nakata kiu by I'c ft Shesheman Sam
Intro
(Shesheman Sam)
So brother do you think they need to here this?
(I’c)
Yah they gotta hear this…
(Shesheman Sam)
Are you sure about this?
(I’c)
Yah I’m…
(Shesheman Sam)
Are you certain about this?
(I’c)
Positive…
(Shesheman Sam)
Ayt…

Verse 1 (I’c)
Maisha yana bana, labda kama chatu…
Vunja mbavu ya kwanza, ya pili nay a tatu…
Hawana huruma waone tu hawa watu…
Tulio wachagua tukijua hawawezi wakawa viatu…
Kila day, Mangi anapandisha bei…
Siwezi mlaumu nafahamu hali inatisha aise!
Maji yanakatika mwezi, hii hali ziiwezi
Mwalimu alipinga dhuruma, mnachekea wezi…
Foleni imesimama, je unasikia wimbo wa taifa…
Siupati hata kwa wifi ni miundo mbinu haifai…
Watu wanaangamia, yako wapi  maarifa…
Niyafwate, I’m gon’ roll up, Wiz Khalifa…
Umeme wa mgao kipande chetu kidogo…
Na nikama hawakioni hawa wetu vigogo…
Walituahidi vingi leo wanatupa visogo…
 

Chorus (I’c)
 Ni mchakamchaka tumekosa likizo…
Kila day tunazisaka na ni kama igizo…
Hivyo niite Martin Luther sina time niko…
Kwenye harakati ka’ Abraham Lincoln…
Oooh Nakata kiu… X 8

Bridge (I’c)
Nili kaza mkanda nikiingoja kasi mpya…
Nabana tumbo bure bora niji nafasi upya…
Twaenda mdogomdogo pengine twarudi nyuma…
 Kila leo bora ya jana na sio kwamba juhudi hatuna…
Oooh Nakata kiu… X 8

Verse 2 (I’c)
Ukimwacha Malkia pekeyake kwenye kichugu…
Hakioti tena umelizwa kama unamenya vitungu…
Hatuwezi endelea hata tuongozwe na Obama…
Bila uzalendo zaidi ya Maalkaida wa Osama…
Mnawaza uShaloMilionea, Oh mama (RIP)
Ila inabidi kujituma saka Dough bana…
Plus tusali sana, Haleluya, Hossana…
Ajira hakuna, jiajiri mwenyewe…
Waliisha toa mikopo sa mnangoja nini mpewe…
Wamewalisha nakuwatafunia sasa mmezewe…
Hamjatulia (woof woof) achampepewe…
Fungueni macho ama nyuma tutarudi jamani…
Au kuzunguka humu ka Wayaudi jangwani…
Njoo tuzisake, toka kwenye maficho yako…
Kwani asie na kitu atanyang’anywa hata alichonacho…
 
Chorus (I’c)
Ni mchakamchaka tumekosa likizo…
Kila day tunazisaka na ni kama igizo…
Hivyo niite Martin Luther sina time niko…
Kwenye harakati ka’ Abraham Lincoln…
Oooh Nakata kiu… X 8

Bridge (I’c)
Kenye Kampeni wanasiasa wanatunga uongo…
Na nyie mwanishangaza mnapowaunga mkono…
Mnauza kura nawakipita mnapunga mkono…
Ati usicheze mbali, unga robo…
Oooh Nakata kiu X 8

No comments:

Post a Comment