ALICHOKIJIBU AFANDE BAADA YA CHIDI BENZ KUMJIBU




Baada ya juzi CHIDI BENZ kukubali kwamba
 pamoja na AFANDE SELLE kumdis, yeye bado 
yuko tayari kufanya nae kolabo ambayo alipanga
 kufanya na Afande wiki moja au mbili kabla hajamdis,
 Afande nae ametoa sentensi ya jibu kutokana na alichosema 
ChidiBeenz.
Afande amesema “yeah mi niko tayari, niko pamoja nae Chidi
 anajua hilo, na hiyo kitu alishaniambia kitambo tukapanga na
 mimi bila shaka matatizo yaliyotokea ni mambo ya kupita lakini
 mimi wimbo wake hata kesho nasububiri beat niandike tufanye 
kitu kilichobora zaidi nafikiri itakua na maana kuliko malumbano 
malumbano yanayoendelea haya sio mazuri, sina beef nae”
Chanzo cha beef yao ni baada ya Afande kuhojiwa East Africa 
Radio na kufananisha kuondoka kwa Ditto  watu pori kwenda
 La Familia, sawa na kuondoka Manchester United na kwenda 
timu ndogo kama Bolton, maneno ambayo yalimkasirisha sana Chidi Benz.
story na milardayo.com

Je! Beef hii ni Dar dhidi ya Arusha?




“These rap cats softer than a new born baby bottom... Eti big fish in this ocean... My pussy cat eats that shit..” Ni maneno yanayosemeka katika ukuta (wall) wa Harry Kaale maarufu kwa jina la One The Incredible aka Moko wa Miujiza. Ni fataki alilolielekeza kwa Joh Makini kuashiria kuwa vita katika ya Weusi kundi huru linalojumuisha rappers kutoka Arusha ambao ni yeye mwenyewe Joh, nduguye Nikki wa Pili, Gnako, Bonta aka Maarifa, Lord Eyez na wengine dhidi ya Nikki Mbishi aka Baba Malcom na One the Incredible na washirika wengine wa Lunduno na Illmatic imeiva.     
     
Chanzo cha ugomvi huu wa kimuziki kati ya pande hizi mbili unaaminika kuanza katika kipindi cha mwaka mmoja na kitu uliopita.  Katika mazingira mengi ya kuzuka kwa beef za hiphop mashabiki huwa na asilimia nyingi za kwao zinazopelekea wasanii fulani kupaniana kiushindani hali inayosababisha beef ya kawaida ama kali. Jina la “Nikki”ni sehemu moja wapo ya kuwepo kwa tension kati ya Nikki wa Pili na Nikki Mbishi. Watu walianza kumsikia kwa ukamilifu Nikki wa pili katika wimbo alioimba na ndugu yake Joe Makini “Niaje ni Vipi” . Hapo ndipo mashabiki wa hiphop Bongo wakatambua kuongezeka rasmi kwa orodha ya wasanii wenye uwezo mzuri kiuandishi nchini wanaotokea Arusha. Baadaye Nikki wa Pili alisimama mwenyewe kwenye ngoma aliyomshirikisha Rama D “Good Boy”.
Kwa upande wa Nikki Mbishi, safari yake ya kuwa nyota katika hiphop ilikuwa tofauti kidogo. Yeye alianza kujulikana nchini kabla hata hajaachia wimbo uliorekodiwa na kusambazwa katika mkondo mkuu wa muziki wa Tanzania. Nikki Mbishi alijizolea umaarufu katika kipindi cha Bongo Flava cha Clouds Fm kwa uwezo wake wa kuchana ,mitindo huru (Freestyles). Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu kwa ukaribu, wanasema Nikki Mbishi ana uwezo wa kurap kwa freestyle kwa masaa kadhaa bila kurudia mada na ndiye msaani ambaye One anamhofia kuliko wote nchini.

Baada ya kuvikwa taji la mchanaji bora wa mitindo huru enzi hizo, Nikki Mbishi aliongezea msumari mzito kwa mashabiki wake katika wimbo wake wa “Punch za kwenye Line”  Kama jina la wimbo unavyojieleza, wimbo mzima ulijaa uandishi mzito unaohitaji muda mrefu kuchambua na kupata maana halisi ya kila alichokuwa anatema (spit), sifa ambayo imekuwa ikipelekwa pia kwa maswahiba wake One na Stereo. Mashabiki wa wasanii hawa wanaofanana majina ya mwanzo wakawa na shauku ya kujua uwezo wa kila mmoja ili kupata jibu na ni mkali zaidi ya mwenzie. Jibu wanalo mashabiki wenyewe. Lakini hapo ndipo story hii iliyotawala vinywa vya mashabiki wa hiphop nchini, vituo vya radio na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa sasa kuhusu beef kati ya Weusi na Nikki Mbishi na One ilipopandikiza mbegu zake.

