madaktari Nchini Kenya watunga wimbo kuhamasisha wagonjwa kutokwenda Hospital


moja ya mabango yanavyosomeka katika mgomo unaondelea nchini Kenya


mgomo unaoendelea nchini Kenya umechukua hatua nyingine kiasi kwamba madaktari nchini humo wamepuuza onyo lililotolewa na waziri wa huduma za matibabu Profesa Anyang la kuwafukuza kazi madaktari wote ambao hawatarejea kazini mpaka leo mchana.
Madaktari wameweka ngumu kurudi kazini japo wahudumu wachache wameonekana wakirudi kazini na pia kukitokea mgawanyiko kati yao, wengine wakirudi wengine wakiendelea na mgomo.
Madaktari hao wamebuni wimbo wao wa kuhamasisha wagonjwa kutokwenda hospitali, na baadhi ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huo ni  “wagonjwa msikujeeeee bado tunagoma, tunagoma, tunagomaaaa”

''kweli duniani kuna lugha mbili ambazo zinawezwa zungumzwa sehemu yoyote duniani na mswahili na mchina wakaelewana nazo ni MUZIKI NA MPIRA''

No comments:

Post a Comment