umekunwa mpaka viatu, sometimes nasmoke rolls za ganja kichwa kiwe fyatu
punguza chenga tafuta goli ***********
askari acha nijipange tayari kwa shambulizi, siulizi mtanange
kiafande silali usingizi hii ndo lifestyle nnayoishi ukinifwata utapotea
usishangae nnavoitwa mbishi afu naishi kwenye ghetto ka la gwair

kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, HEYA HEYA!
kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, MZEIYA MZEIYA!

Ni kama kawa biashara asubuhi jioni mahesabu
kiuchumi sjauawa dhiki sijui shida au taabu
nacheki usawa hakuna bedui, wote wastaarabu
wanapagawa nnavocheza na chui mwenye ghadhabu
ile ki'Gangsta, fegi mdomoni moshi hewani na drive Lexus
gold shingoni kiunoni gani mziki mzito
niko high speed road inachomwa heavy mkito
namuwahi waridi baridi so narudi ghetto
kuta machizi wameshajiri na wame'settle
toka longtime wanansubiri nawapa tano
freestyle za hapa na pale natoa michano wana'smile kwa mitindo ya kale
huyu, yupi mnene yupi ni.. choka mbaya
nipo kimapene wengi mifuko inapwaya
nafanya vile navopenda kwani bongo kama ulaya
maskani kama Jamaica kuna'smell ka ya kaya
nikki, Mbishi, kwa stiki, humtishi
natapika matapishi tumboni siyarudishi
fuatilia nyendo zangu mchimba chumvi utoke dry
bye-bye, mi nawahi na fly bad dont cry

kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, HEYA HEYA!
kichaa cha mbwa ni kama cha panya buku, cha panya buku, MZEIYA MZEIYA!


ukinipenda shangwe, usiponipenda chukua time, niacheni mi niandike rhymes
Nikki Mbishi na Dunga wa Mandugu , MZEIYA MZEIYA
Kama hujui kitaa mamoshi busy, nalipresent toka lunduno Entertainme..
lazima waseme, wacheze kama sebeene, hahaha.. lets go..haha..yeah
MZEEIIYA MZEEIIYA

sihitaji marafiki lyrics by Fid Q ft Vyonne Mwale

   
CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
 udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani


VERSE1
haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao
..washkaji ambao... kosa lako lao wakati hauna mafao/wanaokufikiria wewe muda ambao/ wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao/now
kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi/
kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa/ukihit ndo unang'aa.. upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../ kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground/sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau/
wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza/
U-N-I-T na prof Ludi walionifunza kukaza...
kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

 
VERSE 2;
na usupastaa huwa ni feki.. utakung'arisha ukiwa na Market/
utakupatia senti,utapita juu ya red carpet/
utageuka young & restless, utakupa wanawake/utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake/kwahiyo power its not permanent.. huwa ipo kwa muda tu/respect ur own conglomorete... fikiri kikubwa tu/masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru/
wanazusha najiskia.. so im my own best friend/
sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/
naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship/
tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga/na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE 3
rafiki wa kweli yukoje.. ni mkimya au anayechonga/yule aliyekupa jina?au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?/au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?/ hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe/bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe/
ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?/
kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo/ inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo/unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo/urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo../
nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature/
wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger/
sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea/aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

hisia by Nikki Mbishi, Stereo, Suma Mnazaleti



yeah
yeah
yes
unga waya kwenye spika
kisha weka fire kwenye reefer
ntafutie malaya sinorita
mguu mdogo ntakupwaya kama sneeker
nafuu mgogo kuliko wahaya wanavos'fika
twende sawa, mi ni dawa kwenye fever
home sio kipawa, popobawa wala sinza
kama kawa ukipagawa nakuuliza
wazawa nawapaisha mpaka ulaya kama Visa
weka umakini kando ukose Bundle za ku'surf
dili na mgambo ili akuvunje ka bango chafu
mi ni star wa billboard na msomi mwanafalsafa
na slaa kama wilbroad
hamuoni bado mna'suffer?
hii ni original, ndo maana ina'sound kama demo
enzi hizo game iko original, underground walikuwemo
pure facts than a pure
ukimtoa duke ma'producer wengi wa bongo premature cunts
mitaani sionekani kama jini
dada yako anatamani kuwa na bwana kama mimi
mashetani yanaghani kwa imani kama dini
zao zipo hewani pole zama za 90
na pimp big kwa hisia kama Ben cussons
i think big naingia ubia na main persons
kama rapper ni soccer me footballer
the hood baller, haina ku'beep nina full dollar
don ka tage, na jambazi na blaze peace tu
dili si huna chako, ume'mess unajaza ukristu
nasema ukweli ambao matozi wanauficha
ubabeli ndo umefanya nmfeli words in picture



akili zangu sio fyatu nkisema watu sio wema
kilema, wakati hawautaki na upendo sio upendo tena
nimeona mapema, hawapendi kuona unahema labda unachechema
hauwezi unatema, ukipush unadema
mipango hiyo inabuma kisa jirani unafichwa gizani kwako
hata ukipita mibani ukatize nyikani
ili wakufute kwenye ramani, pesa ikukimbie kifupi ufulie..ka zamani
muumba akuchukie, tena akunyime thawabu, dhambi zao ulipie
mambo yakupindie bila sababu, kote wasimulie, upigwe majungu kama taarabu
hakuna ustaarabu, bila kosa wakushikishe adabu...yo
na kesho unawaza haupati majibu
unaamua kukaza na bado magumu yanasibu
unachanganya ladha tofauti za pombe balaa
usipagawe brotha jikaze ndo ilivyo mitaa
yupi utamuamini wengi wafitini ma'snitch
wapige chini treni itarudi relini skufichi
haina kufichana, kujuta kushika tama, sio juzi na jana
watu waamini kitu kazama
kichwani una mawazo demu wako keshakutosa
fedha hauna yule anazo aki'beep anatuma vocha
kata pochi upate penzi hauna kula uchochoro
utafanyiwa ushenzi kila unaporudi mgogoro
pigana na hela kisela maneno sio pungufu
ukisemwa hulazwi
songa mbele kichwa mkuki
toka, nduki! uso watupie, chuki wachukie. tena usiwanunie
sana wajutie, wakahadithie


nnachokumbuka alimuamini kama mchungaji wa kanisa
yote yanayosemwa mitaani hakujua kama yanamgusa
akaona bora afeli shule, mwisho akafaulu mapenzi
mashauzi ndo vile, mwishoni yamekuwa majonzi
hakujua yesu wa mapenzi mitaani watu wangemuita
aliyemuamini kama mpenzi kawa yuda leo yamemkuta
drop love kwenye usasa, so long ka bi kidude
unampenda kisha unamuacha, asikutapeli kama dude
leo anataka second chance ka Salvador Cerrinza
alishachezea first chance ka movie cheki anakonda
rahisi sana kukubali kile ambacho yeye anajua
hata kama atakuja feli kwa vitendo sio kuongea
anakumbuka game tough yeye na mpenzi walizocheza
leo ana'drop kama clove, uchaguzi daily wanammeza
kila anayesoma likizo sio kweli kwamba ana supp
watoto wanawapita kiuwezo watu wazima mpaka wana'STOP!
AH, we utaona unapendwa kumbe ndo unachunwa
we unaona unapanda kumbe ndo unavunwa
ushambandika kama sticker ukimbandua ndo unasepa
usije ukatekeka akakumwaga ka ana tipa
ah, nilipendwa mpaka wapangaji nyumbani wakawa wananuna
leo love imegeuka mtaji kwenye mzani watu wanapima
sio siri haya mambo nimeshayaona kijana
demu fulani kamteka mwana mpaka mia anabana
washatumia sana pesa kisha wakaja achana
demu kahongwa mpaka chaser kumbe kuna boya anambana
sio kila anayebeba begi ukadhani shule anaelewa


hii ni siri yenye laana kama tupu ya mzazi
kwa roho mkunjufu sitoruhusu utundu wazi
sizungumzi na mwana, nazungumza na mzazi
huu uzungu wa kuuzana kama ruzuku ya jambazi
kumbuka, wema watoto wakwepe mkosi
baba ana nyumba ndogo kigezo kubwa haitoshi
anazuga anakupa support Yuda eskarioti!
pochi inashinda kwa mchumba bi mkubwa ale karoti
ona kijana amekosa malezi kisa mama hana uwezo
baba yupo kwa mpenzi lisa, ama baba hana uwezo
na mama haiwezi shida enzi zimepita kisa ana mpenzi wa kumridhisha
kumbuka, haya maisha safari, pole kwetu waliokufa wamemaliza tayari
wasifasifa sio sifa jijali, njoo pata maarifa hii taarifa ya habari
ona watoto wanaomba wanakosa na wana njaa kwasababu wazazi waliponzwa
na tamaa
hili janga la jamii sio janga la jamaa, binti mwenye kilanga
kalamba dume la mtaa, hii ni.. kwako wewe rafiki ya kujihami
kama huna nia njema huwezi kuwa jirani
sina imani nawe usiwe na imani nami
kama sote si wanyama mi ni simba we ni nyani
ila usilie mama, kaza moyo we shujaa
ingawa dhiki iko uraiani naimani imeshiba njaa
kuwe na imani ile amani ipate nafasi
mchunge mwana wa jirani asidanganywe na fataki

