nishike mkono by Darasa ft Winnie



(intro;Winnie)
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono

Nishike mkono

(verse1)
Mwili kama unavidonda ukinigusa tu naumia
Kichwani mzigo wa dhambi gunia kwa magunia
Dunia sinia pakua unachoweza
Rudisha kwenye njia walimwengu washanipoteza
Mpaka leo mwanangu yupo magereza
 mtoto wa jirani anasomeshwa uingereza
baba ake athumani amekufa mvuvi wa pweza
wana utajiri wa imani masikini wa kifedha
Washanichimbia kaburi wanizike nahema
Washakata miti ya kivuri mifereji ya neema
Unaeza kuta unaemwamini ndio anakuwekea sumu
Hawana alama binadamu wanaokuja kukuhumu
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea

(chorus:Winnie)
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono mkono

(bridge:Winnie)
kumekucha nipo njia panda sioni hata pa kuelekea
na kiza ndio kinatanda niendako nani wa kunipokea
nishike mkono nishike mkono
 nishike mkono nishike mkono
 nishike mkono nishike mkono mkono

(verse2)
unajikuta uko peke yako giza kubwa kwenye mtaa
huoni ndugu wala jamaa uliokuwa nao jana baa
mawazo ya karaa nafsi inakosa raha
upepo mkali na baridi bila koti la kiuvaa
unauliza mungu yu wapi akuonyeshe njia
kelele za uchungu na hakuna anayekusikia
usitamani kiatu changu ukikivaa hutembei
ikiwa siku mbaya ndio masaa hayatembei

(chorus:Winnie)
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono mkono

(verse3)
imagine maisha ya mtoto bila ya mzazi wa kumlea
nambie ndoto za wangapi mtaani zimepotea
imagine mzazi wa lulu maumivu aliyojibebea
sometime tunaishi nje ya malengo tumejiweka
kifuani kama kuna moto moyo wangu unaungua
maumivu nayoisi usitamani kuyajua
nashindwa kupiga hatua muoga nasua sua
maji yakiwa shingoni ndio tunakumbukaga dua
nashindwa kuchagua kati ya mvua na jua
kuna kitu kimemis nawaza kukigundua
natamani kuwa mtoto kibaya aiwez kuwa
vazi la dhambi nilovaa halitakati hata nikilifua
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea

(chorus:Winnie)
Nobody see me cry all I know
Nobody by my side Mungu nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono
nishike mkono nishike mkono mkono


No comments:

Post a Comment