mathematics lyrics -Roma



Song:mathematics
Artist:Roma

It's beautiful day asalaam aleikhum Tanzania

Nimeshatikisa nyavu mimi ndo MVp
Wakakimbia depo kwa polisi wa ccp
Niliwapigisha kuruta kwata la JKT
Nna kipaji mimi kushinda cha T H T
Nawapangisha foleni kama bank ya NMB
Mimi nimesoma pcm sio pcb
So hata tufungwe mimi ni arsenal sio man yu
Kibonde we ni member wa loan board au TCU
Nchi imeuzwa vigogo wanapita ATM
Tuwakemee mafisadi wote wa ccm
kuvua gamba haiwasafishi mbele ya CUF 

chadema mwone Makamba Jk kwa tff
Sihitaji dancer wala mapanga yale ya tmk
Show zangu sio longolongo zile za y2k
na sio bandia kama lile kontena la BOT
Situkuzi kilichofake kama TOT
Mimi ndio roma ntasimama kama KKT
Asante bongo makejoo na mongo tbt
Mistari yangu mitamu kama miwa ya tpc
Na kwa hizi flow mamc mtalazwa kcmc.

Kodi ya walalahoi pombe ya tra
Miili yao ndio biashara ndani ya bba
Fataki anatoa mkopo ndani ya TIA
Mimba hazina uhakika mpaka DNA
Mhaya ishike elimu
Msambaa auze matunda
Mpemba avue samaki
Mnyakyusa avune mpunga
Aah aaah yaah rock city mikono juu yeeah
Mbeya city mikono juu

Mwambieni hatukuogopa tabiri za shekhe Yahya
Mahuti yangetufika bila kumpinga Jakaya
Sisaliti sirudishi kadi ya chama ka Nakaya
bado ainingii akilini hukumu ya babu seya
Wagonjwa wanakufa mapokezi
Dokta anakunywa value

Wazazi wanakufa labour wengine ICU

Wagonjwa wanakufa mapokezi
Dokta anakunywa value
Wazazi wanakufa labour wengine ICU
Waambieni me mzalendo na hii ndo mbiu ya mgambo
Tanesco wakizima umeme hupitisha mzigo wa magendo
Harakati za dokta ricky katika kuinua michezo
Mama Terry wamemsaliti mwasiti wamempa Tangazo
Lady pepeta hawavai msema kwel samunge
Mipira Hawaitumii eti kwa babu kuna kikombe
Mafuta wanapandisha bei kisa wanamiliki sheli
Wachina wanawapa tenda si tunanyimwa vibali
Gongo la mboto wanalia
Misaada wamewatapeli
Bandugu bwaga manyanga
Ayaokote magufuli
Pesa za ujenzi wa shule kala na mkewe headmaster
Thamani ya mabango ya kampeni somesha watoto veta
Wanajiuliza dkt slaa ni wapi anapata data
Hatakama nimevaa mlegezo ikulu napiga chata
Ikulu wamejaa vibaka manzese wanawakamata
Makahaba wanaongezeka boom linapokata
wanauziana kwa minada mali za serikalini
Mhasibu anachek porn si tumepanga foleni
Mmakonde chonga vinyago
Muha avue dagaa
Mmasai alinde geti
Mnyamwezi aline asali
Aah aah yeah A city mikono juu yeaah
Yeeah Iringa mikono juu

Mamc wanapata stress ROMA akitua ubungo
Tanga niliwafunga tatu nawafunga tano hapa bongo
wanafuga rasta ili wapate mademu wa kizungu
We mchaga kauze mitumba muziki
Ushakufunga pingu
Mistari yako meusi it's okey naipaka carolite
Katiba sio msaafu my people needs copyright
Vuta pumzi ya baba ila kwa pua ya kitusi
Na siachi kupiga goti mbele ya altare kasisi
Imamu akizini mjengoni usiukimbie msikiti
Padri akilala na sista aibadilishi ukatoliki
Hata gangstar ulegeza ulegeza macho ''waat'' ukimpa cotton buds
Mnakamata mateja wakati nyi ndo mnauza drugs
Ili ujue fegi imewaka lazma upige tafu
We baba usimtume mtoto aiwashe utamuua mapafu
Popote umuonapo ng'ombe jua hapakosi mmasai
Na Tongwe ndo ngome kongwe
Zanzibar msinitoe nishai
Ndoto zangu kitambo ilkua nije kuwa padri
Zikayeyuka nilipo puliziwa moshi wa weed
Naenda church naamka tena nasali
Napopote utakaponiona shingoni nimevaa rozali
Hip hop ni consious sio usharobaro kubeba nondo
Me natafuta pesa ya kula we unamchek tu alejandro
Unadhani utaandika nini kama sio hadithi za konongo
Me jamii inanihitaji kamuone babu wa loliondo
Magazeti yanauza kwa skendo za wasanii
Machinga wanauza copy cosota wamekula deal
Shabiki anaburn nyimbo na show anaingia free
Underground usile ada urekodi ongeza bidii
Mzaramo acheze vanga
Mkurya apige kwata
Mdigo atungue nazi
Msukuma achunge ng'ombe

Aah you know Tanga is mine
yeaah Tanga mikono juu




No comments:

Post a Comment