playboy lyrics by Nikki Mbishi

yo
kama leo
umeni'call kwa geti yo si ipo kesho
Before the night falls tuifanye iwe siku special
usiku ukapita kwa vita dhidi ya usingizi
na ndoto zisizokwisha natishwa na Jinamizi
masaa yakasogea nikiwaza jinsi ya kutoka..
Peke yangu ghetto naongea na suti na pair za mocca
nna'dress, nafunga mlango natoka, naingia parking
??the place ready on silence nowhere the dog was barking
mwana nawasha ndiga saa 'saba za pm'
nagundua sina akiba nacheki na ATM
na'draw za kutosha naliona duka nashuka
naongeza vocha napiga ananjibu 'bado nasuka'
namwambia ukimaliza nishtue mi niko njiani
pia wakati nakuja unataka zawadi gani
akasema 'yote uipendayo njoo nayo mi ntaipokea'
Usiendeshe gari kwa spidi, 'see you baby take care!'
siku ikazidi fana kimwana alinidhibiti
nikafanya shopping ya maana, lelana
na mlimani city, kama twiga bata
figure matata mithili ya grace, anapiga anakata
grigi alidata na baby face
nchi ya kusadikika ntaku-'treat'ije this way?
wasaa ulipofika malaika aka'display kiss na hug za nguvu
like hey baby i miss you
??nkasa ukofesafiri niskize nikupe ishu


sijawahi kupenda na wala sijui mapenzi na siwezi kumuenzi love cause
Im a playboy
usije ukanipenda nitakuumiza nitakutenda sipendeki nitakupa taabu cause
Im a playboy

sijawahi kupenda na wala sijui mapenzi na siwezi kumuenzi love cause
Im a playboy
usije ukanipenda nitakuumiza nitakutenda sipendeki nitakupa taabu cause
Im a playboy

yeah
kimtego akavuta kiti akapozi muhudumu akaja
nikaagiza chupa ya baccardi na mbuzi wa nusu paja
kazi na dawa, pombe na nyama, utani na story
anacheka utadhani fetty, na of course she spread it jollily
mvinyo ukapanda kichwa sistaduu akaanza visa
nikahisi nikipotezea ataniona nyoka wa kibisa
mashauzi ananiletea, na blouse mbele ime'diss
ikabidi nikakodi uwanja ili nyavu niweze tikisa
mrembo hakuleta utata swadakta akazama ndani
alipovua si ndo nikadata nikapata ladha duniani
shughuli pevu brotha kaka akajihisi yuko nje ya sayari
nikampiga 'starter' na memory ndani ya diary
akatoka na star, shobo zikaponza mwili
wakati playboy, silali na demu mmoja mara mbili
siku tulipoachana ndo mwisho kuongea naye
akipiga nakata, nikipokea piga baadaye
ikabidi atimbe maskani lunduno kuniulizia
akaambiwa yuko nyumbani, na shemeji ametulia
akajiona hana thamani, nguvu zikamwishia
kwasababu nishamtumia, kimsingi ameshafulia
akaja kwa dhumuni akitaka kufumania
nikamtolea mbavuni, machozi akaanza kulia
akitaka penzi la amoni, ambaye sijatulia
mwenzake akaja ubavuni kimahaba akanikumbatia


usipagawe na usanii mi sio kioo cha jamii nitakugeuza big G cause
IM A PLAYBOY
Radio Tv ishi ABC kuna HIV cause
IM A PLAYBOY

usipagawe na usanii mi sio kioo cha jamii nitakugeuza big G cause
IM A PLAYBOY
Radio Tv ishi ABC kuna HIV cause
IM A PLAYBOY

usipagawe na usanii mi sio kioo cha jamii nitakugeuza big G cause
IM A PLAYBOY
Radio Tv ishi ABC kuna HIV cause
IM A PLAYBOY

