TAZAMA RAMANI


 ...............................................................
       

1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2...

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

.......kutoka kwa admin nawatakia AMANI NA UPENDO VITAWALE KATI YETU WATANZANIA

4 comments:

 1. audio yake iko wapi mkuu

  ReplyDelete
 2. Nani mtunzi wa wimbo huu

  ReplyDelete
 3. Shukrani ni msaada mkubwa mno

  ReplyDelete
 4. KUNA BETI ANATAJWA KARUME MBONA SIJAONA?

  ReplyDelete