kabwela lyrics by stamina ft rich mavoko


nimepigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi
maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli
dunia tambala bovu nalidekia kwa shida
jitahidi kui'solve bila kutumia four figure
natamani nisimame ili nione magharibi
moyo umejaa ukame kuhema unajitahidi
macho yote yana ukungu utadhani chungu cha bibi
nataka, kumuomba mungu shetani ananzidi spidi men
vizuri viko wapi navisaka havionekani dah
napata makapi vinono navitamani
sina baba, sina mama, sina babu sina bibi
uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi
umaskini unanipodoa, bila kutumia cosmetics
daily unanizodoa, unanivuta bila magnetics
maisha yangu hayana swagga kama mmasai wa Njiro
Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo
dah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela


sikusoma, kitajiri kichwa kimejaa madufu
maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua lufufu
naichora, lami na mkaa kwa kudhani nitaona chochote
atleast, basi ningekaa nisingeitwa kiokote
pesa imegeuka yuda, daily inanisaliti
mishale inazidi muda, utajiri unaninyima seat
maisha kama gwaride, kuna wa mwisho na wa kwanza
ikisikika nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza
taifa la kichwa changu Raisi wake naona kichaa
na kitabu, cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa
ah, napatwa wazimu shida zinanitia madoa
pesa imekuwa adimu kama bikra kwa changudoa
banda nnalofugiwa sihemi halina dirisha
wasichana wananikimbia wananiita nyoka wa kibisa
msosi wangu sio wa drafti sili mpaka nijitume
maisha yana super shaft yashanizidi nguvu za kiume
dah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela

(http://www.thebongolyrics.blogspot.com/)

ushindi wangu ni wa uchafu kwenye vita ya wasafi
kila nnayemuomba tafu anataka afanye na ulafi
maisha ni kombolela masikini ndio mlinda kopo
cha msingi ni kuunga tela mpaka utoke kwenye msoto
kila jua linapozama natamani pasikuche
hasi inageuka chanya kapeto  anageuka sunche
naona alama za mlango ila sioni pa kutokea
hii pesa imetoka jando inataka kuni-babu seya
nimegeuka konokono natembea na  mzigo wa shida
silali, nimekuwa pono maisha unakwenda na mida
shida zishanipa ustaa, zaidi ya kanda ya loketo
tumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto
vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani
na vijiko vya uhalifu nishaviweka kwenye sahani
mi nadhani, haya maisha yana ramani
na aliyewachorea masikini peni ilimgomea njiani
ah

leo nimepata kesho nimekosa
nnachohifadhi maumivu tu
life ni ngumu bado inanichosha
nakula mbichi sili mbivu  boo


huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela
huwezi amini bado kabwela
sina uhuru kama niko jela

2 comments:

  1. Mistari imekomaa...hii ngoma haina mpinzani

    ReplyDelete