DIAMOND
Hivi nyie ma MC, mnachoimba kitu gani
Mara Bangi, mara matusi sa ndo muziki gani
NEY
Hii ni Hip Hop, H.O.P
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi
kabane pua nyumbani
DIAMOND
hata bibi yangu mi aliniambia
mwanamke anahitaji kubembelezwa
Kupeti-peti matunzo pia
ukienda rafu utampoteza
Muziki ni mfano wa binti muzuri
na ndo maana namtunza kwa vazi la utuli
NEY
ah piga kimya, we ndo hufai kabisa hauna maana
wabana pua kila siku mnalogana
Bibi yako alikuambia muziki ni kama binti
Mbona unawachezea unawatema kama Big G
Mara Wema, Mara Jokate, Mara Naj, Mara Penny
Je mnafanya muziki mpate mabinti?
DIAMOND
uhh, hata wazee wa zamani, walishasemaga kazi na dawa
cha muhimu jukwaani, ni kuhakikisha wanapagawa
ule mchezo wa kuringaringa, ndo huwa wanadata
badilika usiwe mjinga, utawakamata
Hivi nyie ma MC, mnachoimba kitu gani
Mara Bangi, mara matusi sa ndo muziki gani
Hii ni Hip Hop, H.O.P
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi
kabane pua nyumbani
NEY
Mziki wenu ushirikina, ndo umetawala
Q-Chillah analalama, anasema umemloga
Mganga wako aliyekutoa, umemkimbia hujamlipa
Bila skendo za magazeti, basi husikiki
DIAMOND
ah, mi ni mti wenye matunda, milele siogopi kupigwa mawe
Ubaya wenu wengi "kayumba", elimu mlitupa sadakalawe
NEY
bado hujanishawishi, bongoflava inanipa kichefuchefu
kwanza nyie malimbukeni wa umarufu
mnaleta maringo mpaka kwa mashabiki
wabana pua nyie watoto sio ridhiki
mnavaa nguo za dada zenu, zinawabana mapaja
Nyie makakaduu
NEY, DIAMOND
ah nyie watoto mchelemchele...haya matusi bwana
kwenye show viuno mbelembele... mbona unatutukana?
ah nyie watoto mchelemchele...haya matusi bwana
kwenye show viuno mbelembele...
Nimewanyamazisha, Brazameni vipi we bado unabisha?
DIAMOND
hata mimi nina mengi ninayajua, ila we mtemi utaanzisha utata
michezo yenu kutoboa pua, bora ninyamaze usinipige mbata
Hivi nyie ma MC, mnachoimba kitu gani
Mara Bangi, mara matusi sa ndo muziki gani
Hii ni Hip Hop, H.O.P
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi
kabane pua nyumbani
Hivi nyie ma MC, mnachoimba kitu gani
Mara Bangi, mara matusi sa ndo muziki gani
Hii ni Hip Hop, H.O.P
Waasisi wa Burudani
Tushachoshwa kutwa mapenzi
kabane pua nyumbani
No comments:
Post a Comment