usipagawe na usanii mi sio kioo cha jamii nitakugeuza big G cause
IM A PLAYBOY
Radio Tv ishi ABC kuna HIV cause
IM A PLAYBOY

chukua time by suma mnazareti ft Ommy Dimpoz

nenda sepa, leo nimekushtukia
usitaki tongo, si ulikataa
nenda sepa, nani unamwita dear
usitaki tongo, acha tamaa

chukua time, chukua time
chukua time, time time time
chukua time, chukua time
chukua time, time time time


ah,  
nillikupenda sana, kisa sio star ukanitosa bwana...mh!
enzi hizo miss bwana, mtaani uliniona ka' shabiki sana...ah!
una pub ndio, tena we ni star wa bongo movie sio....umesahau!
nilikutaka ndio ukanitosa kisa upo kwenye cover sio....kwa dharau!
we ni model pia mpaka, asanali anakujua
nilikutaka pia enzi za chuo we ndio ukawa unajisikia
huu mziki kipaji, show ya kwanza uliniona mzugaji...ah!
wivu wa kwanza mtaji, CD yangu ukaimwagia maji...mh!
mi na upendo ndio, ila haya mapenzi nayaona sio...eti!
alinihit ndio, niwe nawe, ili kesho utambe kwa wenzio
sitaki!


nenda sepa, leo nimekushtukia
u-sitaki tongo, si ulikataa
nenda sepa, nani unamwita dear
u-sitaki tongo, acha tamaa

chukua time, chukua time
chukua time, time time time
chukua time, chukua time
chukua time, time time time


ah, 
nikiwa nawe nitahit ndio, kwa tv magazeti na redio
miezi sita haupo, mshamwagana kashuka chati kwa skendo
kwa style hii hunipati, ah we tapeli mzugaji
eti unapenda nyimbo yangu mh, nakujua muuaji....ah 
mie sikutaki ndio, nilivyotoka nilikuwa na mpenzi ndio...maana
niko hapa leo, alinipenda hata kabla sija'hit mwaka jana
umenitunza ndio, kwenye noti umeweka namba ili iweje sio...ah
mie situmiki hivyo, hata kama nina njaa hunipati hivyo....eti
nilikutaka mimi ukakataa, kisa sio star sina chapaa
leo niko hit unashangaa, shobo zimezidi mh nakukataa
nilikutaka mimi ukakataa, kisa sio star sina chapaa
leo niko hit unashangaa, shobo zimezidi mh nakukataa


nenda sepa, leo nimekushtukia
u-sitaki tongo, si ulikataa
nenda sepa, nani unamwita dear
u-sitaki tongo, acha tamaa

chukua time, chukua time
chukua time, time time time
chukua time, chukua time
chukua time, time time time

mdananda lyrics by Shetta

(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda

(verse1)
anapenda ku'bang anakazi huyu jamaa, na ma'star kadhaa wenye jina ndani ya Dar
si nikajaa mi mzawa wa Dar na nikaachwa kwenye mataa
Nashangaa namba zake nimezidiwa mang'aa mashaka alikuwa kando
Nilihisi mchizi Bonge la mwana, ah Kumbe mgambo
Vitani hawezi kushika zana, ah kweli kufa kufaana\
Nimeamini ya leo sio ya Jana {kweli ya leo sio ya jana}
Vizuri kufa na Ujana, ila Life ya dunia ni tamu sana
hizo sekunde na dakika bora zingerudi nyuma
niwe bonge la bitozi hata salamu ningeuchuna
Mbio zimegonga ukuta, kusanuka kishanuka na matuta nimeruka nimeanguka siwezi tena nyanyuka
hata, hata shabaa alinitonya wewe ni rafiki bar
nikapuuza kwakujua na mzawa wa kitaa
ghetto la darstamina pia nikalitaa nilihisi kama nabanwa
si ni wewe nilikulea ukiumia na'feel pain
utetezi juu yako kama jeshi la UN
Ulidaiwa sikusita kukulipia madeni
leo iweje uniingize mkengeni

