nakata kiu by I'c ft Shesheman Sam
Intro
(Shesheman Sam)
So brother do you think they need to here this?
(I’c)
Yah they gotta hear this…
(Shesheman Sam)
Are you sure about this?
(I’c)
Yah I’m…
(Shesheman Sam)
Are you certain about this?
(I’c)
Positive…
(Shesheman Sam)
Ayt…

Verse 1 (I’c)
Maisha yana bana, labda kama chatu…
Vunja mbavu ya kwanza, ya pili nay a tatu…
Hawana huruma waone tu hawa watu…
Tulio wachagua tukijua hawawezi wakawa viatu…
Kila day, Mangi anapandisha bei…
Siwezi mlaumu nafahamu hali inatisha aise!
Maji yanakatika mwezi, hii hali ziiwezi
Mwalimu alipinga dhuruma, mnachekea wezi…
Foleni imesimama, je unasikia wimbo wa taifa…
Siupati hata kwa wifi ni miundo mbinu haifai…
Watu wanaangamia, yako wapi  maarifa…
Niyafwate, I’m gon’ roll up, Wiz Khalifa…
Umeme wa mgao kipande chetu kidogo…
Na nikama hawakioni hawa wetu vigogo…
Walituahidi vingi leo wanatupa visogo…
 

Chorus (I’c)
 Ni mchakamchaka tumekosa likizo…
Kila day tunazisaka na ni kama igizo…
Hivyo niite Martin Luther sina time niko…
Kwenye harakati ka’ Abraham Lincoln…
Oooh Nakata kiu… X 8

Bridge (I’c)
Nili kaza mkanda nikiingoja kasi mpya…
Nabana tumbo bure bora niji nafasi upya…
Twaenda mdogomdogo pengine twarudi nyuma…
 Kila leo bora ya jana na sio kwamba juhudi hatuna…
Oooh Nakata kiu… X 8

Verse 2 (I’c)
Ukimwacha Malkia pekeyake kwenye kichugu…
Hakioti tena umelizwa kama unamenya vitungu…
Hatuwezi endelea hata tuongozwe na Obama…
Bila uzalendo zaidi ya Maalkaida wa Osama…
Mnawaza uShaloMilionea, Oh mama (RIP)
Ila inabidi kujituma saka Dough bana…
Plus tusali sana, Haleluya, Hossana…
Ajira hakuna, jiajiri mwenyewe…
Waliisha toa mikopo sa mnangoja nini mpewe…
Wamewalisha nakuwatafunia sasa mmezewe…
Hamjatulia (woof woof) achampepewe…
Fungueni macho ama nyuma tutarudi jamani…
Au kuzunguka humu ka Wayaudi jangwani…
Njoo tuzisake, toka kwenye maficho yako…
Kwani asie na kitu atanyang’anywa hata alichonacho…
 
Chorus (I’c)
Ni mchakamchaka tumekosa likizo…
Kila day tunazisaka na ni kama igizo…
Hivyo niite Martin Luther sina time niko…
Kwenye harakati ka’ Abraham Lincoln…
Oooh Nakata kiu… X 8

Bridge (I’c)
Kenye Kampeni wanasiasa wanatunga uongo…
Na nyie mwanishangaza mnapowaunga mkono…
Mnauza kura nawakipita mnapunga mkono…
Ati usicheze mbali, unga robo…
Oooh Nakata kiu X 8

huyu demu by Steve RnB ft Blue(Verse1: Steve RnB)
Niko ndani ya club
nikoo na huyu demu anadatisha
Masela wanauliza nani anaitwa
Niko zangu VIP nimekausha
Jina Hanifa alivyo mzuri anadatisha
Masela wanauliza nani anaitwa
Lakini mimi nimekausha

(Chorus: Steve RnB)
Kuanzia juu mpaka chini
Huyu demu anasiri (aah)
Hiyo siri naijua mimi
Ni wengi kawapiga chini
Ila sijui kwanini (aah)
Ila yeye kanipenda mimi (I told ya)
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimfuate
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimguse
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae

(Verse2: Steve RnB)
Wanashoboka masharobaro wanajipitisha
Wanajiuliza nn nampa
Mtoto mzuri nmemdatisha
Mimi nmekausha sina noma
Na mtoto hanifa si tunajirusha
Anavyokatika
huyu mtoto ananidatisha

(Chorus: Steve RnB)
Kuanzia juu mpaka chini
Huyu demu anasiri (aah)
Hiyo siri naijua mimi
Ni wengi kawapiga chini
Ila sijui kwanini (aah)
Ila ye kanipenda mimi
(I told ya
Let's go now)
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimfuate
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimguse
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae

(Verse3: Blue)
Miaka kama nane
Baby honey niko nae
Kila day inakua mpya
Napenda kuonana nae
Ukisikia harusi jua naoana nae
Sio kicheche sio mapepe
Wacha watoto wazae
Chomoka out komesha masista duu
Ebu dharau we mwenyewe matawi ya juu
Ukiwa na mimi mr blue
Kila kitu juu
Hii nyimbo kwako boo
Sogea karibu
Wanasema tupendane wengine washaachana
Wakati tuko nyumbani tabia zinafanana
Kaa mbali nae
Ukiona amekatiza kwa kitaa
Usiende mbali usije ukavamiwa na vichaa
Kwanza atakataa
Pili demu wa superstar
Mpaka home tabata wanajua Hananifaa
Subiri aje akifika naondoka nae
Pigeni muziki waziwazi nicheze nae
Aachani nami siachani nae
Anapendana nami napenda nae

(Chorus: Steve RnB)
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimfuate
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Niko nae huyu demu
Popote alipo usimguse
Niko nae huyu demu
Nakupa tahadhari
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae
Shubiru shubiru
shubiru shubiru
Kaa mbali nae

Shubiru
Kaa mbali nae ....till fade
........................
............................

Mrs superstar by Young Killer ft Nemo & Bright
(Verse1:Young Killer)
Kila mwanadamu anaupendo kwa yule ampendaye
Mwingine anawaza vipi atampata yule amtakaye
Sio kwamba nact no nipo real
Japo msodoki ni mdogo ila nauwezo wa kufeel
Fikra zangu zinatuma
Nidate kwa maunda zorro
Najua nitaleta jealous kwa brother banana zoro
Sasa vipi nikiwa penny hivi ntakuwa free
Au kama nngekuwa na mwasiti wa THT
Ila penny nahisi diamond atanisumbua
Hata mwasiti pendo langu atalivua
Kwanza long time ago
Nilishazmikaga na wema
Na scandal za magazeti moyo wangu ukamtema
Nikawachukia mapaparazi nikahisi wameharibu bahati
Moyo wangu nikauweka bond kwa chiku mwanaharakati
Ila wote tunachana hatutadumu maghetoni
Nilipozimika na besta marlaw akapiga honi
Madam ritha na salama wakaogopa mcharuko wa bss
Nmemov mpaka da wolper nimchane face to face
Ila roho inakataa inaogopa waigizaji
Macho yalishatua kwa flora hbaba akamhitaji

(Chorus:Ne-mo&Bright)
Wapo wengi natamani kuwa
Nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs superstar nani nimwite love
Mrs superstar nani nimwite love

(Verse:Young Killer)
Hizi hisia zangu sidhani kama nakufulu
Sidhani kama nakufuru
Akili inanituma niende sambamba na lulu
Ila naogopa yasinitokee ya kanumba
Nikasukumwa nikafa wengine wakang'oa mchumba
Ama Ray c nikimchek machoni haishi
Kile kiuno bila mfupa kingenipikia mapishi
Ila ghafla nikaogopa niliposikia ana mchizi
Baada ya kuuliza ni nani kumbe mnako lod easy
Navyokupa utanipa upendo wa kina
Au tutaachana njia panda kama amini lina
Kwa love sitaki kukosea niwe na mrembo mwenye visa
Niwe na thea au nimwache nidate kwa Monalisa
Nikadata na diva
Ila sauti ni soo ye ni mgonjwa
Kwa raha zangu atanifia itakua soo
Sura pesa aunt ezekiel young sina hela
Vanesa mdee najua huwezi ishi kisela
Mara Jokate kichwani  akanitawala mpaka basi
nkajua hata nikisema basi hatanipa nafasi
Namuomba mungu anipe gift special
Kama isingekua kizunguzungu basi
Ningekua na recho

(Chorus:Ne-mo&Bright)
Wapo wengi natamani kuwa
Nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs superstar nani nimwite love
Mrs superstar nani nimwite love

(Verse3:Young Killer)
Usiku silali usingizi autokei
Namuwaza Johari
Ila ule ukaribu na Ray
Unanipa wasiwasi na mimi sitaki nijute
Basi nikaamia kwa Dayna baada ya kusema nimvute
Shilole naogopa kumwambia yanayonisibu
Kwa khadija nikakope kopa nije kumpa taratibu
Nahisi atanihadhibu pedeshee wa yafitina
Maana atahitaji matunzo cha ajabu mimi uwezo sina
Nampenda Uwoya mtoto wake ataniitaje
Kaka au baba ndikumana atanionaje
Hizi hisia zangu wala siitaji maswal
Me napenda kuitwa babu Bi.Cheka atakubali

(Chorus:Ne-mo&Bright)
Wapo wengi natamani kuwa
Nao in my life
Muda mwingi natumia kuwaza nani atanifaa
Mrs superstar nani nimwite love
Mrs superstar nani nimwite love

sema nao by Ney wa mitego(Verse1)
Me ndio raisi wa manzese yule tozi kasanda
Manzese mikono juu naiongoza kamanda
Wanangu nyongeni ganja msiogope polisi
Ila tu msile unga mtapoteza nafasi
Me ndio gangster rapper na kiboko ya marapper
Wanaleta ushindani mwishoni wanatoka kapa
Me natengeneza hela wao wananuka vikwapa
Eyo mchovu wape salam kubum kubam
Waambie watakufa nao mziki umebadilika
Napenda mnavyonidisi wala hamnitishi
Walap diamond we si mtoto wa kigoma
Mpe salam zitto kabwe mwambie afanye siasa
Aachane na bongofleva huku atumtaki kabisa
Maneno mengi propaganda hajui kutekeleza
Kigoma allstars tayari kawatelekeza
Naongea na ridhiwan eyi ridhiwan
We si mtoto wa rais ridhiwan
Mwambie dingi yako masela hawamuelewi
Wamakonde wa mtwara hawataki tena korosho
Wanataka gas si mtawauwa kwa mkong'oto
Nani rafiki wa Lowasa peleka salam
2015 nataka agombee uraisi
Nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi

(Chorus)
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao

(Verse2)
Sina beef na polisi Mbunge wala raisi
Hizi ni salam tu nataka tuishi peace
Mkimaindi amna noma
Sio muelewa kula kona
Hizi salam toka bongo nataka zifike kenya
Uganda hakuna matata najua ngoma inapenya
Mambo vipi ccm mnasemaje chadema
Cuf bado ngangari au tayari mshabuma
Na salamu muhimu ziende kwa watu maalum
Nani nimtume kuzimu afikishe salamu
Kwa kanumba na ngwair
Siku ya misiba yao kuna watu wamepigaa hela
Wanamiliki magari wameota na vitambi
Kwa hela za rambirambi
Kwa majina nawajua mkizingua nawataja
Msisitizie Na kanumba Baada ya yeye kufa
Na bongo movie imekufa haiuzi kabisa
Hizi salamu ziende kwa madam ritha na bongo star search
Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi
Namuona walter chilambo kapigika kama zamani
Haji ramadhani kachoka yupo kitaani
Milion hamsini zao anazila nani
Hacheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani
Tanzania bila uchafu kumbe inawezekana
Yoo Jakaya mualike tena Obama
Japo ujio wake kwa wengine ni lawama
Walalahoi wenzangu mishe zao zinakwama
Nani nimtume dodoma afikishe salamu bungeni
Kuna wabunge vilaza bungeni wao wanalala tu
Na wakiamka kila hoja ndio tu
Kuna vilaza part two wao matusi na kulumbana tu
Mawaziri vivuli wanakazi gani wana  maana gani  wana faida gani
Wabunge viti maalumu wana kazi gani wana faida gani  Mbona me sielewi

(Chorus)
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao
We nenda wape salamu zao
Waambie sina tatizo nao
Wakivimba wapasuke
Hizi salamu zifike kwao

KAMA HUWEZI - BY RAMA DEE Feat LADY JAYDEE


(Verse 1: JayDee)
Vipi mpenzi huoni mbali
Kweli huwezi kwenda mbali, na mie
Kweli mengi huletwa ndani
Si halali kuyapokea yote unitupie
Tutagombana kila siku mpenzi
Tutaudhiana kila siku ndani
Tutatishana kugawana mali
Bila kumjua mchawi wetu nani

(Chorus):
Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma

Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma

 
(Verse 2: Rama Dee)
Hizi lawama ziishie leo leo
Isifikie wakwe wanivue vyeo
Kwa gubu lako tu, mamii
Lawama zako zisinitie uchizi
Nibadili mipango yetu mingi
Hatutagombana tukifata yetu
Hatutaudhiana tukipanga yetu
Hatutafikia kugawana mali, mimi na wee

(Chorus):
Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma

Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma(verse)
Tutagombana kila siku mpenzi
Tutaudhiana kila siku ndani
Tutatishana kugawana mali
Bila kumjua mchawi wetu nani
Hatutagombana tukifata yetu
Hatutaudhiana tukipanga yetu
Hatutafikia kugawana mali
Mimi na we
 
(Chorus):
Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma

Kama huwezi
Kuwa mkweli
Kamwe mpenzi mbele hatutofika mama
Kama pesa, zipo za kututosha ma


Song written by Rama Dee

Mwambie Mwenzio by Stamina ft Darasa and Warda
[Intro - Stamina]
You know what Tidi..
This is One Love Effects man
Shodobwenzo on this one
Its Moro Town baby!!

[Verse 1 - Stamina]
Uh!
Wakuja rudi bush, mji unahitaji waliosoma
Kicheche usikae uchi huku umevaa sketi ya ngoma
Safisha kope braza Mungu sio Deus
We ushangai mzungu mweupe ila anakivuli cheusi..uhh!
Kuitwa lijali anamaana nyumbani tule
Ukimwi kuutibu aghali sa iweje upate kwa bure!?
Binti usitoe mimba ukihisi utakosa soko
Zaa umtunze kinda mbinguni usichomwe moto...what!
Acha kuiba we fisadi uliyetukuka
Mshtue na Ngaliba nae aache watu wanakufa
Dogo unaekunywa gongo ukifa utazikwa la mboto
Na denti skuli ndo mchongo ya mjomba mwachie Mpoto
Teja pandisha mlege rudisha kete kwa pusha
Mwambie atanyea debe akikamatwa na vya Arusha
Acha makuzi mpendaji ili ufike mbali
Mapenzi king'amuzi na pesa ndo dijitali

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Verse 2 - Stamina]
Ewe mtegemea ndugu mwenye mikono na miguu
Maskini tatizo sugu kuliko hata Mr. II...eeh!
Baba la baba weka ubaba kila levo
Kitaani usawa unakaba hadi padri anaishi devo
Mabadiliko daima huanza na wewe
Kama unakokwenda siko uliza ili usichelewe
Mche Mungu kama hajapanga hajapanga
Kama riziki mafungu kwanini ushinde kwa mganga!?
Kusoma mpaka uchizi ni kukosa kujiamini
Mvivu unaependa usingizi utakufa ukiwa maskini
Endapo utailaza akili usitegemee shida kukuamsha
Hakuna mpenzi kama dili funga nae pingu za maisha
Hakuna tofauti kati ya tajiri na maskini
Uvae bukta uvae suti ila wote tutazikwa chini
Usimtenge mkiwa kisa wazazi wake walimtupa
Hata ng'ombe ana mziwa ila akila sumu anakufa

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Verse 3 - Stamina]
Uuh!
Huna hata cheti cha form 4, na una ndoto za kuwa raisi
Nyumbani unajaza choo, hupaswi kungoja na urithi
Kufeli hasara akili hailetwi na milo
Sio kisa dunia duara ndo denti upate ziro
Kila kitu kizuri duniani huletwa na pesa
Braza elimu haina umri usiogope kusoma memkwa
Ujanja hauna miaka kiujinga we baki mdogo
Acha uchu wa madaraka kwa kuongoza hadi vigogo
Hivi vifo vya wasanii vinatokea ka ajali
Ehh Mungu mshushe Nabii atukumbushe kusali
Tumia akili maishani uongoze jahazi
Na usitafute utajiri kwa kumtoa kafara mzazi
Hujachelewa bado cha msingi we piga kago
Shukuru bado unahema wala usishe vilago
Kijana taifa la leo usilale we ijenge kesho
Ukoloni mambo leo usikufanye ujione special...What!!

[Chorus - Darasa]
Vipi umekaa chini na muda unakwenda mbio?
Kwenye nchi masikini na wengi wa matukio
Wambie jamaa huu ni mwendelezo sio ujio
Koo ina kitu cha kusema nipe muda na sikio
Ukiwa mtaani hizi ripoti mwambie mwenzio
Ka umechill maskani jirani mwambie mwenzio
Mfanyakazi au mkulima shambani mwambie mwenzio
Mwanafunzi na mitaa ujumbe mwambie mwenzio

[Outro - Warda & Darasa]
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!

Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!
Mwambie mwenzio...mwambie mwenzio!