mwaka jana lyrics by Izzo business ft shapsin

2011 nakuchukia, ulifanya niporwe demu kisa pesa sikuwanayo
zilizagaa kila sehemu, konde nilipiga moyo
ulimtesa baba yangu kutwa kushinda mahakamani
uliuvuruga ubongo wangu, chuo sikutamani
mwakyembe akawa hoi, na sichoki kumuombea
2011 na hapa nakuchukua, Mr ebo kama ndoto, leo hatupo nae
five star matumbo joto, pengo lao nani akae
bora upite bora uende, tuliobaki tusonge
umetesa wamachinga, japo mbeya nyumbani kwangu
jangwani na mafuriko, labda mipango ya mungu
umeleta marafiki, japo wengi siwaelewi
wanafiki, kuzua hawachelewi
pesa nyingi ulizuia, hata katu sikupata
jina tu lilinisaidia kwenye viwanja vya bata

nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!

wengi wao hawaamini, japo kocha waliletewa
taifa stars wapewe nini ,kwenye challenge wakazomewa
ghadaffi king wa libya, leo hawapo naye
afghanstan nako msiba, Osama hawapo naye
2011, mwaka wa vioja
sio kwako labda kwangu, na haya mawazo yangu
nilipata simu ya vitisho nkatishiwa maisha yangu
ah, usinikoshe naapa kwa jina langu
masoko ya biashara vya vilio vilitawala
kila siku tu moto, masoko yanaungua
wakubwa mpaka watoto mabomu yanawalipua
nazungumzia gongo la mboto, nani asiyejua
marlaw kaweka besta ndani, basi iringa oya oya!
leo niko na manecky, na ngoma iko on fire
diamond mtoto wa tandale sio kwa uchawi wala ndumba
labda yalimcheza machale akatoa pete ya uchumba

nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!

niko hapa swagga zangu ziko full bro
yes business and i run the show
they like what, what more
baada ya keshokutwa, ni mtondogo
niko hapa swagga zangu ziko full bro
 yes business and i run the show
they like what, what more
baada ya keshokutwa, yo mtondogo

nikiwa street na machizi tume'chill tunabonga tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa club na sina habari na mitungi napombeka tu
nakuchukia mwaka jana!
nikiwa ghetto na my baby tuna'hug na kudance tu
nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!
nigga i hate you, nakuchukia mwaka jana!

[Shapsin]
wabongo walikosa heshima takwimu zinaonyesha tu
labda kwasasa ndo lazima maana wanawarudisha full ah

No comments:

Post a Comment