Baby madaha kugombania ubunge

Msanii Baby Mahada, amesema kuwa malengo yake aliyojiwekea ni kuja kugombea ubunge anauwezo mkubwa wa kufanya kazi hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hivi, msanii huyo alisema kuwa hashindwi kuwatumikia wananchi hivyo baada ya miaka kadhaa atakuwa katika mchakato huo. Alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya kutaka kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na vitendo vya baadhi wanasiasa kutowajali wananchi ambao ndiyo waliowapa dhamana. “Malengo yangu ni kuja kuwa mbunge na kikubwa ambacho nataka kukifanya ni kuwatumikia Watanzania, ambao kila siku wanalia juu ya wasansiasa ambao wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya maisha yao binafsi,” alisema. Hata hivyo mwandisi alimuuliza swali, msanii huyo kwamba atatumia chama gani katika mchakato wake huo, ambapo alijibu kuwa hataki kuweka wazi chama chake lakini muda ukifika kila mtu anaweza kujua.
Source:http://www.pekuatz.com/news/baby-madaha- ataka-kugombea-ubunge%E2%80%A6

No comments:

Post a Comment