MR NICE AONGELEA ALICHOKUTANA NACHO NDANI YA SIKU 14.
Siku 14 baada ya kuamua kuiuza sauti yake tena kwa watanzania katika single mpya ya ‘TABIA GANI’ iliyomrudisha baada ya ukimya wa miaka saba, Lucas Mkenda MR NICE ametibitisha kupitia millardayo.com kwamba mialiko ya showz aliyoipata mpaka sasa ni zaidi ya mitano, na kilichomshangaza zaidi mingi imetoka nje ya nchi.
Nchi zilizomualika Mr Nice baada ya single mpya ni Kenya, Rwanda na Burundi, na kwa upande wa Tanzania amepata showz kadhaa za mikoani ila ameshindwa kuzikubali mpaka atakapo itambulisha rasmi tabia gani kwa wakazi wa 88.4 Dar es salaam japo tayari ana mialiko ya Songea, Mwanza na Arusha.
Sababu nyingine inayomfanya ashindwe kuikubali hiyo mialiko ni pamoja na kusubiri kwaresma ipite kwanza, ambapo amesema “mapokezi ya hii single yamekua makubwa na kunishangaza, kweli kila mtu alikua anatamani kuona Mr Nice amerudi, nimekua nikipata simu nyingi wengi wameisikia Club, mwingine wimbo wako ndio ringtone yangu sasa hivi, kwa hiyo nimefurahi sana, najipanga tu kikazi, sasa hivi nina meneja zaidi ya mmoja, nina personal manager wangu na kuna mwingine anashughulika na mambo ya masoko tu, kuna mambo mengine ukiniuliza hata siyajui, hiyo ndio kazi yao”
http://millardayo.com

No comments:

Post a Comment