nimekasirika by Hamidu ft young D and mr.Blue

Bendera inapepea ikiangaza pande zote
hii ni gari inayosogea hadi ndani ya matope
Boom! kwenye air,  hewa ina cocaine
saluti segerea inayofanya watu wanyooke
Bora maskini ila sio kolombweha
ah, demu unayemuamini ndo atakupa gonorrea
niskize mimi uone kama utapotea
hii ni sumu juu ya ulimi afu mtoto amekolea
B:O:B mtu be! na D wa mtu che eh
hatuna dhiki ila sio daily starehe
mishemishe zikikubali party inaanza day break
Vichwa vya msumari, boya boya stay back!
siogopi Mic naeza chana hata Msibani
Hizi vocal za fataki zina hustle darasani
Na swagger ni marashi beat inatoka pwani
Nyimbo inatoka classic sound ka Miami


Nimekasirka!
Nataka niwape flow, na niwapake chalk
wakilisha watu wa ghetto na wasaka dough
nataka niwape flow, mpaka mwisho yoh
now ma baby kwenye floor C'mon let's go
Nataka wenye chuki zao waende likizo
wakilisha TZ chama la bongo
wakilisha yoh, sababisha yoh
vagamisa mpaka mwisho wa maisha yoh


Flow zangu dili kama Bomu za mogadishu
Piga simu leta dili acha bifu
japo watoto wananibip mi ni jembe wao ni visu
I was born 19:87 huku nakaa nyamala
nilianza hustle mdogo mdogo wakaniona fala
Nimeanza ku'make dough kabla ya kujua ku'flow
so, haini'Pain nikikosa kufanya show
Mi ni mjeshi commando ha!
Nashika bango naitangaza namba yangu right? 26!
sina mpango nawanao fagilia maisha yangu right? 26!
wanao sniff na ku smo' (smoke) mi ndo nnao wa control
kitaa kinaaminia mi kiboko ya  mabishoo
Ninja, ringa mbele ya dada zako uone unavyochekwa ujinga
sina sifa ya kuringa, nimepinda
sema kwa kusaka dough,
nta'hustle mwanzo mwisho mpaka mnipe ukomandoo
Mi ni solja sina moyo wa kungoja
Namshukuru muumba
kila nnapo pita nasifika nakubalika sifuasi kusadikika najua binadamu sijakamilika
niliowakosea mnisamehe, na dua njema mniombee
sitoacha kuwakilisha lile chama la wavuja jasho
ambacho
Ninacho sina, sina nnacho, nnacho sina, sina nnacho
nnachokiwaza kichwani mwangu
sipendi kumueleza kila mtu matatizo yangu


Nimekasirka!
Nataka niwape flow, na niwapake chalk
wakilisha watu wa ghetto na wasaka dough
nataka niwape flow, mpaka mwisho yoh
now ma baby kwenye floor C'mon let's go
Nataka wenye chuki zao waende likizo
wakilisha TZ chama la bongo
wakilisha yoh, sababisha yoh
vagamisa mpaka mwisho wa maisha yoh


No comments:

Post a Comment