Kwa mujibu wa story za chini kwa chini ni kwamba Nikki Mbishi alimshirikisha Rama D kwenye chorus ya Punch za Kwenye Line lakini baadaye Rama D akaomba kuondolewa sauti zake kwenye wimbo huo kwakuwa hakutaka kugombana na Joh Makini ambaye inasemekana hakuwa anampenda Nikki Mbishi. Kutokana na uamuzi huo wa Rama D, Duke ambaye ndo producer wa wimbo huo pamoja na uongozi wa MLAB wakaamua kumchukua Grace Matata kufanya chorus. Kwao MLAB huo ulikuwa ni uamuzi uliofanyika kwa kutopenda kwakuwa Grace kipindi hicho alikuwa bado msaani mchanga na asiyejulikana kwa wengi kama ilivyo sasa.

 Baada ya hatua hiyo kukaanza kuzuka maneno kutoka kwenye kambi ya River Camp Soldiers na kuonekana kuwepo uwezekano wa kambi hiyo kuwadiss Lunduno (kundi huru lililopo maskani wanapotokea Stereo na nikki ambao kwa sasa wamejitoa). Kambi ya Lunduno kupitia One ikatupa jiwe lake kuelekeza kwa River Camp soldiers ambao kwa sasa wapo ndani ya kundi kubwa linalowajumuisha pia member wa Nako 2 Nako liitwalo “Weusi”.

Kwa mujibu wa mahojiano na Clouds FM, One alidai kuwa alirekodi wimbo katika studio za Tongwe Records ambayo kuna mstari unasema siwezi kuuza kura yangu kama Bonta akimaanisha wimbo wa Bonta uitwao “Nauza Kura”. Pamoja na dongo hilo lililoekezwa kwa Bonta, hakuna jibu la wazi kutoka kwa Bonta zaidi ya kujibu “Sina tofauti nao” alipoulizwa kuhusu msimamo wake.

Katika mahojiano hayo One alisema anashangaa kujikuta yupo kwenye beef na Weusi wakati anawasiliana mara kwa mara na Joh Makini pamoja na Lord Eyez ambao kwake ni kama kaka zake kimuziki. Japokuwa kauli hii ya One inakinzana na status yake hapo mwanzoni kabisa mwa makala haya ambapo anamdiss wazi wazi Joh Makini.

Mahojiano hayo yalifanyika kutaka kuwepo ufafanuzi kuhusiana na status ya facebook aliyoiweka jumatano (28/03/2012) iliyosema: “Niki wa pili: sijakutaja, usijihusishe, this is none of your biz..Do you homo…”



One alifafanua kuwa sababu ya kuandika status hiyo ni kutokana na hatua ya Nikki wa pili kumtumia ujumbe Nikki Mbishi ambao Mbishi alimfowadia ukisema kuwa wao akina One bado ni wadogo kwenye muziki na hawawezi rap, pia album ya Mbishi inasound kama single moja.

Kuhusu namna anavyowachukulia members wa Weusi, One anasema “Ni wazi kuwa siwakubali Weusi, si kama nawakosea heshima bali ni jibu nitakalokupa kama ukiniuliza kama shabiki, mimi si shabiki wao, Ujue nina waheshimu wao kama kundi lenye mafanikio kulingana na kile wanachofanya, hivyo hiyo ni heshima kubwa niliyonayo kwao lakini mimi si shabiki wao” (phatbeattz.blogspot.com).

Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kutomkubali Bonta kama msanii hali inayoashiria kuwa ni ngumu kwa Bonta ama Weusi kwa ujumla kukaa kimya; “Ninaposema Bonta hayupo conscious namaanisha kuwa naheshimu anachofanya, ana ujumbe wa maana lakini uwasilishaji wa ujumbe wake kwa umma ndio tatizo. Kwa neno moja naweza kusema Bonta ni MC mbovu,na ninaposema hivyo namaanisha kuwa hajui kurap, anachofanya nikuongea na wakati mwingine anapata beat nzuri za kuongelea. Nadhani huu ni muda wa kuwaambia ukweli” (phatbeattz.blogspot.com)

Hata hivyo kama mwenzie One, Nikki Mbishi pia ameonesha wazi kung’ata na kupuliza kuhusiana na suala hili “if my mind is a belly then am bellyful I don't think if there is a space to put this cow meat a.k.a BEEF......”

Tayari mashabiki wa pande zote mbili wameanza kujihusisha moja kwa moja kwa kutoa mawazo yao katika kurasa za wasanii hao. “Tunachoshindwa kuelewa wabongo siku zote ni hiki.., Ukweli haui-justified kwa pesa, umaarufu na ujanja ujanja wa maneno. Muziki utabaki kuwa Muziki. Hip Hop itabaki kuwa Hip Hop. Kama "samaki Kwenye Hii Bahari" atazingua.., "tunamvua" tu kwani niaje...!? SUPPORT KWA Nikki Mbishi BabaMalcom NA WOTE WANAOSIMAMA FOR HIP HOP!!!”  


Wengine wameshindwa kuzuia chuki zao na kuandika maneno makali dhidi ya Weusi kuonesha namna wanavyoiunga mkono kambi ya akina Nikki Mbishi. “Watajichubua tu hao weusi. Watoto wazuri wanajiita weusi, hatutaki matozi. One, stereo na Nikki Mbishi wana big screen inayoönyesha u2po wa mabitch weusi. One wagonge ta**o, Nikki mbishi, wachinje huku wanakuchea, stereo watie vitasa watoto wanazingua”.

Vyombo vya habari husasan radio ambavyo siku zote vinaongoza kwa kukuza beef za aina hii vimechukua nafasi zao kwa kufanya mahojiano kupata ufafanuzi juu ya suala lenyewe hali inayolikuza zaidi.

 MLAB ambayo ni nyumbani kwa One, Nikki Mbishi na Stereo imeonesha kutofurahishwa na beef hiyo inayoendelea kukua kwa kasi. Meneja wa wasanii na Studio wa MLAB Patrick Gondwe amemuomba Nikki Mbishi kuachana na beef hiyo.  “ Kama kaka, nakuomba kuachana na suala hili Nikki! Kambi zote mbili ziache kuwagawa mashabiki…..Wapo kwa ajili yetu na hilo ni suala muhimu… Hatutakiwi kutawaliwa na vyombo vya habari.. Siku zote habari mbaya ni habari njema kwao….kutatokea mengi ya kuchanganya  lakini mwisho wa siku sisi tutapoteza mara mbili. Tukubali kukosa (lose) kwa kutokuandika vitu hasi kwenye mitandao ya kijamii na kuziba midomo yetu dhidi vyombo vya habari kuhusu suala hili. Nakuomba sana”

Uamuzi wa kukaa kimya kwa pande zinazohitirafiana unaweza kuwa na faida na hasara. Faida ni kuwa mashabiki wa pande zote mbili watapata fursa ya kuujua ukweli wa jambo lenyewe na kutafakari. Kwao Weusi na akina Nikki Mbishi wanaweza kutumia mahojiano na vyombo vya habari kuzuia kuwagawa mashabiki wao. Hasara ni pale ambapo pande hizi zitajikuta zikitumiwa na radio ama watu wenye lengo la kufanya biashara kupitia mgongo wao. Mfano halisi ni jinsi Darlive ilivyotumia beef ya Roma na Izzo kibiashara.

Kama beef hii ikiendelea kukua madhara yake yataenda mbali zaidi ya hapa ilipo. Beef hii inahusisha wasanii wanaowakilisha mikoa mikubwa yenye ushindani katika muziki wa hiphop, Arusha na Dar es Salaam. Kwa muda mrefu Arusha imekuwa ikitajwa kuwa ngome imara kwa hiphop nchini hivyo beef hii inatoa picha ya wazi ya ushindani kati ya Arusha na Dar es Salaam.

 Hatari ni pale mashabiki wa pande hizi mbili wakigawanyika katika misingi ya kimkoa. Ikiwa hivyo itakuwa ngumu kwa wasanii kama One, Nikki Mbishi na Stereo kwenda Arusha kufanya show wakihofia usalama wao. Historia ya mkoa wa Arusha inatueleza ni kwa kiasi gani watu wa huko walivyo na ushirikiano katika kupinga kitu wasichokipenda. Japo katika hiphop beef zina umuhimu wake, tuombee Mungu beef hii isije kufikia hatua ya watu kupigana wanted katika maskani zao bali kuwapa hasira za kiuandishi wote wanaohusika na mwisho wa siku kuwapa mashabiki muziki mzuri.


Fredrick Bundala aka Skywalker

Tone Radio

www.toneradiotz.com

MPIGIE KURA MTANZANIA MWENZETU ILI ASHINDE SHINDANI LA MODAL24 LINALOFANYIKA NEW YORK, MAREKANI






Mpigie kura Mtanzania mwenzetu ili aweze kushinda shindano la modeling la kutafuta modal24 kwa ajili ya kufanya photo shoot ya bilboard New York, Marekani.

Katika shindano hilo linajumuisha washiriki wapatao elfu moja (1,000) na katika watu hao yeye yupo katika nafasi ya tisa kati ya watu elfu moja.

Jinsi ya kumpigia kura ingia web; www.project.badoo.com, utakuta picha ya Joseph Adriani unachotakiwa kufanya ni kulike hizo picha au link (theproject.badoo.com/gallery).

Huyu ni mwanamitindo wa kwanza wa kiume ambaye anafanya kazi zake nje ya Tanzania naomba tumsaidie ili aweze kufika malengo yake. Joseph Adriani alishawahi kufanya muziki na alishashiriki katika shindano la Bongo Star Search 2008 na alifanikiwa kuingia katika 10 bora.

new track:kaoge by Qchillah


i don't wanna fight (lyrics) by Maurice Kirya

Look at them fighting
Like two roosters in a cage
Hear them preaching
With the words full of rage
They've lost the way
Coz they forgot where it began
They are ruled by so much money
When it's gone
They go down

I was a little boy
with many dreams in my head
I needed no money
Just a guitar in my hand
I wanted to move the world
I wanted to inspire the world
I wanted to be superman yeah
So I'm singing for you today
So I could return to innocence

Bwonoba Kuba Mi Go
Olinga Ekyenyanja (x4)

I don't wanna fight,
I just want to sing

Now look at them fighting
Like two roosters in a cage
Now Hear them preaching
With the words full of rage
See They've lost the way
Coz they forgot where it began
They are ruled by so much money
When it's gone
They go down

I was a little boy
with many dreams in my head
I needed no money
Just a guitar in my hand
I wanted to move the world
I wanted to inspire the world
I wanted to be superman yeah
So I'm singing for you today
So I could return to innocence

Bwonoba Kuba Mi Go
Olinga Ekyenyanja (x4)

I don't wanna fight,
I just want to sing

Music is not what I wear
Music is not the style of my hair
Music is not who I date
Music is not whether my album is early or late
Music is not Fun cigars, Bikinis
Drug, sex, violence and money
Music is a pastor a teacher a mother a healer a mentor a preacher

I was a little boy
with many dreams in my head
I needed no money
Just a guitar in my hand
I wanted to move the world yeah
I wanted to inspire the world
I wanted to be superman yeah
So I'm singing for you today
So I could return to innocence

Bwonoba Kuba Mi Go
Olinga Ekyenyanja (x4)

I don't wanna fight,
I just want to sing


watch video


new video:SISHIKI SIMU by MARYA


new tracks


1*Young Gifted and Black by One The Incredible 2*Kijiti by JCB ft Lavosti 3*mjeshi by chindo 4*unaniumiza by Peter Msechu ft Bella 5*mombasa queen by Hemed

new video SIRI YA PENZI ya SHAA


new video FITINA by LINAH


Tutoke (LYRICS) by Quick Rocka ft Shaa and Q-Chilla

Intro:
M-Chali c'mon bounce to this,bounce to this(Shaa)
We takin over now,Yeiye iyee*2
Chali..(Q-Chilla)

CHORUS:
Imekuwa longtime sana hatuja toka baby
Sa' narudi ndo nataka tule happy,*2
Nakuja tutuke*8

VERSE 1:
Imepita longtime since i left pipi girl,
kabla sijawa famous na kupata hizi dough,
batta la manati b'coz of low budget,
kuwahi kurudi home asubuhi tuwahi classez,
Sasa imechange sio vile sio kama kipindi cha shule,
Sasa batta huku na kule wala usiogope usiwire,
twende tuka party tuwashtue mazee,
tukapige monde mimi nawe baby,
pretty pretty mama nimekumis sana nakuja unitulize roho,
naughty naughty drama hazina time bwana lets party all night long,
full moon party in zanzibar abroad vacations in december,
na vile we' ni mjanja all way tutachanja,
never stay sobber please wasaha ganja,
hold ma hand n follow ma lead coz i'm the one that u've ever needed,
take a ride inna high speed to the limit,
live inna easy way but just rock it,
najua utaipenda sana na hivyo vyote ntafanya kwa ajili yako msichana,
nataka utambue yo' ma best girl ever- na hiyo sexy talk (aaha') yo a diva,

CHORUS:
Imekuwa longtime sana hatuja toka baby
Sa' narudi ndo nataka tule happy,*2
Nakuja tutuke*8

VERSE 2:
Nipo q.u.i.c.k na navigator nakuwaza all the way,
nataka uni-tease kiss n cares me nna three c'z bill zote on me,
itakuwa raha si tukila raha kila day kila saa tuki-shine tu mama,
mos-mos tukipiga steps kwenye dance floor na we' mtoto mrefu,
nata na midundo kulean' back haaaa' back it up girl wee nifanye nifurahi,
We rollin we rollin....
yani vile nakuta wote tuwe high nishakula kitu hakuna kujidai,
Just fallin just fallin...
katakata baby kiuno kamata jinsi unavyo dance hadi watu wamedata,
unavyozungusha me utanipagawisha kiuno chako baby girl kilicholegea mfupa,
unavyopanda na kushuka me unaniacha hoi,
na pale unaponikiss na kusema i love u baby boy,
nikiwa nawe kila muda nai-enjoy,
everytime i'm smilling ni mcheshihuniboi,
nimedata na lips na hizo zako kiss bambataa na zako hips na vile unavyo dress maa,
so tell me kama kwangu unafuraha ndo maana napenda kuwa nawe kila saa,..*2

CHORUS:
Imekuwa longtime sana hatuja toka baby
Sa' narudi ndo nataka tule happy,*2
Nakuja tutuke*8

VERSE 3:(Shaa)
Nasubiri tena sana unitoe ma bby usiniangushe please..
niko tayari nimependeza just how u like it boy ajili yako wewe tu,
kwahiyo fanya haraka njoo quick quick quick rocka,
wajua mimi niko weak weak by yo swagga,
nimepanga kukupa utakacho,
take me out show me off baby boy,
baby boy oooi oooi yeah,

 CHORUS: :(With 'NJOO TUTOKE'-Shaa)
Imekuwa longtime sana hatuja toka baby
Sa' narudi ndo nataka tule happy,*2
Nakuja tutuke*8

Outro:
Quick rocka...Shaa...Quick rocka....Shaa,
yeeeah tutoke ma baby..tutoke ma girl*2,
Njoo-o njoo njooo oooh ooooh oooh!
You alrdy know what it is Marco Chali Holla..

mwenyeji wenu yu sehemu mbaya

kwanza natanguliza samahani kwa wadau wote wa kibabra..maana takribani wiki moja sasa...hakuna jipya humu bloguni..mwenyeji wenu kuna dharura(ajali)..nimepata .na kama mjuavyo waTanzania wanaopenda kuharibu uTanzania waliniibia kila kitu ambacho kinaniwezesha kurusha matangazo humu bloguni...hivyo bado natafuta vyanzo vingine...much love all followers...nmewakumbuka sana wadau wangu..get to yu soon

R.I.P E-Sir



Issah Mmari


Born Issah Mmari, on May 20, 1981 in California Estate, and raised in South c estate Nairobi, Kenya, E-Sir was a Kenyan hip hop artist signed to the Ogopa DJs label who was famous for his deft lyrical ability and command of the Swahili language. He is still widely regarded as one the best rappers to emerge on the Kenyan hip hop scene. He first came to be known in 2001 by his song "Jo", a song done in the same style as Black Rob's "Whoa." The song proudly declared E-Sir's arrival on the Kenyan music scene and was featured on the Ogopa DJs debut album . He went on to release his debut album "Nimefika" in 2003 which was a big hit with virtually all the songs on the album becoming radio singles. He won 4 categories in the 2003 Kisima Music Awards.
E-Sir died in a road accident on March 16, 2003, while in the company of fellow label mate Nameless. He was on his way back from a concert in Nakuru town that was to help promote the album. His fans were shocked and grieved for days on end after hearing the news of his death. His death was considered coming at a time when his career was starting to take off. His other hits include "Mos Mos," "Boomba Train," "Hamunitishi" and "Leo ni Leo." His only posthumous song was the collaboration between him and Nameless called "Maisha".
E-sir's younger brother Habib is also an upcoming rapper in the Kenyan music industry. He has couple of singles to his name, some of them with his partner Manga
     

    

chek ya show ya mkasi ya MwanaFa



ngeli ya genge lyrics by Juacali

Verse 1
Naandika hii verse ka niko na njaa
Naenda kupika bila makaa
Nawaita na mnakataa
Mnasema kanisa haina mavijana
Kushiba ni baada ya sala
Kuiva nao siku hizi ni balaa
Utageuzwa kima na makusaga
Pika ive tunamanga
Sukuma chumvi na ka uganga
Chuma ngumi teke kadhaa
Boxer chupi na mahandra
Toka nyuki asali chang’aa
Koma kumi utashangaa
Ama stima zitazima
Twende kwa kina Faridah
Jiekee hina kwa mafinger

Chorus
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge

Verse 2
Nataka ukae poa ka kina
Fatiya Halima na Eva
Watoto wazuri
Ndoto nzuri huisha
Ka ume---- zote kabisa
Ukasanya moto ukapatia
Bahati mbaya ukashikwa
Mabati waya ukapigwa
Mashati za Wanja zikaishia
Chukua zingine uanze kupima
Vua pengine ni ya Peter
Beste yangu mtu wa shida
Hii miti ni yangu wee tuliza
Unadoea kiusfisi na hanjaalikwa
Unapokea dishi na hiajapikwa
Chakula na mbichi na haijaiva
Tuma sista Eastleigh manjiva
Lakini chunga vile atajivaa

Chorus
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge

Verse 3
Ma-mini puma na adida
Ma-G-string shuka na ma-
Mambuyu kwao ni kushangaa
Pudu zao zinaamka
Njugu kibao anatafuna
Mamatha huku wanashtuka
Hanya huyu utajuta
Kama sumu inaua
Maziwa iko tutakunywa
Kama njumu zinatupa
Kabisa tutakataa kuvua
Matope kila mahali panguza
Polepole ngazi tunashuka
Pole eka kazi ya sungua
Mwisho ganji itaingia
Vitisho wangapi watasikia (Genge damu, California)

Chorus
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge
Hapa
Tunacheza na maneno
Ngeli ya genge

Quick Racka ku''hit the floor'' hivi karibuni



MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Quick Racka, amesema kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘On the floor’, ambayo itakuwa maalumu kwa kwa ajili ya mashabiki wake wa klabu.


Msanii huyo alisema kuwa wimbo huo utaenda sambamba na video ambapo baada ya kukamalisha video ya ngoma yake ya ‘Fire Atherm’ kazi ndiyo itakuwa inafuata.


Alisema ameamua kutoa ngoma hiyo kwa ajili ya mashabiki wake kwani ni wimbo ambao utakuwa unachezeka hata sehemu zote hasa kwenye kumbi za starehe kama vile klabu.


Hata hivyo aliongeza kuwa kikubwa anachotaka kufanya ni kutoa ngoma mbili ambazo ni hizo ‘On the Floor’ na ‘Fire Atherm’, ikiwa sambamba na video zake.


“Maandalizi yapo na ngoma hiyo mpya tayari inakamilika lakini kikubwa nachotaka kufanya ni kutoa zote kwa mpingo pamoja na video ili tu mashabiki wangu waweze kuona nini kinachoendelea katika muziki wangu,’ alisema.

Na Laurent Samatta wa Dartalk.com

chek na lyrics ya wimbo wake wa

DIAMOND KUIMBA TAARABU






MSANII anayewika kwa sasa wa muziki wa kizazi kipya bongo, Diamond, amesema kuwa anafikiria kuimba nyimbo za taarabu baada ya kukosa mpinzani kwenye bongo fleva.

Aidha alisema kuwa katika muziki wake hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango alichokuwa nacho kwani katika kuthibitisha hilo ndani ya nyimbo zake hakuna msanii yeyote aliyemshirikisha.

Aliongeza kuwa kikubwa kinachomsukuma kufanya kila aina ya muziki ni kutokana na kipaji alichokuwa nacho kwani hakuna kitu anachoweza kushindwa kutokana na uwezo aliyokuwa nao.

Msanii huyo aliongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyokuwa kwa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.

“Naweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu nina kipaji cha kuimba nyimbo aina zote hivyo endapo nikifikia muafaka naweza kufanya kitu hicho ingawa mashabiki wangu watastuka sana,” alisema.

Hata hivyo alipoulizwa kama anatshirikiana na wasanii wakongwe wa nyimbo hizo za mipasho, alisema kuwa kwanza atasimama mwenyewe lakini baada muda ataweza kuwashikisha vichwa kama Isha Mashauzi, Mzee Yusuph na wengi kibao.

Na Laurent Samatta wa Dartalk.com




new track:UNKNOWN - SORRY (Produced By PANCHO, Mixed & Mastered by HERMY B) by Bhitz Music.


ComScore

NEW TRACK: Beka - SIDILI NA WEWE

 
Msanii Beka ambaye zamani alikuwa kwenye kundi la THT ila kwa sasa hayupo tena ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la SIDILI NA WEWE. Huu ukiwa ujio wake mpya kwa mwaka huu 2012, anaomba mashabiki wake wampokee vizuri kwani kwa sasa kazi ndio kwanza inaanza na anasubiri maoni yenu kuhusu wimbo huu mpya.

mpita njia by Alicios Theluji ft Juliana Kanyomozi

NEW TRACK: Jose Mtambo ft Belle 9 - NAONGEA NA ROHO


Oiii Peeps!!!!!
Tongwe  Records now comes up with Jos Mtambo ''The Legend of Kigambonino''  featuring Belle 9 in the track NAONGEA NA ROHO
Jos Mtambo talks to the souls of the brothers and sisters we lost.These were very influential people  in East Africa such that would they be alive today
much would be accomplished.Jos pays tribute to these people and remembers their effort in making E.A the place to be.We salute them all and respect their contribution.

PEACE
J-MURDER
CEO
TONGWE RECORDS

CREDITS
 SONG: NAONGEA NA ROHO
 ARTIST: JOSE MTAMBO FT BELLE 9
 PRODUCER: J-RYDER
 STUDIO: TONGWE RECORDS

chek ujio mpya wa mr Nice katika video ya tabia mbaya

Khalid chokoraa afafanua tuhuma za uchawi zinazomkabili


Mkali wa muziki wa Dance Tanzania Khaleed Chokoraa wa bend ya Mapacha watatu ameamplfy kuhusu tuhuma za yeye kutumia uchawi kazini.
Amesema “watu wanaogopa tu lakini sio kweli, hivyo vitu havipo Mapacha watatu japo katika mila na desturi za kiafrika ni vitu vya kawaida kwa hiyo sio mbaya sana vilevile”
Khaleed alitoa kauli nyingine tata kwa kusema “hata Mungu mwenyewe anakwambia kwamba jisaidie na yeye akusaidie hivyo ni kuomba Mungu, kila mtu anaomba Mungu kupitia imani yake”

source:http://www.miilardayo.com/

mwanamuziki Lady Jaydee aelezea sababu za kutoonekana kwenye show nje ya band yake kwa muda mrefu sasa


Mwimbaji Star wa bongo LADY JAY DEE amezitaja sababu chache zinazomfanya asionekane kwenye majukwaa mengi ya kibongo akiperform.
Exclusive na millardayo.com Jide amesema”wakati mwingine mapatano inatokea muandaaji wa show anashindwa kulipa ninachotaka, au mwingine anashindwa kuniweka kwenye show yake kwa sababu anaona sijafit kuwepo”

moja ya usafiri anaomiliki Lady Jaydee kwa ajili ya band yake
Kwa kumalizia, Jide amesema bei anayochaji kwa show moja ni moja ya sababu zinazofanya wengi washindwe kumudu kumuona kwenye stage za show mbalimbali za kibongo, kwa sababu anataka MILIONI 10 za kitanzania kwa kila show moja ndio maana mara nyingi amekua akionekana akiperfom na bendi yake ya Machozi katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge tu

source:http://www.millardayo.com/
click hizo link kupata lyrics zake
mimi ni mimi by lady jaydee ft Oliver Mtukudzi
wangu by lady Jaydee ft mr Blu 

Action lyrics by Cpwaa ft Ms Triniti,ngwair, Dully Sykes

Cpwaa na Ms Trinity
 
dully sykes


Mangwair
INTRO
A, A,Action tonight
A,A,Action tonight
Brainstormusic baby, show time,show time,show time,
A,A,Action tonight,
A,A,Action tonight,
Pwaa is in the building!

Verse 1 : Cpwaa
Whats up, whats up, Pwaa is in the building, get up get up!
Whats going on yo! Yeah we on yo,
Hit me on my BBM we uptown yo! Ok!
Tired of the daily scenes, tired of the drama queens,
Let’s get dirty if you know what I mean, Lets hit the party,
I wanna rock this body, wanna smack somebody!
Take it to the left, take it to the right
Give it to me, give it to me baby all night,
Drop it down, take it to the top, back it up back it up, baby don’t stop,
Once it pops, that’s a wrap.
We don’t run this town; we make it spin 360,
We so fresh and so crispy, yeah she is looking at me she miss me
Ooh no she wanna kiss me, she tipsy,
Camera down, lights off then…..action

Chorus:
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah Pwaa is in the building
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action”
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah

Verse 2: Ms Triniti
Gimme like, gimme like, Gimme like,
Gimme like, gimme like, Gimme like  ACTION TONIGHT!
Gimme like, gimme like, Gimme like,
Gimme like, gimme like, Gimme like ACTION TONIGHT!

I need your action, skin to skin connection,
Put your arms around my body, ready for your flexion,
My Yute you a star
You a light it up from a far,
Easy na easy na Rasta,
Uno know you raise di bar,luv uno like cooked food pasta
And Yah,when you are ready,Rated R,
Da Re mi fa so la, you a take it from the la,
Uno fly high like Kilimanjaro,
Keep on lovin me na star,
Mi wha fi thank your ma and your pa,
Chap chap lova lova, chap chap lova lova!

CHORUS 2
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah Pwaa is in the building
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action”
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah

Verse 3: Dully Sykes
Me I burn dem,
paparazzi wananisaka kama lulu
kwenye paper 400 waniuze,
Me I burn dem,
Kina dada wananipenda nashukuru
mpaka mama anawaomba wapunguze,
Me I burn dem,
paparazzi wananisaka kama lulu
kwenye paper 400 waniuze,
Me I burn dem,
Kina dada wananipenda
nashukuru mpaka mama anawaomba wapunguze,
Swaga za dada zangu watu wanaleta fitina,
ngoma utaminya wewe sisi itapigwa na titina,
Swaga za dada zangu watu wanaleta fitina,
ngoma utaminya wewe sisi itapigwa na titina,
Hey hey Rey Rey give me some action,
Beat ya Marco na Mj bonge ya production,
Hey hey Rey Rey give me some action,
Beat ya Marco na Mj bonge ya production,
Hey hey Rey Rey give me some action,
Beat ya Marco na Mj bonge ya production,


CHORUS 3
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah Pwaa is in the building
Give me some “Action”
Show me some “Action”
I need to see some “Action”
Ooh na na na naaa Action yeaaaaahhhh,
oaaahhh oaaaah

Bridge Ms Triniti
Wind low, wind low,wind ooh ooh oooh oh,
Wind slow, wind slow,wind ooh ooh oooh oh,
Wind low, wind low,wind ooh ooh oooh oh,
ooh ooh oooh oh, ooh ooh oooh oh,
Action…..oooooh ooooooooh
Action…..ooooooh oooooooooh
Action…..oooooooh oooooooooh
Action…..ooooooooh oooooooooh



Bridge: Mangwea
Pour me my liquor, lit me more fire Mr DJ keep on spinning
set the roof on fire!
Pour me my liquor, lit me more fire Mr DJ keep on spinning
set the roof on fire!

Gimme likkle, gimme likkle, Gimme likkle,
gimme likkle, Gimme likkle, gimme likkle ACTION TONIGHT!
Gimme likkle, gimme likkle, Gimme likkle,
gimme likkle, Gimme likkle, gimme likkle ACTION TONIGHT!

Outro: Ngwear
Give some, ACTION
Show me, ACTION
Give some, ACTION
Cause I need some, ACTION YEAAAAH
Yeah ha ha haaa holaaaaa!

watch video

bado nipo nipo lyrics by MwanaFa

Wagwan Blood…
the personality change,…hii ya leo hii!
Hermy…


MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?

Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa
Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua
Mi nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia
ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa
napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu
kwani na mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu
watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao
wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao
sioi leo,sioi kesho-kutwa wala mtondogoo
sioi mchana,sioi jioni,usiku wala majogoo
morale nliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa
ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa
eti nizibe maskio
wengine nifumbe macho
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?

hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/
watu wana watu wao wengine toka zamani/
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako/
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/
sijui ni dhiki au tamaa tu??/
watoto wanaanika njaa tu/
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu/
msinipe headache/staki kufuata Mkumbo/
nyi anzeni mi niacheni,staki kufanya gamble/
marafiki wanauzana/ndio zao vicheche/
na daima wanateteana/usiwaamini usiniangushe/
anataka kuolewa na anamegwa kama kawa/
demu wako akiuza wenzake,zinduka nae analiwa/yes’
staki kuoa sababu staki kulia/
najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia/
nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi/
ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi/
alilala na bibi arusi/siku moja kabla ya arusi/
na wala sio bwana arusi/bado mnanishauri arusi?/
eti nizibe maskio/
wengine nifumbe macho/
nisione wakati naibiwa??/
hamuwezi kuwa hamjalewa/

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?


usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania/
watu na akili zao washajichuuza na wakalia/
sikatazi watu kuoa/
na hata nikiwakataza neno langu sio sheria/
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri/
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari/
inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri/
ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari/
wanatoroka na wazungu/wanamegwa na vibabu/
wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu/
ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe/
au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe/
wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee/
haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume/
kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria??/
sio kila demu umuonae unaweza muoa/
eti nizibe maskio/
wengine nifumbe macho/
nisione wakati naibiwa??/
hamuwezi kuwa hamjalewa/
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi/
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini/

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?
Outro
Yes yes…it’s yo boy FA
na Hermy B..ni kazi chafu but lazima mtu aifanye/
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri/
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari/
yeeeeah,love is love my people/
ladies,behave basi/…au sio??