ALICHOKIJIBU AFANDE BAADA YA CHIDI BENZ KUMJIBU




Baada ya juzi CHIDI BENZ kukubali kwamba
 pamoja na AFANDE SELLE kumdis, yeye bado 
yuko tayari kufanya nae kolabo ambayo alipanga
 kufanya na Afande wiki moja au mbili kabla hajamdis,
 Afande nae ametoa sentensi ya jibu kutokana na alichosema 
ChidiBeenz.
Afande amesema “yeah mi niko tayari, niko pamoja nae Chidi
 anajua hilo, na hiyo kitu alishaniambia kitambo tukapanga na
 mimi bila shaka matatizo yaliyotokea ni mambo ya kupita lakini
 mimi wimbo wake hata kesho nasububiri beat niandike tufanye 
kitu kilichobora zaidi nafikiri itakua na maana kuliko malumbano 
malumbano yanayoendelea haya sio mazuri, sina beef nae”
Chanzo cha beef yao ni baada ya Afande kuhojiwa East Africa 
Radio na kufananisha kuondoka kwa Ditto  watu pori kwenda
 La Familia, sawa na kuondoka Manchester United na kwenda 
timu ndogo kama Bolton, maneno ambayo yalimkasirisha sana Chidi Benz.
story na milardayo.com

No comments:

Post a Comment