propaganda lyrics by FidQ ft Marco Chali




Song:PROPAGANDA
Artist:Fid Q ft Marco Chali
Producer:Marco Chali
Time:
Year:2011

(Chorus:Marco chali)
Polisi wanasapoti gangsta rap ‘’ili uhalifu uongezeke’’
Wabana pua kuimba mapenzi ‘’je itafanya ukimwi usepe’’
Media zinapromoti beef ‘’wanadai zinakuza muziki’’
Wadau wana wasanii wabovu ‘’nyie wakali mtatoka vipi’’
Hizi ni PROPAGANDA usiuliza ni nani?ili iweje?
Hizi ni PROPAGANDA utaibiwa ukicheza blanda
Yule last king of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda

(Verse: 1-Fid Q)
Machungu unapozimwa ili ufunikwe na  asiyeweza
Mbaya zaidi wanampa promo halafu kwenye  show umemmeza
Hautaki kuwa tatizo maana unaweza tatuka
Uwezi jua wapi nitatua ka jiwe gizani likitupwa
Wanaficha ili ili nisione wakati tayari nishajua
Hamkomi igeni nione jinsi msamba mnaupasua
Hivi mnaishi ili mle au mnakula ili muishi
Kumbuka a small leak will sink a ship
Mazingira hatarishi mabwana afya wana mapesa mob
Uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo
Ogopa kuoa haraka kama unaogopa talaka
Na ukivote in hurry ujue unatengeneza corruption
Maneno yao ni matamu lakini midomo yao inanuka
Ukipewa usisahau ukitoa toa bila kukumbuka
Usihofie kupitwa ilimradi muda haukuachi
Amini kesho itafika kama ipo ili uipate
Tunachukiana kwasababu tunaogopana
Tunaogopana kwasababu hatujajuana
Hatujuani kwasababu kwasababu tunatengana
Dunia ni nzuri walimwengu hawana maana

(Chorus:Marco chali)
Polisi wanasapoti gangsta rap ‘’ili uhalifu uongezeke’’
Wabana pua kuimba mapenzi ‘’je itafanya ukimwi usepe’’
Media zinapromoti beef ‘’wanadai zinakuza muziki’’
Wadau wana wasanii wabovu ‘’nyie wakali mtatoka vipi’’
Hizi ni PROPAGANDA usiuliza ni nani?ili iweje?
Hizi ni PROPAGANDA utaibiwa ukicheza blanda
Yule last king of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda

Verse:2-Fid Q)
Polisi huniita me mzururaji na wanajua me ni Mc
Kasha hunipa ishara kama wanavuta uradi kwa tasbihi
Baya lisilo nidhuru ni jema lisilo na faida
Nashkuru kote nasikika napotoa haya mawaidha
Kuanzia kata,tarafa,wilaya.mikoa hadi ngazi ya taifa
Nikifa siachi skendo nina uhakika nitaacha pengo
Kwa hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu
Pia ni kama Liberation struggle machoni mwa chegu
Ukiwa mkali kama marco chali raia watafeel tu
Wajinga ndo hufa kwa wiv sababu hawako real tu
Rafiki sio urafiki usipochanganywa na kazi
Mlango sio mlango mpaka ufungwe au uachwe wazi
Haupaswi kumuamini muongo hata kama akiongea ukweli
Ni dhambi kutumia dini kama njia ya kututapeli
Wanajiingizia kipato kwa kivuli cha misaada
Hawatufunzu tuwe viongozi labda  viongozi wakuwafuata
Utata uja tunapoanza kuwachunguza
Badala ya kuwafuata ndipo siri zinapovuja
Tunajenga tabia kasha tabia zinatujenga
Ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda
Kama umevutiwa na asali jiandae kukwepa nyuki
Huwezi kumtisha kwa mawe adui aliyeshika bunduki
Ni uchunguzi tu wa kisayansi ambao haukufanikiwa
Kama ule wa ng’ombe kula nyasi tu halafu anatoa maziwa


No comments:

Post a Comment