I am Supplying by Langa

(intro)
Lyrically and naturally gifted
Rais wa kitaa don’t get it twisted

(verse 1)
Rushwa umaskini vita vya kidini
Lini Africa tutapata tiba ya ukimwi
Watoto wa maskani maua yanayokua sakafuni
Yanayochanua kwa tabu, jua na maisha duni
Wezi wa punje za wali wanapigwa matofali
Majangili walio vitini wanalimbikiza mali
Wengi wamekufa milangoni mwa hospitali
Haupati huduma bila hongo ya daktari
Viongozi wa kesho watakuwa na ujuzi gani
Kama waalimu wanauzia wanafunzi mitihani
Nenda mikoani sio kwa wagogo sio Arusha
Usishangae kukuta watoto wadogo tu mapusha
Wengi wanapewa vyeo,japo hawana upeo
maTrafik wameshageuza madereva vitoweo
Nendeleza harakati kwa kupitia sanaa
Nilianza kuvaa khaki kabla ya Dr.Slaa

(chorus)
I am not buying, I am supplying
I make music I don’t do crimes
I am not buying I am supplying
Streets want me music me fans dem are crying

(verse 2)
Je sheria zimewekwa ili zitusaidie
Au labda zimewekwa ili masikini waumie
Usiamini kila kitu unachoona kwenye video
Kazi zinatolewa kwa undugu na upendeleo
Ukiwa hapa Bongo hupati michongo
Ukikimbilia ulaya unaishia kuosha vyombo
Matumizi ya mali ya umma kwa faida binafsi
Kinyume cha maendeleo na adui wa haki
Sio swala la njaa, ni swala la ulafi
Misaada yote inayotolewa inaishia wapi
Kama kuna mwisho wa dunia basi hizi ndo ishara
Binadamu mpaka dini kageuza biashara
Mimi naamini mungu sisemi uwongo
Ukweli ni mchungu kama ladha ya Gongo
Nakueleza mambo usiyofundishwa darasani
Yaani kama kuhani au nabii wa mitaani

(chorus)
I am not buying, I am supplying
I make music I don’t do crimes
I am not buying I am supplying
Streets want me music me fans dem are crying

(verse 3)
Wananichekea usoni kisogoni wananisema
Wanatafuta mabaya wanajifanya hawaoni mema
Mungu pekee ndo mwenye mamlaka ya kunijaji
Sio mshkaji mwenye taji anayejifanya mjuaji
Haki iko wapi? Unaweza kusingiziwa hadi mauaji
Rushwa kama jadi kwa mawakili hadi majaji
Mapolisi ni wauaji wenye kibali cha kikazi
Ndo maana,nawaogopa kushinda hata majambazi
Tunatapa kama wafa maji japo tunaishi nchi kavu
Viongozi wanatumia vyeo vyao kutoa shavu
Mi ni sauti ya jamii,ninachokiongea kipo
Naeleza malalamiko ya watu kupitia hiphop
Power to the people kama vile Steve Biko
Sio propaganda za wanasiasa kwa ajili ya mshiko
Mimi ni zaidi ya msanii niite mwanaharakati
Sitaki mashabiki mimi nataka wafuasi

(chorus)
I am not buying, I am supplying
I make music I don’t do crimes
I am not buying I am supplying
Streets want me music me fans dem are crying

(outro)
I’m not buying I’m supplying
I tell the truth u know I’m not lying
The harder the battle,the sweeter the victory
Ukishindwa kupanga, umepanga kushindwa

Moyo mashine by Ben Pol

[Verse 1]
Najua kukikucha ntajuta kama nikikuta unanitania
Maana moyo wangu nimekupa uweke
Mimi ni mfungwa tena ni mjinga
Nimejileta gerezani
Tena sikuwaza ntakuwa mateka
Mmh

[Pre-Chorus]
Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti
Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

[Chorus]
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme)
Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosaga
(Wacha waseme)
Nimekupendea nini

[Verse 2]
Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno
Ila vitendo
Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno
Pasina vitendo?
Kiziwi, hata ukimwambia “nakupenda” wata hasikii
Ila vitendo oh
Wewe sijui sababu za kukupenda
Siwezi sema, ila utaona ah

[Pre-Chorus]
Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti
Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

[Chorus]
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme)
Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosaga
(Wacha waseme)
Nimekupendea nini

[Bridge]
Oh kama moyo ulisimama nlipokuona
Hukuongea, hukucheka, nilikuona tu
Na tabia sikufahamu, labda niache mwanadamu
Ukipenda usishangae ni upofu wa moyo
Kumbe moyo ulinirubuni, hukusema umependa nini

[Chorus]
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha waseme)
Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosaga
(Wacha waseme)
Nimekupendea nini