sumu by Fid Q

[Verse I:]
Aliyeniumba alinipa mdomo hivo nina haki kuongea
Hii bahati meotea, safi kamwe siachi kui-share
Hamtaki niwe fair, trust me man huwa happy nki-care
Naona watachosema mshkaji uko smart upstairs
Usiache kuongea, usiache we ni incharge huna spare
Kipaji ka' Ngwair, mapaji ka' bahati aliowagea
Flag pepea, hitaji zaidi ya maji na mmea
Ilikuwaje wa muache hadi mshkaji ulaji wa drugs ukamzoea
Tunamoka ili kusafiri kihisia
Au kufoka pia ikitoka ukaisikia huwezi toka au ukitose kuingia
Kinachochosha nia, ni kosa ulichojua utapatia
Nawachota kihisia, nasota, je inatosha fidia
Shibe ya mdau hainilazi njaa sababu mganga yupo juu
Nafurahi ambavyo wadau wakimuona star wanalamba miguu
Asiye nihitaji simuhitaji, kamwe simuachi aje azinzi
Bandidu kama tsotsi sipigi goti ka' PNC
Hakuna ambae hakosi, labda kwa
Yangu self esteem haitoki ka' ripoti za TMZ
Na hainizuii nsile mkate, kwa kuhofia kiungulia
Na u-Emcee hauniachi, huniangalia ka
Ka' Bruce Lee hizi karate, ntakupigia utaishia
Na sinto sita kusema ahsante au kuwasifia mkinisaidia
Washkaji baadhi hawana haki ya kui-pressure hii medulla
Wako radhi kukupa pombe na siyo pesa ya kula
Nawaona vyura tu kama Snura, hii sura ya mhuni haina kwere
massawe anavaa suti mtaani, nyumbani kunguni tele
Kwa magonjwa yanayotibika tunapoteza maisha, Huruma
Tunachanga kwenye msiba ukifa, hawajali ukiumwa
Au wanaweza wakahisi umekufa kwa kukutwa umezirai
Usipo sh'tuka Afrika unaweza kuzikwa ukiwa hai

[Hook:]
Sumu
Sumu, Sumu
Sumu
Sumu,Sumu

trumpet plays...
[Verse II:]
Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji
Ukinizuga kwa ulaji, nakupa fact kwa lugha ya kishkaji
Unataka vitu rahisi, mi' nawapa vitu halisi
Utata unamtaka ibilisi, na siyo bi kaka ka' Idris
Mr. Nice jua la utosi na mtaa unakiu ile mbaya
Hawamsupport, isipokuwa anawapromote aliowa-inspire
Wakati,sio kama Mox, Stosh hakupaswa kumgwaya
Lakini, mzee bila noti ni zaidi ya Nyoshi akiwa vibaya
I didn't come this far, just to come this far
Siwezi sanda kama bikra hata nikiishi ki-star
Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unachotafuta
Pesa sadaka, wazushi wanaivuta kwa
Binadamu wako wapi mnanitoa mie nsiwemo
Leo nawapa ofa ya mswaki afu kesho mnaning'oa meno
Oyoooo.. time is money nafasi haijali kuzuga
Wema anataka saa ya almasi zari anaujali muda
Washa sana nyasi, rasta ogopa fast futa
Wanashindwa kujinafasi kwa unafiki nafsi zinawasuta
Wabongo wa majuu hamna upendo, mnajigawa
Ubongo hauna miguu lakini skendo zina mabawa
Aliyemtia umasikini Afrika leo analia kwa yanayomsibu
Na hutangaza akimpa msaada kiasi cha kumtia aibu
Dunia siyo chafu ni chafu uchafu tukiutazama
Sumu ndani ya watu, na ndiyo hapohapo tunapokwama
Hawaamini kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili
Wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili
Cha kupewa hakishibishi ukipewa lazima ukumbushwe
Dunia mwendo wa ngisi, kung'aa sio lazima star ashushwe
Ukiacha hisia zikuendeshe, kwa ujeuri utaishia kufeli
Sababu neno la ukweli sio zuri na neno zuri halina ukweli
Ntasahau vyote, milele ntamkumbuka aliyeniumba
Na daily ntakaa mkao wa pusha tu kama Umbwa