(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda

(verse2)
Nilikuwa ndani ya ghetto na'settle mipango ya kesho mara ring ring
kucheki alikuwa mwana, story ilikuwa hivi nanukuu Michapo
"mwanangu sio siri una zali la mentali
kuna binti mtaa wa pili anadai anakukubali
anasema nyimbo  zako unajua panga mistari
Tajiri, hatari wekaa tuchume mali
isitoshe ana figure matata hana dosari
hata leo tukienda atakuhonga hata gari
kifupi sijajivunga na pozi zilikimbia
ghorofa nilionao mnyamwezi nikajitupia
pe..pendo ulikuwa faster kama goli la feste
tuliishi kwenye bungalow sio nyumba za gesti
shida nilizishinda hata kwa manji navimba
kumbe nimepewa goma limepiku si..
yule dada mwathirika nimetumika bila kinga
na mchizi alishajua nnapotimba nachinjwa

(chorus)
Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
we si rafiki
mbaya sitaki
nasema sitaki
sitaki yuhaki
mnafiki rafiki gani mdananda

agano jipya by suma mnazareti ft Staminah

[Suma]
Mistari imejaa ubabu, hadi mababa wanaamkia
ubibi kaitaka haraka, watakimbizwa hadi atalia
kama kila awamu walikula, awamu ya nne wamekomba
madogo wameiteka dira, watu wazima game mtasanda
utanganyika una kivuli cha ujinga tabu na shida
kijana akivaa msuli, basi ujana ushampoteza
nauli imepanda kidogo, kigamboni watu wanalia
bush ashabanwa ule mchongo, soon wataanza kuogelea
maduka ya dawa za siri, wateja wakubwa madada
ukihonga honga kiakili, usije ukadhani ulipendwa
money iligeuka power, ghadaffi akaachia nchi
wageni wanatesa wazawa, kariakoo imekosa weusi
mi nahitaji namba kumi, sio moja ntakosa stand
viongozi wameanza na umimi, hili taifa wanaliweka bond
tamaa ikizidi uwezo, mwili lazima utumike
shida ukii'use kama kigezo, hiyo sketi lazima ishuke


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah

[Staminah]
hii sio system ya madilu, haina shobo kwa mademu
kingunge mtafute mwiru, ngombare ashasanda game
mistari sukari guru hii lazima itakunogea
ila mashaka yatakudhuru, usijaribu ku'compare
mzungu akijichubua ujue moyoni ana uAfrika
dogo usikimbilie kukua, omba wakukubalie kifikra
vesti ya mcheza summo, betina lazima ikupwaye
kitambo kama gurumo, mabeste nicheki baadae
kila mwembamba ni model, sharo usiishi kiisidingo
na kifo ndo mwisho wa nyodo, jipange uache maringo
nimezaliwa jangwani, kivipi unitishie ukame
mkulima, rudi shambani hii ndo mundu ya machame
kabwela, mwenye kitambi bepari utamtesa nani
kokote mi kwangu kambi, anthony unipe ramani
sadaka ni sadaka ila zaka iende kweisaka
mamlaka yenye dhihaka, nasaka mpaka waraka ah


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah

[Staminah & Suma]
Ndevu zingekuwa ndio kimo, Osama asingeujua ugaidi
na mvi sio utu uzima, jipange uache ugaidi
juisi haipashwi wala mstimu haumwagiliwi
bubu acha magumashi, chunga usimfokee kiziwi

wanataja walikotokea ili waongeze mashabiki
mi kwetu ndo mwisho wa reli, ukifwata level hizi hufiki
ustaa bongo unapeperuka, ka trouser bwanga ya loketo
so ukipata weka jenga, ili kesho wasikuite kapeto

ukikumbuka ulikotokea, maasai utachana chupi
na usiogope kupotea kama njia huikumbuki
darasa, bila dawati gonga nyundo ya kilimo
mchungaji, tumia torati shetani akija na mzimu

yeah
upendo penda unapopendwa, usipopendwa stress zinatosha
upendo wa mke umezidi ndugu, mama mkwe mpaka kasusa
cha maana ndo chenye maana, kwa wenye maana bila dhana
wachanaji sio wale wa jana, wanaochana leo wana laana


tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
moro na kigoma majembe ndo tuko mjini
[umetusoma, hujatusoma sikiliza track kwa makini]
[sema yeah!] staminah na mnazaleti
haina kupoa kila mchongo unajiseti
[sema yeah, staminah na mnazaleti] ah ah, ah ah


songa lyrics by songa

[Intro]
Yeaah… Duke Tachez.. yeeah

[verse1]
Yeah, kwa uzima nafungua kinywa nachomoa hii habari
Naisoma kwa kina vina vinatoboa ka’ bikari
Nimepima homa kwenye roho ya hii sayari
Wanasema n’na ngoma eti nakohoa mistari
Sihitaji support kupost stanza nia
Verse ni lugha mbili ka’ noti ya Tanzania
Vibaraka wana njaa, bosi anawaza mia
Ni mkosi balaa, kitaa tozi anatanga njia
Mbwiga hasifiki kwa ubingwa wa busara
Ukiona giza na jogoo haliwiki ujue mida ya kulala
MC vipi? Mbona huwakilishi shida ya fukara?
Au umeshapata tija umesahau tiba uchwara?
Mdomo… hauachi tathmini ya amani ya mswaki
Mtoa roho angepokea rushwa maskini gani angebaki?
Stuck kwenye move mi’ ni mkali kwenye flow
Na-scratch maujuzi m’ ni chaki we ni black wall
Mzungu anaiga kwenye shida ndugu Mungu,
Narusha machungu zaidi ya miba ya nungunungu
Nyoa dungu huu ni msiba mbwiga tubu
Nimeshika rungu nyumbu anasinywa ka’ sungusungu!

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

[verse2]
Wazazi wanasema nimeshakua
Ina maana… vibaya na vyema nimeshajua
Jua linazama tazama inanyesha mvua
Nakesha kwa dua kumuombea anayekesha akivua
Alfajiri inafika na mwezi unazama
Jogoo la Mbishi lawika na wezi wanahama
Yamaanisha zienzi tenzi kwa ujenzi salama
Uweze chutama japo kuna washenzi wanabana
Wanasema mi’ ni mkali ila why sisikiki?
Bei ya sukari inafanya ninywe chai na pipi
Rafiki… mnafiki hanifai kwa dhiki
N’nachomshukuru Mungu tu uhai silipii
Cheza pazuri, ukiweza eneza kauli
Wajinga wanatoa macho ka’ wamepoteza nauli
Tenzi shule kwa hizi tungo nikumbuke
Hizi verse nagawa bure kwenye midundo ya Duke

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

[verse3]
Baba ananiambia… Maneno hayavunji kuti
Sawa nachana ila mbona flow zangu hazifumi suti
Mi’ mweusi roho yangu haifugi chuki
Dada anasema usiposoma mdogo wangu utarudi bushi
Meza ukweli kwa pressure uteme uongo
Palla anasema Mhaya nd’o kauleta umeme bongo
Kama husajiliwi jitahidi uchenze ndondo
Mwema Mungu sio Said anayesema ubebe gongo
Sifuri ndio inaanza na moja ndio ya pili
Cha ajabu ya pili inaanza na kwanza inasubiri
Hoja ya kishamba haina haja ya kuijadili
Hii ni hoja ya kijanja pata stanza na akili
Hii mic ni shamba na mimi ndio mkulima
Navuna ninachopanda na ulimi ndio unalima
Hapa utaganda huu sio Umwinyi na Ujima
Mzazi mwambie mwana mjini si pa kupima…

[chorus]
Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

Niite SONGA!
Kanuni ya harakati,
Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
Niite SONGA!
Thamani ya muwajibikaji,
Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

miss Tanzania lyrics by Solo Thang




(verse 1)
BABA YAKE ALIKUA MKOLONI KIPINDI HUYU MISS MWALI
MCHONGA ALIKATA UTEPE LAKINI HAKUVINJARI
SABABU ALIKUA BUSY KUMLINDA NA GETI KALI
KUMBE WENZAKE WANABINJUKA KUSHTUKA AKAKAA MBALI
DEMU ALIKUA NA HESHIMA KABLA HAIJATANGWAZWA RUKHSA
CHUKUA CHAKO MAPEMA UKIMKONYEZA TU UMEGUSA
ANA KIFUA KIMEBETUKA SIO MAZIWA NI MADINI
KAYAACHA WAZI WATU WANASHIKA HAPO NDIO ANAPONIUDHI MIMI
WATU WANAGONGA TU IKULU TENA KWA MITINDO HURU
KAVU KAVU BILA KINGA HAJALI VINAVYODHURU
KAWA SHANGINGI NA AMEDATA HANA UWOGA WA KUNGURU
ANAPENDA SANA CHAPAA HAIMTOSHI KODI NA USHURU
ANA KIJUNGU MATATA LAINI KAMA NYANYA MASALO
ANATINGISHA AFRIKA NZIMA NA MZIGO KILIMANJARO
USIMCHEZEE KWA VIDANI SIO PETE SIO HERENI
ANAMILIKI TANZANITE KAMA ARDHI YA MERERANI
SURA DHAHABU INAITA KAMA AMEZALIWA GEITA
TATIZO NDIO KICHECHE KILA MWANAUME NDIO AMEPITA
HATA BENJA HAKUTOKA KAPA HUYU DEMU HAJATULIA
KAMA RUSHWA NDIO KIKWAPA ANANUKA NA KUNUKIA



