KHADIJA KOPA AWEKA WAZI KUHUSU MALIPO YA SHOW ZAKE MWAKA JANA!


Tayari tukiwa tumezivuta zaidi ya siku 50 toka kuanza kwa mwaka mpya, Malkia wa muziki wa taarab Khadija kopa ambae mwaka jana alipiga showz nyingi sana nje na ndani ya Tanzania, amekubali kutangaza kiasi cha pesa alicholipwa kwa show za nje na idadi ya showz zenyewe.
Khadija amesema “nimefanya show nyingi sana zaidi ya 70 Tanzania na nje ya Tanzania mpaka nimeumwa, kwa ulaya kama Uingereza, Ugiriki, Holand na kwengine na kote huko kwa show moja nalipwa dola 2500 na huwa napunguza mpaka dola 2000″
mwanamama Khadija Kopa akiwa nje ya gari analolimiliki
Khadija ameweka wazi kwamba “muziki umenifanyia mambo mengi mpaka sasa, ndio nautegemea kwenye kila kitu , nina kibanda changu wanangu wanakaa pale Zanzibar, na kuna nyumba nyingine sijaimaliza iko Znz, nina vigari vyangu viwili Mitsubish na Noah, na ninatembelea Noah, nina mwanangu anasoma private anasoma form five, kula yangu mpaka wazazi wangu nawalisha kwa kazi hii hii”
Showz 20 za nje ya nchi alizofanya kwa bei ya dola elfu mbili kila moja, ameingiza zaidi ya shilingi milioni 60.

source:millardayo.com

No comments:

Post a Comment