picha by Songa


(Verse1)
Baada ya mishemishe na tabu,
Nikaamua nisiz counter nizizike gadhabu,
Ila cha ajabu,
Nikapokea message mtu simjui eti “Hi baby What’s up!?”,
Kabla sijamjibu nikacheki Picha,
(Whatsapp) nikaona sura ya mrembo aliyeumbika,(waooh)
Uzuri wake ni kama kajiumba mwenyewe,
Nika pose..nikamwambia waiter lete chupa nilewe,
Huku nikiiwaza hii text,
Ni kweli amekosea namba au anani test,
Ila haina Noma fresh,
Nikamjibu cool..huku nikisikiliza ngoma za Reks,
Mtoto akataka atume Picha,
Ili nimkumbuke anadai ni muda mrefu umepita,
Kiuhakika nikamjibu poa tuma nna imani zitafika.

(Chorus)
Whatsapp.. Facebook mpaka Insta!! PICHA,
Badoo.. Telegram mpaka Twitter!! PICHA,
Kila kona mazee nnayopita nakutana na!! PICHA,
Nakutana na!! PICHA,PICHA (rudia×2)

(Verse2)
Macho yangu hayakuamini,
Alivyotuma picha nikasema ni yeye au ndo camera 360!?,
Kwanza ni mzuri hupandi dau maskini,
Alivyo msafi ntatembea naye peku viatu vya nini!,
Mara akatuma PICHA na kimini,
Akaona haitoshi nyingine akapiga na bikini,
Mtoto ana figa kuuliza ana miaka 20,
Nikaahidi kuwa naye awaache vibaka wa mjini,
Akadai na PICHA zangu anazihitaji,
Mi nikatuma nilizopiga kwenye magari ya washkaji,
Nikajiongeza thamani ili asinione choka mbaya akanitema huku akisema ni mzugaji,
Basi mazoea yakazidi,
Tukapanga tuonane ili tujuane zaidi,
Siku ya kuonana nikaulamba moka na suti,
Ila nilivyomuona live tu Mwana nikatoka nduki.

(Chorus)
Whatsapp.. Facebook mpaka Insta!! PICHA,
Badoo.. Telegram mpaka Twitter!! PICHA,
Kila kona mazee nnayopita nakutana na!! PICHA,
Nakutana na!! PICHA,PICHA (rudia×2)

(verse3)
Mmmh…kwanza ngoja,
Nayosema ni kweli na sio kwamba vioja,
Kumbe ni bibi ambaye anajikongoja,
Na hata akisimama figa yake ni kama moja,
Mwenzenu sina hamu na Picha,
Kuanzia Whatsapp Facebook Instagram mpaka Twitter,
Yaliyonikuta kiukweli inasikitisha,
Nashindwa kujuta nabaki kutikisa kichwa. PICHA.


(Chorus)
Whatsapp.. Facebook mpaka Insta!! PICHA,
Badoo.. Telegram mpaka Twitter!! PICHA,
Kila kona mazee nnayopita nakutana na!! PICHA,
Nakutana na!! PICHA,PICHA (rudia×2)