waya by Joh Makini


swiitch RuRroofer

(Intro)
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you
Eeeenhe ama gona halla at you
eeenhe

(Chorus)
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you

(verse1)
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki
Wacha izo mbana bwana
Me sina ma story mob story ni moko tu
Temana na zile mob story mitoko  tu
Story mikoko tu
Marafiki mapopo full
Demu full you wanajifanya wamelewa
Na kumbe wanastress za kuolewa boo
Subiri maisha yawapigie buuu
Nipe namba me nicome through
Makini sio aru aru
Nshazichanga changia mawazo tujenge ekaru
It’s been a looong time hustle
Tz JayZ raso
Wallah kwako mimi Nachotaka nilipaki
mazima mama k national park
baba k mama k I know you smart
joh nimebarikiwa wala sio kismat
you play smarter
rafikizo walisema nini it doesn’t matter
ulimbo nimenasa kaumbo ni swadakta
ulingoni sikuachi zile fimbo me nachapa
malingo ndo kabisa unazidisha nikikupata
deal zangu ndefu hazina ukingoni
natabasamu kama kidoti wa kingoniii
wapinzani hawaemi maji shingoni soo

(Chorus)
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you

(verse2)
hata walete compee compee
ushindani siogopi
mweusi ni kampuni
shori me silopoki na nikivuta waya
ujue nshajikoki
self made pesa ya starehe sikopi
cash flow kwenye mzunguko me sitoki
kesho haitakuwa na shaka  siongopi
poteza muda ila sio hii bahati
ati usinipotezee katikati binti
nipoteze kwenye moyo
mangi mtamu nitakuruhusu kuwa mchoyo
sikuja kula tunda nimekuja kupanda mbegu ya matunda
sisi tuwe mizigo maisha yawe punda
kwa lugha ya nyumbani nikuKunda
leo nimegonga lite kesho nitapenda
si unajua kupenda kweli sio kupendaga
vile unakaa ni co star kwenye hili movie
na vile me ni star haswa it’s gona be a movie shoreee

(Bridge)
ama gonna halla at you
ama gonna halla at you

(Chorus)
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Excuse me miss can I get your number
Can I get your number?
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you
Eeeenhe ama gona halla at you
ama gona halla at you

(outro)
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki 
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki
Na nikivuta waya waya
Ujue nshajikoki koki

…….beat plays till fade


hela by madeeit's time for manzese music baaby

(Chorus)
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa

(Verse1)
Habari zenu jamani
Na Hali ni gani
Mliopo duniani mna raha heeh
Game hatushindani na  hatubishani
Nani ni Bingwa wa raha heeeh
Siku hizi ela inakupa u star
Ni rahisi kumpinga hata Jah
Mwenye ela atakuhamisha Dar
Na akitaka hata jela utakaa
Hela imeleta hata vita imeua majita
Hali mradi balaa
Hela imevunja kanisa
Leo hakuna misa tunashinda bar
Yule kijana wa home sio star
Anatukana hata waliomzaa
Wivu tamaa na njaaa
Ukiendekeza juu ya kidole utakaa Llaa

(Chorus)
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa

(Verse2)
Hii dunia ni njia na nishapitia
Na nakaribia kusepa 
Wengi wanaisifia ila mi naichukia
Na naona ni ngumu pia kuikwepa
Basi nyinyi watoto someni
Ya akina wema kadinda komeni
Kesho mufike kule bungeni
Msiendekeze ya mabrazamen
Mengi nimepitia nikiwahadithia
Wengine mtalia sana
Ina mengi dunia usipoangalia
Watakutatisha tamaa
Eti Masaki kuna Mungu Watu
Nje Jongoo kumbe nani Chatu
Hivi nyie darasa la tatu
Mshaisoma hadithi ya kibantu Heeee Llaaa

(Chorus)
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa

(Verse3)
Enyi nyinyi wadada wa mjini
Mnauza chini mnataka nini hela
Siwezi weka akilini chumvini mimi
Alafu nikupe hela
Kama wewe una act Tom Boy
Hata kunshike kwa wapi huchojoi
Hata ufungue hii nati sienjoy
Nakula bati kuliko hata toy

(Chorus)
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa
Heeee laa

it's time for manzese music baaby

kemosabe by Fid Q

Niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/
Sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
Kwahivyo nikaenda Dar na treni… of thoughts../
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
Sikutaka kuivaa mikosi..nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport..password.. pin..lakini ni crack codes/
Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/
Je mimi ni kaka mubaya…? kaka aso haya../
KAKA..? huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka.. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/
Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui?
Mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball…. hata kwa mpira wa makaratasi/
Unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
Ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE.. life ni zaidi ya ku-have fun/
Kwani.. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/
Nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/
Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
Ndiyo.. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
Mie ni mbishi.. muulize Nikki – hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba