Dear God by Kala Jeremiah

Intro:
Rock town records
Dear God let me to talk you
cause am in jungle God
I need your help
I watch my back
I see myself!!


Verse:
Asante Mungu leo ni siku nyingine
nakuja mbele yako baba nina ombi jingine
Baba wewe ndo kimbilio sina tena mwingine
si unacheki sina furaha kama watu wengine
Wengine wanakula bata na kusaza zingine
mimi bado niko ziro na masela wengine
Pengine labda umesisahau au umenichoka pengine
lakini hapana we sio kama viumbe wengine
Uliniumba wewe baba sio mtu mwingine
tena mimba yangu ililelewa na baba mwingine
Baba alikua busy na mademu wengine
nimeshamsamehe mwambie ana mtoto mwingine
Mwambie nampenda sana sina baba mwingine
mwisho wayote mlaze pema kama watu wengine
Tukiachana na hayo nina mambo mengine
baba mziki wangu ndio tatizo kubwa jingine
Nachana sana promo wanapewa wengine
wengine wanasema niende kwa mganga pengine
Lakini mi nimebatizwa kama wakristo wengine
naijua Biblia zaidi ya vitabu vingine
Mungu wa islael Mungu wa mataifa mengine
Mungu wa Yakobo Mungu wa Isaka Mungu watu wengine
Usikie kuomba kwangu unipe njia nyingine
Naombea watoto mayatima na wenye shida wengine
Wananchi maskini na tabaka jingine
Mungu baba tupe neema kama nchi zingine
Watembelee mafisadi mmoja baada ya mwingine 
wakumbushe kula kwa jasho kama watu wengine
Ona mpaka nasahau mengine
baba ajira zipo chache hawapati wengine
Vijana wanakula unga hawana kazi nyingine 
dada zetu wanajiuza wengine
Pengine labda ndio sodoma na gomora nyingine 
wanaume sikuhizi ni mashoga wengine
Wanadai haki zao kama haki zingine
wanaandamana hadharani mataifa mengine
Wanaoana kwa harusi kama ndoa zingine
tuachane na hayo masuala nina swala jingine
Hivi ni kweli umewatuma manabii wengine
maana kila kukicha kuna kanisa jingine
Huyu nabii na huyu ni nabii mwingine
huyu anaponda na huyu anampinga mwingine
Wanahubiri kuhusu pesa sio kitu kingine
toa ndugu toa toa ulichonacho kingine
Mungu nionyeshe njia nioneshe ishara nyingine 
yapo mambo mengi tu siwezi taja mengine
Hata demu wangu nahisi ana mshikaji mwingine 
mana kabadilika kawa kama yule mwingine
Niliyemfuma live akiwa na boya mwingine
nisamehe dhambi ya kuzini sina dhambi nyingine
Mwokozi wangu niongeze pesa zingine
rafiki zangu niongeze tena wengine
Wawe wote waukweli sio masnitch wengine
wakuchukua siri na kuvujisha kwingine
Naombea madaktari waongezwe posho zingine 
ili usije kutokea mgomo tena mwingine
Mana walikufa watu wasije wakafa wengine
mwisho wa yote nashukuru kwa uhai mwingine
Ninajua sahizi watu wamelazwa wengine
rafiki zangu walishagongwa na magari wengine
Kama Farook Warango na machizi wengine 
mlaze pema Kanumba na rafiki wengine
Tutaonana Yesu akirudi kwa mara nyingine 
asante sana kwa baraza jingine
Japo magamba yamevuka yakabaki mengine
classic moja ina watu wengine
Wanadai nchi imeuzwa kwa jamaa mwingine 
Sajuki Vengu na wagonjwa wengine
Wanyooshee mkono wako wape Afya nyingine
Ameen!!

No comments:

Post a Comment