Hatimaye MBUNGE JOSEPH MBILINYI (sugu) NA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS MEDIA GROUP wapatanishwa.


Hatimaye MBUNGE JOSEPH MBILINYI (sugu) NA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS MEDIA GROUP wapatanishwa.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.





Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia).

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. 

Ugomvi huo uliotokana na sababu za kimuziki ulianza takribani miaka miwili iliyopita

Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
(Picha na Anna Nkinda - Maelezo)


Alichosema Joseph Mbilinyi almaarufu kama Sugu muda mfupi baada ya upatanisho
‘’KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA KABISA…KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE…KUANZIA SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA KWA UTEKELEZAJI…HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZA…BAADAYE WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI 
YA WATU WANGU WA KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI HIVYO HIVYO…NA KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI…NA HATIMAYE SUALA HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE. TUNDU LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU… WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO…VITA YETU ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA…LAKINI NAOMBA NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO INAVUNJA JESHI LAKE…ASANTENI SANA

Alichosema Rugemalila Mutahaba muda mfupi baada ya upatanisho
''tumepanga mikakati ya jinsi tutakutana na mh. Sugu kuendelea kusaidia sanaa yetu hii ni kweli kabisa tumesaini bila shinikizo lolote, tunaamini sasa ni hatua ya kusogea mbele tuachane na yaliyopita'' 

Alichosema Dk. Emmanuel Nchimbi muda mfupi baada ya upatanisho
 ''wamekubaliana na kusaini kumaliza tofauti zao baada ya kikao cha mwisho cha upatanishi kati ya Ruge na mr 2 ambapo katika upatanishi huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kuamini kwambas upande mmoja hauutendei haki upande mwingine''

Alichosema Adili mmoja ya wasanii ambao wapo kwenye kundi la Anti-virus jana muda mfupi baada ya kupatana kwa Sugu (anti-virus) na Ruge (clouds media)

‘’Leo nafikiri WaTanzania watakuwa wamekuwa wameshudia na mpaka serikali imetuskia na wanaharakati wote mmefanya kazi kubwa sana, studio na maisha ya wasanii yatakuwa poa, na tulichokosa sisi watoto wetu watakikuta, Hii ni vita itaendelea mpaka mfumo utavyokaa vizuri, Anti Virus with No Apology movement inaendelea" na vinega wote hakuna ambae ataweza kuuza msimamo daima. Najua habari hii imewapa shock ila ni sign of victory...One love everyone...kinega4life’’ 

habari na michuzijr.blogspot.com na millardayo.com

No comments:

Post a Comment