mia lyrics by mtu chee


Mtu chee! haha, Young Dar es salaam
Country Boy na Staminah! haha

[Young D]
yeah
ah sina hela, ila siwazi biashara ya karanga
ma alijua nitakuwa sela, tangu niko mtoto mchanga
akaniambia, nitatoka nikijipanga
daddy pia alinihusia, nisioe demu wa kichaga
nikamwambia maisha ya karata
akaniambia nani anachanga
ha nahisi napiga picha na yesu
mara naota nahitajika sana kwetu
njia safi ila naogopa kwenda peku
nishakunywa maji ya baraka, huwezi nipa hukumu
mi ni paka rapper ukinifwata, ha! nakupa pumu
kila ninapopita, naona pagumu
nimepigika afu sina majukumu
oh ona, life sio easy bila speed lazima uteseke
im so busy busy hadi nashindwa kuwa kicheche
napenda rasta niichore nna rangi nyeusi chache
napenda kuwa mlokole where the church at?

kuanzia ilala temeke hadi ngarenaro, 100!
kijenge juu niko kwa masharobaro, mia!
whats up jembe? hii track b'ana iko, mia!
ka vipi iitwe..mia, mia, mia!

kinondoni masaki hadi kigamboni, mia!
tandale hadi kimara makoroli, mia!
whats up jembe? hii track b'ana iko, mia!
ka vipi iitwe..mia, mia, mia!

[Staminah]
ah mi ndo jua la utosini, sizuiliki na miwani
ukitaka battle na mimi, omba kibali kwa diwani
usijisifu una mbio, sifu na anayekukimbiza
ndio nazifanya sio, hadi mwanga unaogopa giza blaza
mziki una graph, we shuka ninapopanda
kwa hizi tenzi nawa'surf bila bundle na wanasanda
mi kinyesi kwenye bafu huogi bila kunitoa
mnaojiita mna level chafu hizi Jiki zinatia madoa
mziki mechi ya viziwi, siuchezeshi na filimbi
mchezo hautabiriwi, pweza ameshanipa ushindi
kocha kavunjika nyonga, kepteni naongoza ligi
huu ndio mlima wa kitonga we reli usije kwa spidi
ah , Boomshakaraka walio chini wataningojea
sio prrrrr mpaka maka sitelizi nikapotea
staminah, nasukuma kete hata dafti waliweke bondi
muosha maiti bora usepe leo umepewa maiti ya zombie
ah

Iringa na tanga zenji mpaka bagamoyo, mia!
Mji kasoro ndani ndani kwa mkoyoyo, mia!
whats up jembe? hii track bwana iko, mia!
ka vipi iite..mia, mia, mia!

Rchuga na mwanza mbeya mpaka musoma, mia!
DSM Dodoma mpaka Kigoma, mia!
whats up jembe? hii track bwana iko, mia!
ka vipi iite..mia, mia, mia!

[Country Boy]
ah ili unijue inabidi  uwe spy kama ndama unisumbue
baadae kwenye game we kamanda na ugundue
wenzako wanashuka mi napanda nifafanue
kuna tofauti ya kati ya shuka na sanda
conscious rappers tuko wachache wengi wao hawako real
kwa hizi stanza waache wadate mpaka haters wata'feel
yap, women lie men lie, know  i speak the truth
na sober boy siko high straight ndani ya booth
mistari yangu kama kisu fake emcees nawakeketa
wakijitusi tu wakijileta mi nawatwanga nawapepeta
nahitajika, sio kimapenzi nichokwe kama shetta
nina uhakika, kama deal kimziki si tunapeta na kuandika
mpaka peni imeanza tetemeka, na imebainika
tangu nitoke wengi wao wanateseka, ninatafutwa kama hela
utaponiona we niokote, mziki kama mkate wa bwana so inabidi tule wote
niaje gangster, sharobaro tupieni kiduku
washtue, machizi wa ngarenaro leo mambo iko huku
hii track, basi iitwe mia
nyie wanafiki imewateka
wanaogopa kushangilia huku vichwa vyao vinanesa
C'mon

until mashabiki ma'promoter wa muziki, mia!
machizi ma'miss na marafiki, mia!
whats up jembe? hii track bwana iko, mia!
ka vipi iitwe..mia, mia, mia!

aka mi na'underground wote na ma'legendary, mia!
gangster, snitches na ma'ordinary, mia
whats up jembe? hii track bwana iko, mia!
ka vipi itwe..mia, mia, mia!

hehe as usual, we create they follow
mtu chee we in the house baby
manecky, this beat is the real thing
aight, ah, FBaby!

1 comment: