bado kidogo lyrics-Banana Zoro

asubuhi kila siku naamka riziki nakwenda kutafuta
Naamini kuna siku ntapata
Sijachoka kutafuta nashukuru mpenz wangu una subira maana kupata ni za
mungu kudra
Mitihan mingi tumepitia lakin yote ulivumilia wewe wewe weee
Tuliwahi kufukuzwa na nyumba mmh tatizo kodi
Nikanyang'anywa na la urithi shamba kisa wanataka kupima viwanja
Wewe hukuondoka wala hukuogopa
wewe ni wa kipekee wewe wa pekee sijaona
kama wewe

Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado
Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado

Majira hubadilika mara mvua,jua katikati ya masika,mapenz yetu
hayajabadilka licha ya radi za mikasa kutupiga matatizo yalivuma shida
nazo zina mwisho wake usimsahau muumba hizi zote ni kudra zake,matatzo
yaliumbwa shida nazo zina mwisho wake
Mitihani mingi tumepitia lakini yote tumevumilia
wewe wewe weweee ni wa kipekee

Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado
Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado

Ndo maana kila siku me bado napambana naamini kuna siku tutapta
sana..sababu najua kila mtu ana siku yake

Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado
Bado kidogo subiri kidogo ngoja kidogo muda baado

No comments:

Post a Comment