(CHORUS)
miss Tanzaniaaaa
nakupenda ila hujatuliaa
vitendo vyako sitojivunia
sifa yako kubwa umefulia
MISS TANZANIA

(VERSE 2)
BORA ANGEBAKI KUWA MODO KAMA FLAVIAN MATATA
ILA DEMU AMEJIACHIA KISA ANAENDEKEZA BATA
SITACHOKA KUWAKILISHA JINSI ANAVYONIACHA HOI
JUZI JUZI KAOPOLEWA NA HANDSOME BOY
KABLA HAPO SHOGA ZAKE WOTE KASHAWAONA MABWEGE
SABABU HAWANA DIRA NA YEYE AMESHAHONGWA NDEGE
ANAFAA KUA MISS DUNIA MAANDALIZI LONGOLONGO
TATIZO ANAKULA SANA AKIJAMBA NI SONGOSONGO
MARA GHAFLA KANENEPA KUMBE MIMBA B.O.T
KUMBE DEMU ALIGAWA EPA WATU WAMEPIGA HAFU JII
ALIZUGWA NA AKAUNT HEWA KUWADI BWANA BILAL
MARA MDOMO NAE KAZIMWA BILA HATA PICHA YA KABURI
KINACHOMPONZA HUYU SHAWTY UTULIVU SIFURI
ILA HAKUNA ANAEPINGA KWAMBA HUYU DEMU NI MZURI
MIXER SIASA NA BIASHARA DEMU AMESHAKUA CHOTARA
MISHE ZA DAR AKIMALIZA MJENGONI ANAKWENDA LALA
KADRI MIAKA INAVYOKWENDA DEMU ANAZIDI FULIA
KUMBE WEUPE NI MKOROGO ONA MWILI SASA UMEFIFIA
DEMU KAZIDI UMALAYA WACHA MABWANA WAMTEME
HAOGOPI KULIWA MTUNGO KISA NAGAWA UMEME

(CHORUS)
miss Tanzaniaaaa
nakupenda ila hujatuliaa
vitendo vyako sitojivunia
sifa yako kubwa umefulia
MISS TANZANIA

(VERSE 3)
WADAKU WALISHAMFUMA ANAKULA DENDA NA RICHMOND
DOWANS AKAZIDI KETE AKAMVISHA PETE YA DIAMOND
BINTI MASKINI AKANASA BWANA MSHENGA NDIO LOWASA
SHEMEJI HATAKI HATA PICHA NDIO TABIA GANI SASA
NDOA ILIFUNGWA KWA VIFIJO VIGOGO WAKALA PIZA
KEKI NZIMA WALE WAO SHARE YETU SI NI GIZA
SIO HAYO DEMU ANA MENGI YA KUCHUKIZA
MALI GHAFI ASHAZINADI FORSALE ANAJIUZA
MTAANI ILIVUMA RUMOR DEMU KAWA MAMA HURUMA
UCHUMI UMEFUNGWA DRIP MAEMDELEO NDIO KALI HOMA
MALI ASILI NDIO KITASA KILA UFUNGO NDIO UNAPITA
TOKA ALIPOVUNJA UNGO NUSU KARNE IMESHAPITA
MAPENZI KAFANYA MRADI ANAMEGWA NA MAFISADI
AMANI KWA TIME BOMB BINTI AMEKUMBATIA RADI
VITENDO VYAKE VIBAYA VINAFANYA ADHARAULIKE
TABIA KATIBA SIO MSAHAFU NDIO USEME ISIBADILIKE
MIKOSI INAYOMKUTA NDIO KWANZA ANATABASAM
HAJALI WALIOMZUNGUKA KAMA NAO BINAADAM
MBAGALA WALIMBAKA MPAKA AKAMWAGA DAMU
NA JUZI GONGO LA MBOTO KAANZA KUJAMBA MABOMU

haturudi nyuma lyrics by Juliana ft Kidum

Mpenzi, Mpenzi
Mpenzi wewe (wewe)
Mpenzi wewe Mpenzi wewe
Mpenzi wewe Mpenzi wewe (eeeeh)
Verse 1
nieleze vipi mimi ntaweza kuishi bila wewe
ukiniacha ukienda zako, penzi wewe
kama ni ukweli, yale nasikia kwa majirani
ya kwamba utakuja kwenda zako
uliniahidi, tutakuwa tukijadiliana
na maswali yangeleta utata
kwa nini chinichini
unanificha yanayokusinya
lakini unayosema, ni majirani
kwa nini kando kando
unanificha yanayokuudhi
lakini unayateta kwa marafiki

ukiniacha mi ntalia
ukienda zako ntabaki naumia
kama ungelijua
uoga ni lao, kukupoteza
ndio nasema, baby

Chorus
nakuomba please ubaki nami
nasema penzi
nakuomba ubaki, tujaribu tena, tunayo nafasi
ya kuanza tena
tunayo nafasi
ya kujikosoa, haturudi nyuma kamwe
haturudi nyuma kamwe

Juliana wee

Verse 2
watu wanasema kama karibuni wee unaoa tena
ya kwamba nianze kujipanga
si ukweli, nimekataa
ni tahadhari kubwa kwangu, na unanitisha
sijui nimekosea wapi
uliniahidi
kama kila jambo lote la nyumbani
ni muhimu kuliweka wazi
Ni kuki shenge
Uguma buri gihe umbabaza
Kandi uzi ko ngukunda
Ni kuki rukundo
Uguma untera umujinya
Ukica amatwi ngukunda

ukiniacha mi ntalia
ukienda zako ntabaki naumia
kama ungelijua
uoga ni lao, kukupoteza
ndio nasema, baby

Chorus

nakuomba please ubaki nami
nasema penzi
nakuomba ubaki, tujaribu tena, tunayo nafasi
ya kuanza tena
tunayo nafasi
ya kujikosoa, haturudi nyuma kamwe
haturudi nyuma kamwe

kabwela lyrics by stamina ft rich mavoko


nimepigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi
maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli
dunia tambala bovu nalidekia kwa shida
jitahidi kui'solve bila kutumia four figure
natamani nisimame ili nione magharibi
moyo umejaa ukame kuhema unajitahidi
macho yote yana ukungu utadhani chungu cha bibi
nataka, kumuomba mungu shetani ananzidi spidi men
vizuri viko wapi navisaka havionekani dah
napata makapi vinono navitamani
sina baba, sina mama, sina babu sina bibi
uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi
umaskini unanipodoa, bila kutumia cosmetics
daily unanizodoa, unanivuta bila magnetics
maisha yangu hayana swagga kama mmasai wa Njiro
Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo
dah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela


sikusoma, kitajiri kichwa kimejaa madufu
maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua lufufu
naichora, lami na mkaa kwa kudhani nitaona chochote
atleast, basi ningekaa nisingeitwa kiokote
pesa imegeuka yuda, daily inanisaliti
mishale inazidi muda, utajiri unaninyima seat
maisha kama gwaride, kuna wa mwisho na wa kwanza
ikisikika nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza
taifa la kichwa changu Raisi wake naona kichaa
na kitabu, cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa
ah, napatwa wazimu shida zinanitia madoa
pesa imekuwa adimu kama bikra kwa changudoa
banda nnalofugiwa sihemi halina dirisha
wasichana wananikimbia wananiita nyoka wa kibisa
msosi wangu sio wa drafti sili mpaka nijitume
maisha yana super shaft yashanizidi nguvu za kiume
dah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela

(http://www.thebongolyrics.blogspot.com/)

ushindi wangu ni wa uchafu kwenye vita ya wasafi
kila nnayemuomba tafu anataka afanye na ulafi
maisha ni kombolela masikini ndio mlinda kopo
cha msingi ni kuunga tela mpaka utoke kwenye msoto
kila jua linapozama natamani pasikuche
hasi inageuka chanya kapeto  anageuka sunche
naona alama za mlango ila sioni pa kutokea
hii pesa imetoka jando inataka kuni-babu seya
nimegeuka konokono natembea na  mzigo wa shida
silali, nimekuwa pono maisha unakwenda na mida
shida zishanipa ustaa, zaidi ya kanda ya loketo
tumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto
vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani
na vijiko vya uhalifu nishaviweka kwenye sahani
mi nadhani, haya maisha yana ramani
na aliyewachorea masikini peni ilimgomea njiani
ah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela