bado nipo nipo lyrics by MwanaFa

Wagwan Blood…
the personality change,…hii ya leo hii!
Hermy…


MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?

Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa
Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua
Mi nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia
ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa
napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu
kwani na mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu
watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao
wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao
sioi leo,sioi kesho-kutwa wala mtondogoo
sioi mchana,sioi jioni,usiku wala majogoo
morale nliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa
ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa
eti nizibe maskio
wengine nifumbe macho
nisione wakati naibiwa?
hamuwezi kuwa hamjalewa
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?

hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani?/
watu wana watu wao wengine toka zamani/
ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako/
wadogo usoni wanahifadhi wazee wako/
sijui ni dhiki au tamaa tu??/
watoto wanaanika njaa tu/
hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu/
msinipe headache/staki kufuata Mkumbo/
nyi anzeni mi niacheni,staki kufanya gamble/
marafiki wanauzana/ndio zao vicheche/
na daima wanateteana/usiwaamini usiniangushe/
anataka kuolewa na anamegwa kama kawa/
demu wako akiuza wenzake,zinduka nae analiwa/yes’
staki kuoa sababu staki kulia/
najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia/
nafahamu nna Bahati mbaya kama nalala na bundi/
ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi/
alilala na bibi arusi/siku moja kabla ya arusi/
na wala sio bwana arusi/bado mnanishauri arusi?/
eti nizibe maskio/
wengine nifumbe macho/
nisione wakati naibiwa??/
hamuwezi kuwa hamjalewa/

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?


usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania/
watu na akili zao washajichuuza na wakalia/
sikatazi watu kuoa/
na hata nikiwakataza neno langu sio sheria/
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri/
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa simu na gari/
inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri/
ndio maana mi nipo nipo sitaki kuvamia shari/
wanatoroka na wazungu/wanamegwa na vibabu/
wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu/
ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe/
au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe/
wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee/
haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume/
kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafkiria??/
sio kila demu umuonae unaweza muoa/
eti nizibe maskio/
wengine nifumbe macho/
nisione wakati naibiwa??/
hamuwezi kuwa hamjalewa/
mi nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi/
so miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini/

MwanaFA unaoa lini(bado nipo nipo kwanza)
Unasema(bado nipo nipo sana)
eeh (bado nipo nipo sana)
MwanaFa unaoa lini(bado nipo nipo mwana)
Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!!?
Outro
Yes yes…it’s yo boy FA
na Hermy B..ni kazi chafu but lazima mtu aifanye/
sipendi wanawake napenda wanawake wazuri/
wanaojitunza wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari/
yeeeeah,love is love my people/
ladies,behave basi/…au sio??

No comments:

Post a Comment